Hivi askari wa Moshi na Arusha hawatoshi?

R CHUGGA

Senior Member
Nov 28, 2011
124
13
Leo asubuhi nimeona msafara wa magari manne yaliyojaa askari na gari la maji ya kuwasha yakielekea njia ya Chalinze-Segera nilipofuatilia nimegundua ni askari wa Ukonga na wengine wa Pwani na wanaelekea huko Arumeru kwa ajili ya ulinzi.
Ndo nauliza inamaana hao askari wa Arusha Moshi hawawezi kuimarisha ulinzi hapo Arumeru?
kazi ipo huko!!
 
matumizi mabaya ya fedha za umma wakati askari haohao hawajalipwa malimikizo ya stahiki zao
 
Nahisi harufu ya damu ya watanzania wasio na hatia huko Arumeru...

Said Mwema umeua watanzania wengi sana kupitia jeshi lake, latest in wa5 Songea, usiende kuua wengine Arumeru acheni wananchi watumie haki yao ya kidemokrasia kuchagua mbunge wanayemtaka na sio kuwapelekea vitisho. Jiandae kujibu mashtaka ya mauaji yote haya baada ya 2015 wenye nchi tutakapoikomboa toka kwa wakoloni weusi CCM
 
Leo asubuhi nimeona msafara wa magari manne yaliyojaa askari na gari la maji ya kuwasha yakielekea njia ya Chalinze-Segera nilipofuatilia nimegundua ni askari wa Ukonga na wengine wa Pwani na wanaelekea huko Arumeru kwa ajili ya ulinzi.
Ndo nauliza inamaana hao askari wa Arusha Moshi hawawezi kuimarisha ulinzi hapo Arumeru?
kazi ipo huko!!

Kama kweli balaa.
 
Nina rafiki yangu ni mjeda!! kila wakati wa uchaguzi huwa wanaenda zenji kusaidia kuiba kura!! Hata hao FFU watakuwa wamelamba bingo za kutosha ili kuilinda CCM ishinde kwa hali na mali kama wenyewe wanavyopenda kusema. Subiri tuone! Safari hii patachimbika!!
 
Je wakati wa uchaguzi mkuu watafanyaje maana kila jimbo litahitaji askari wa kutosha pamoja na gari la maji ya kuwasha! watakodi toka nchi jirani?
 
Wanaenda kusaidia kuiba kura!ndio maana hukataza wananchi kulinda kura eti wakae meta 100!
 
Nna ndugu yangu polisi singida,ananiambia kuna askari mia mbili akiwemo yeye watatia timu hapa jimboni.
 
Je wakati wa uchaguzi mkuu watafanyaje maana kila jimbo litahitaji askari wa kutosha pamoja na gari la maji ya kuwasha! watakodi toka nchi jirani?

Simple, uchaguzi mkuu unakuwa rahisi kuiba kura kwani kila watu hubakia kwenye majimbo yao kulinda kura na hivyo kujikuta wanazidiwa nguvu. Ila uchaguzi mdogo kama huu ni kuwa wananchi wote wapenda demokrasia wanajitolea kwenda jimbo moja kuhakikisha haki inatendeka na hivyo kuwapatia wakati mgumu sana wachakachuaji CCM, na hivyo kuamua kutumia mabavu ikiwa ni pamoja kuua raia wanaotetea demokrasia yao.

CCM haichomoki Arumeru bila kutumia nguvu za dola. Haitashinda uchaguzi bali watafanya mapinduzi ya matakwa ya wananchi. Na haya ni maandalizi ya mchakato huo. Kama kila kitu kinafuatwa na kinafanyika kwa uwazi na ukweli hatakufa hata sisimizi.

Simba na Yanga ni wapinzani wakubwa sana lakini kwa kuwa huwa wanashuhudia kichapo cha halali uwanjani huwezi sikia wameuana. Ila kama refa atapiga filimbi ya penalty wakati faulo imefanyikia kwenye centre circle hapo ndipo utakapoona kuwa bila ya kufuata haki na kanuni za mchezo zinazokubalika kisheria hakuna amani.
 
Afande mwema huku askari wako wakija waelekeze upole na utu,hawa wameru ni tofauti na raia wa arusha mjini.ni vyema Chagonja akaingia mitini mapema...mpeni kazi ya uratibu huku Kamanda basilio matei mana anasikiliza pande zote,mstaarabu
 
matumizi mabaya ya fedha za umma wakati askari haohao hawajalipwa malimikizo ya stahiki zao

wanajua wajanja wa moshi na arusha hawawezi kufanya ujinga wanaoutaka. Ndo maana wanapeleka wazaramo na wakw.ere. Wamesahau kwamba hii italeta chuki kwa polisi wa maeneo husika na kuendelea kukosa kura.
 
Nimeshuhudia magari yenye maji ya kuwasha yakiingia kituo kikuu cha polisi Arusha.

Inawezekana polisi wanajiandaa kuwahadaa wana wa nchi, hasa Wameru wakati wa kampeni. Hii inadhihirisha udhaifu na uvivu wa kufikiri kwa viongozi na watawala wa nchi hii.

Inasikitisha kuona serikali inatumia nguvu kubwa, gharama kubwa kwa ajili ya chaguzi ndogo. Inadhihirisha pia kuwa hii nchi inaongozwa kidikteta.

Where is the freedom of democracy? Where is the people's will? Where is the equal distribution?
 
Si mbaya sana kama yakiwepo hapo arusha mjini,standing-by kwa lolote ambalo linaweza kutokea huko arumeru mashariki.na kuhitaji nguvu ya ziada.

Lakini pia yawe tayari kumlinda kamanda Lema dhidi ya washiri na Tendwa wao. Maana imedhihirika kuwa washili ni sehemu ya ukoo wa Siyoi Sumari.
 
safi sana'Wanalazimisha kuchukua jimbo ngoja waone jinsi wana arumeru walivyokomaa kisiasa
 
wewe wewe mtoa habari wewe mlalamikaji wewe shahidi wewe mchambuzi wewe hakimu yani kila kitu wewe khaa
 
hizo hela wanazotumia kwa magari, polisi, mamluki, *****, na kulipana per dm........wangelijua
wakazitumia kuboresha maisha ya mtanzania wala wasingefanya yote hayo na kujichosha
 
Hakuna ubaya wowote yapo kwa ajili ya usalama, mbona hayo magari yalikuwepo Arusha na Chadema wakashinda ubunge.
 
Back
Top Bottom