Hitaji Kuu la Tanzania: Msukumo (Inspiration)! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hitaji Kuu la Tanzania: Msukumo (Inspiration)!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Nov 5, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Nov 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wapo wanaosema tunahitaji utawala bora. Wengine wanadai tunahitaji viongozi bora. Wote wanasahau hitaji kuu la Tanzania na Watanzania.

  Watanzania wanahitaji msukumo. Wanahitaji kutiwa moyo. Wanapaswa kuzinduliwa.

  Wananchi wamekataa tamaa. Wamekosa mwelekeo. Wanahitaji Dira.

  Wana wa Afrika wanataka Uongozi wenye msukumo. Wanahitaji dira ya kuwasukuma mbele. Wanalililia Azimio la Arusha.

  -----------------------------------
  "All this we can do. All this we will do" - The Inspirational Barack Hussein Obama
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hivi wasomi wanamchango gani katika hili la msukumo kwa watu ili wasiendelee kukata tamaa? Kibaya hata wasomi wamesalimu amri na kukata tamaa!
  Naona kama kila tatizo tunalichukulia kama linaletwa na wanasiasa kule sio kweli.Tuanze kuwa role models wa kujenga uchumi na kuinua kipato kwa kutumia usomi wetu ili watu wengine wapate moyo wa kuona inawezekana.
  Wanasiasa wanatuangusha na rushwa, Yes!Lakini tunajiangusha wenyewe kwa kuendelea kuwa wavivu, kukosa ubunifu na kudhani maendeleo yatakuja kutokana na miujiza ya wana siasa. Kwasababu hiyo rushwa ya wajanja wachache inakuwa kama ndio njia mbadala ya kuboresha maisha yetu bila kujari athari zake kwetu na kwa vizazi vyetu.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Nov 5, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Hata iweje hamtakuwa kama Marekani na Ulaya. Endeleeni kupiga longolongo tu
   
 4. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wasomi ndio wanao tuletea malalamiko mengi tunayo ya changia humu, baadhi hata kwa risk za maisha yao nadhani huo pia ni mchango. Na hii ni kwa sababu wanakerwa na mambo yanayo endelea nyumbani.

  Wasomi si watu wa kulaumiwa kabisa its clear where the finger should be pointed (Our constitution). Raisi ni product wa nguvu za ajabu alizopewa hili ni tatizo kubwa kwetu. Iwapo atutopata Raisi muwajibikaji basi ujue wahalifu wengi watapeta.

  Na hawa wahalifu sio hawa wakila siku tunao wajadili, no wapo wengi wenye athari kubwa mno kila kona ya nchi.

  Hawa ndio wanaoleta matatizo makubwa kwa namna ya uzembe wa kazi, ufinyo wa expertise kwenye secta wanazopewa kuongoza, daily corruption, wizi wa mali za umma, kupachikana kwenye kazi (Yaani uwezi kumuweka mwanao mhasibu wa kampuni kisa ana degree sijui ya sheria ata ua kazi na kuleta hasara, kuna watu wametumia miaka mitatu kujifunza hiyo kitu, huyu akupi kazi tu bali na idea za kuweza ku-expand).

  Yaani in short not much is being invested for hawa wasomi, na the government has no plans for them. Kwa sababu there's no point of educating more people if your not going to create opportunity for them or even opening the doors for them to create their own fate.

  Serikali aijiamini, Benki etu azina imani na wasio na asset, serikali ai-invest na wala aifikirii ni jinsi gani iwatumie wasomi wake. si ajabu ukakuta watu ambao wange benefit nchi in other sectors leo ni wabunge tu. Hii ni explanation kwamba serikali aina au labda aijui iwaumie vipi. Sasa hapo msomi atasaidia vipi?. Zaidi ya kujiunga tu na system au kulalama, come to think of it isnt that what we do here all the time.
   
