Hivi amani huombewa au hujengwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi amani huombewa au hujengwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 5, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wananajamvi nauliza:

  Hivi amani huombewa (au huombwa), kuihimiza au kuijenga? Nifafanue kidogo: Hapa nina maana kipi kinakuja cha msingi zaidi kuliko kingine: kuomba tu na kuhimiza kuwepo amani nchini au kuijenga amani hiyo katika misingi iliyo imara na ya haki? Kipi katika vitu viwili hivi kinaweza kuiokoa nchi katika farakano (na hata vita ya wenyewe kwa wenyewe) huko mbeleni?

  Ninaanzisha mada hii kwa sababu sasa hivi naona watu wengi katika jamii, wanasiasa na viongozi wa dini pia wanahimiza na kuwataka watu waombe kuwepo kwa amani -- badala ya kuhimiza viongozi wa nchi na serikali kujenga misingi imara na ya haki katika jamii na kuendesha nchi katika misingi hiyo.

  Nawasilisha.
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anayetoa amani ni Mungu.So you have to pray for it and than unachukua hatua kuipata.Its only when you have prayed for it ndio Mungu anapobariki every step you take kuipata.
   
 3. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  You are more ideological.... Timiza wajibu wako kwanza kwa kufanya (kujenga) Mungu anachofanya ni Baraka....kwa hivyo usipofanyakazi eti utegemee Mungu atanyesha Mvua ikupe chakula pasi na kulima ni uhuni.....Tayari tunajua Mwenyezi Mungu hutwazia mema viumbe wake...ila sisi ndo wahuni ...
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani hufanyiwa kazi na si kuombewa tu kwa mdogo. Baba angu siku zote alikua akiniambia kuwa "Hard work is prayer in action". Tatizo Tanzania tume kuwa watu tunao tumia dini vibaya na kudhani kupiga magoti tu kuta suluhisha matatizo yetu.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama hakuna haki nchini, uonevu uliokithiri, wizi wa rasilimali za umma na majibu ya kuudhi kutoka kwa viongozi hasa pale mtu anapoyahoji hayo amani kweli itakuwepo hata tukiomba kwa Mwenyezi mchana na usiku?
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kweli unayosema. Hawa viongozi wa CCM walio madarakani wakisaidiwa na baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wanatoa kauli majukwaani kuwahimiza wananchi waiombee nchi amani. Hii si mbaya -- lakini ni wanafiki tu kwani wanajuwa wazi kwamba amani haitapatikana kutokana na nchi kuendeshwa kihovyo hovyo, watu wananyimwa haki zao, wenye nacho sheria haziwagusi nk, nk.

  Mimi kwa upande wangu naona badala ya kupoteza muda kupiga kelele za kuwepo amani, basi watu hao wawe wanapiga kelele kukemea maovu hayo. Hii inaweza kusaidia.
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,009
  Trophy Points: 280
  Amani ni tunda la haki na uadilifu. Mungu yeye keshaweka sheria yake katika kila jambo, na ni njema kwa kila hali. Hivyo basi amani haiombwi bali inajengwa. Suala la maombi linakuja baada ya dhamira kuhukumika kwa kuiacha haki na hapa ndipo watu huomba wasamehewe ouvu wao na kurejeshewa amani walioipoteza ama inayotaka kutoweka, kwakutokuwa waadilifu katika misingi ya haki.
  Mungu hahitaji sana maombi yetu ya mda mrefu na msisitizo, zaidi ya anavyohitaji maisha yetu kuwa manyoofu katika kila nyanja tunayoikabili.
  .
   
 8. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Yote mawili yanahitajika. Amani ya kweli hutoka kwa Mungu hivyo ni wajibu wetu kumwomba atupatie hata hivyo hilo halichukui nafasi ya wajibu wetu. Ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha amani hiyo inakuwepo. Watu watimize wajibu wao kuchagua viongozi sahihi; watimize wajibu wao kushiriki mabadiliko ya katiba; nk
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Penye red: Unayosema ni sawa -- lakini wananchi hushindwa kufanya hayo -- kama vile kuchagua viongozi sahihi -- iwapo misingi ya sheria na haki haipo, au kama ipo basi huchakachuliwa na walio madarakani na hivyo kupata viongozi wabovu. Kwa hiyo tunarudi palepale -- sala hazitasaidia iwapo hali hii itaachwa kuendelea -- yaani kutokuwapo sheria, haki na utawala bora.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Maombi huwa hayasaidii kuyaondoa maovu katika jamii -- na pengine ni njia moja inayohimizwa na hao waovu walio madarakani na maswahiba wao wanaofaidi nchi katika kuwapumbaza wananchi -- yaani kusisitiza waombe amani huku wao wakiendelea kula jasho za wengine.

  Mimi naona hata kuiponda Chadema kwa eti inataka kuleta vurugu ni mbinu tu za hao -- Chadema wanachosisitiza si vita, ni kutaka iwepo misingi ya haki na sheria. Na hii ikipatikana basi itakuwa ni hofu kubwa kwa wezi na mafisadi.
   
 11. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Kuombea amani inafaa tu kama maombi yataelekezwa kwa Mungu kuwaondoa viongozi wasiotenda haki katika majukumu yao. Pia kukemea kwafaa zaidi kwani hujenga misingi ya amani.
   
 12. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mungu ametupa akili ya kujua mema na mabaya tutende yaliyo mema ndipo amani itapatikana.
   
 13. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Watu wanashindwa kufahamu kitu kimoja mhimu kuwa amani ni zao, ni tunda la haki. Hata kama mutakesha kwa maombi kama hakuna haki lazima amani itoweke.

  Amani siyo mvua, hata mvua nayo mkikata miti na kuifanya nchi jangwa hutoweka hivyo lazima tupande miti (haki) ili kuwezesha mazingira yaweza kuwa rafiki ya uundwaji wa mawingu yaletayo mvua (amani)
   
 14. e

  emalau JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Hiyo mada inaendana na fikra zangu, mimi mara kwa mara nawaambia kwamba mungu hapotezi muda kwa vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wa binadamu. Mungu amemuumba binadamu akampa na akili na utambuzi wa mambo kuliko viumbe vyote vingine, akaumba na mito na maziwa ili kwa kutumia akili zenu muweze kuvuta maji kuyapeleka katika sehemu za kilimo n.k. Pamoja na kukupa yote hayo leo hii unapiga magoti eti unataka atume mvua inyeshe kwenye shamba lako, kama ndo hivyo hakuna haja ya kukupa hiyo mito ni bora isingekuwepo ili aendelee kunyeshea shamba lako.

  Kama mada ilivyo sisi kama binadamu tuliopewa akili tunatakiwa kutambua kwamba haki isipotendeka hata tukeshe makanisani na misikitini amani haitashuka kutoka kwa bwana ila ni kwa kutumia akili alizotupa mungu kuweka misingi na ujenzi wa amani. Mungu mbela na agawe otaileo , huu ni msemo wa kabila fulani ukiwa na maana kwamba mungu anakusaidia lakini kwa kuangalia juhudi zako kwanza.
   
Loading...