Hivi Azam FC mpo serious kweli?

Hichilema

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
1,039
940
Kitendo cha timu ya Azam Fc kugomea mechi ya kirafiki kabla ya kuisha kisa maamuzi mabovu ya mwamuzi kinaonesha mlivyo na utoto. Lengo kuu la friendly match ni kupima mbinu na utimamu wa mwili, kwa nini mkimbie?

Na leo mlipaswa kuwa na mechi dhidi ya Club Africain naambiwa mmeisusa kisa droo ya CAFCC inaonesha mnaweza kukutana nao round ya pili. Jana wakati mnacheza Club Africain walikuwa uwanjani kuwasoma kwa ajili ya mechi ya leo. Mnadhani kuna kitu mmeokoa? Hakuna.

Huyu kocha Msenegal na wasaidizi wake kutoka kwao hawatawasaidia kitu, kikosi pia ni kidogo na kinakosa quality kwenye maeneo muhimu kama beki wa kati, beki wa kulia, kiungo namba 10/8 mzuri na winga wa kulia.

Msipobadirika hata Waethiopia hamuwatoi na ngao ya jamii Yanga akipenda atawakandaa na ligi hamchukui. Muda ni mwalimu mzuri.

Pia soma: Azam yagomea bao la 4 huko Tunisia, yasingizia refa alikuwa na upendeleo
 
Kama hawako serious si ndo vzr kwa SSC na YNG... league iwe nyepesi
 
Timu ya Azam ina utoto mwingi. Yaani hapo wakichogomea ni kuepuka aibu ya kupigwa goli nyingi wasitrend kwenye mitandao. Kuna timu imepigwa 27-0 na Bayern lkn walimaliza Mechi na wakagundua makosa yao.

Kesho wakicheza watakuwa tofauti. Miongoni mwa faida za kuonewa kwenye Mechi ya kirafiki ni kuzoea figisu za Mataifa ya kaskazini.

Waarabu huwezi kiwafunga kama unazirazira. Kwenye CAFCC atakutana na St George na huenda CA ya Tunisia. Atawezaje kuhimili figisu kama Mechi ya kirafiki tu anaanua tanga?
 
Wamekuambia Mchezaji wao kavunjwa mkono... tena Friendly Match... ulitakaje wkt walishaona Game imetoka nje ya malengo yao?
Mbona friendly matches nyingi wachezaji wanaumia? Man u vs Arsenal(Amad Diallo), Man u vs R. Madrid (K. Mainoo) mbona hawakutoa timu?
 
Kitendo cha timu ya Azam Fc kugomea mechi ya kirafiki kabla ya kuisha kisa maamuzi mabovu ya mwamuzi kinaonesha mlivyo na utoto. Lengo kuu la friendly match ni kupima mbinu na utimamu wa mwili, kwa nini mkimbie?

Na leo mlipaswa kuwa na mechi dhidi ya Club Africain naambiwa mmeisusa kisa droo ya CAFCC inaonesha mnaweza kukutana nao round ya pili. Jana wakati mnacheza Club Africain walikuwa uwanjani kuwasoma kwa ajili ya mechi ya leo. Mnadhani kuna kitu mmeokoa? Hakuna.

Huyu kocha Msenegal na wasaidizi wake kutoka kwao hawatawasaidia kitu, kikosi pia ni kidogo na kinakosa quality kwenye maeneo muhimu kama beki wa kati, beki wa kulia, kiungo namba 10/8 mzuri na winga wa kulia.

Msipobadirika hata Waethiopia hamuwatoi na ngao ya jamii Yanga akipenda atawakandaa na ligi hamchukui. Muda ni mwalimu mzuri.

Pia soma: Azam yagomea bao la 4 huko Tunisia, yasingizia refa alikuwa na upendeleo
Nimeangalia clip clip za ile game aisee ule moto walokua wanapelekewa sio mchezo ,wale madogo wa kialabu hawakua na Nia nzuri kulikua na goli ata 7 pale
 
Wamekuambia Mchezaji wao kavunjwa mkono... tena Friendly Match... ulitakaje wkt walishaona Game imetoka nje ya malengo yao?
Hamna kitu ndugu yangu ile game walizidiwa Sana ..
Wanajitetea t wale watt wa kialabu waliwazidi kila kitu hasa speed wachezaji wa azam wengi walionekana wazito sana inaweza kua sbbu ya mazoezi magum,
Walikua wanakimbizwa sana
 
Wamekuambia Mchezaji wao kavunjwa mkono... tena Friendly Match... ulitakaje wkt walishaona Game imetoka nje ya malengo yao?
Kama ni hivyo basi hata Yanga nao wangetoka uwanjani kule Malawi baada ya mchezaji wao Dennis Nkane kuumia.
 
Back
Top Bottom