 5. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  having no sense of direction na kutotambua how to deal and sort our problems realistically.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Chuo gani kinafundisha hayo unayoyasema? ..my take...anza kwako na watoto wako...make the proud of the country and its people..let them work for the nation and for themselves succesfully...tuanze kupima watu..je wao wenyewe kwenye maisha yao walikuwa succesfully?
  Unaweka waziri wa biashara hata hajawahi kuwa na kiosk aone hurdles zake atakuwa mbunifu.. i dare to say NO..bado sana
   
 7. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajua humu kuna watu wana accusations za ajabu, typos wata ambatanisha na vitu vingine sio kwamba awakueliwi bali ni finyu tu.
  Ukifanya kiswahili hawaoni bali kizungu, hicho ndio cha maana si ajabu kwao kujikana.

  I thought i should mention kwa sisi tusiokua na time ya kushinda humu ndani all day, kwani wao english is about big worlds too much time on the thesauras rather than being experts on the subjects, their justifications leave them naked of the're naivity.

  Thinking wanawatisha watu, labda .......

  PS. chale embu mtio adabu huyu mtoto
   
 8. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2009
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Contena you are right, big up man

  No plans at all, the elites becomes street mongers no matter what they have in their brains, their brains is full of new constructive ideas but where to put them into applications as a result instead of being constructive the opposite is true---nafikiri ndo maana ile patriotism watu wengi inawatoka and then they start running from their own country, because it is a bizzare to become a fugitive in your own country.
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  again kama una akili zako timamu why would you gamble with your future. I my self aim for certainity, sasa kwani mwingine ajaribu hatari alafu utalaumu wasomi how?

  Its the policies and the government strategies to blame 100%.
   
 10. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Katiba ni kitu cha kwanza ambacho kinapuuzwa hasa na viongozi, wanapovunja sheria kwa kuwa na uhakika kuwa hakuna kitakachotokea kwao. Hapa ndio pakuanzia kujua Tanzania tunahitaji nini.

  Swala hapa ni kuwaelewesha walio wengi haki zao kikatiba na kujua kuwa kwa kufuata katiba mabadiliko na maendeleo mangi yanaweza kutokea. Ukiangalia nchi nyingi zilizo endelea wananchi wana deal sana na katiba na wanajua wapi kuna haki zao au wapi wanaweza simama kidete kupinga kitu chochote kinachoenda nyuma ya katiba. Kwa kifupi ni kuwa Katiba inapaswa kutoa haki ya vitu basic ambavyo ni Life, Liberty and pursuit of happiness -kuishi na kujiendeleza kimaendeleo au kufanya kile kinachomuendeleza mtu binafsi au nchi na vile vile kuwalinda wananchi katika hali yoyote.
   
 11. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  hatuwezi kulaumu government 100% hata kidogo. lawama ni za pande zote watawala na watawaliwa. kama watawala hawafai kwanini tuendelee kuwapa madaraka for more than 50 years? si ni kwamba tumeridhika nao?

  kama haturidhiki nao kutoka moyoni basi tuwatoe.

  tatizo letu tunapiga kelele sana lakini tukipewa madaraka kidogo hata uenyekiti wa mtaa tunakaa kimya
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Nov 6, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zakumi,
  Mkuu samahani sana nilikuwa sikuiona hii hapo mwanzo kumbe imekugusa kiasi hiki..
  Well, nitakujibu kulingana na hoja zangu za awali..
  Kwanza tuanze na Marekani wenyewe maanake sipendi tufananishe nchi hizi mbili kwa sababu hatulingani kabisa.. Ni sawa na kulinganisha Bacelona na Yanga, kwa sababu tu wote ni mabingwa wa nchi basi unashangaa kwa nini moja ina matokeo tofauti na nyingine.

  Marekani hiyo spirit yao imetokana na kuwa na DIRA - Declaration of Independence. Huu ndio mchoro wa ramani wa nchi waliyokusudia kuijenga na ndio uliozaa Constitution yao na hata American dream ambazo ni nguzo muhimu ktk ujenzi wa Taifa lao..
  Kina Bill Gates, Napster na wengine wote ni matokeo ya watu walio pursue dream hizo na kwamba ipo sheria haki na wanajua safari yao inakwenda wapi..Kama dereva vile wa gari anavyoweza soma alama na kujua haki zake, sheria na safari yake kwa wakati mmoja..

  Sisi on the other hand tunataka kujenga Taifa pasipo ramani, yaani tunafyatua matofali na kuweka nguzo ovyo ovyo wananchi wakibebeshwa zege hawafahamu kinachojengwa zaidi ya kufikiria TZ itakuwa kama Amerika!.

  Nyerere alikuwa na fikra za jengo lake, Kaingia Mwinyi kabomoa nguzo kajenga zake, Mkapa naye kaingia na ufundi wake.. mwisho JK amejikuta ana nyumba nusu ambayo hajui ataanzia wapi.. Kusema kweli JK hajui aanzie wapi zaidi ya kuendelea kufyatua matofali kwa miaka yote minne kwani hana ramani ya nyumba..

  Tatizo langu kwenu na ubishi wote huu ni pale nyie mnapotoa suggestion kwamba tujenge tu, kila mtu ashike kifaa anachoweza kukitumia tujenge nchi badala ya kusubiri ama kuitegemea serikali itufanyie kila kitu..Kweli wapo watu wanaosubiri ama kutegemea serikali iwafanyie kila kitu lakini pia ni ujinga kufikiria kwamba tunaweza jenga nyumba (nchi) pasipo kuwa na ramani..

  Mfano mkubwa ni ujenzi wa nyumba nyingi nchini kujengwa ktk viwanja visivyopimwa..Matokeo yake ndiuo utata tulokuwa nao kila siku serikali inapotaka kujenga barabara au daraja inabidi watu wahamishwe na kulipwa fidia kwa sababu tu tumeanza na wananchi kufanya maamuzi yao kisha serikali inafuatia..matokeo yake barabara zinajenga si nzuri, pia bado hazitazami traffic for the next 20 yrs.. meaning miaka ijayo watabomoa tena nyumba nyinginezo kuongeza barabara..
  Yote haya yanatokana na kutokuwa na mwongozo - Dira..wananchi wote hatufahamu tunajenga kitu gani zaidi ya kila mmoja wetu kufikiria ujenzi wa kibanda chake.

  Mimi sii mpenzi wa Itikadi ambazo zinafuatwa kama msahafu..I believe in Idea kulingana na mazingira yetu yaani hakuna msahafu wa siasa ama itikadi unaoweza kulinbgana na maisha yetu.. Sii Ubepari au Ujamaa wa kuchongwa Ulaya..Lakini pamoja na yote haya huichukulia Siasa ama Uchumi kama imani ya dini. Sote tunataka kuokoka, tunataka mwisho wa maisha yetu kulazwe mahala pema peponi..Hata Pagan humwomba huyo Mungu Jua, Manson na Shetani wote wakiwa na imani kwamba maisha yao yote yanafuata barabara itakayowapeka ktk mafanikio..Na kwa kufuata Dira au (a Navigation system) inawasaidia kutopotea njia..
  Tatizo la Tanzania leo hii mbali na kutokuwa na Dira tunaenda kwa baraka zake Mungu. Hivyo hata tukikimbia haiwezi kusaidia kitu kwani tunakwenda tusikojua, pengine mbio zetu zitatufikisha haraka Jahanam!
   
 13. J

  Juja wa Majuja Member

  #13
  Nov 6, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hitaji la Tz sio msukumo maana hakuna msukumaji.
  Unahitajika moyo wa UZALENDO , yaani mapenzi ya dhati kabisa kwa TAIFA. Mtu wakati wote anachokiwaza kiwe ni kwa ajili ya TAIFA. HILO NDILO LILIKUWA LENGO LA AZIMIO LA ARUSHA. Tofauti na hapo ni UBINAFSI hatimaye RUSHWA na baadaye UFISADI
   
 14. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #14
  Nov 6, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tatizo lenyewe unalikwepa ni 100% the government.

  Reason, mimi na wewe ata tukienda kupiga kura bado kuna watu millioni 35 wengine wa kuwa convice jamaa hawafai (CCM). Nadhani unaona the amount of people who congregate whenever a CCM high official arrives, na raisi akienda ni mfarakano, hivyo the challenge is to win over this people and educate them CCM si chama.

  Until then we rely on the government to take us out of this mess. And their strategy doesnt seem to work, no one can challenge it, wasomi wameamua kukimbia fields zao na kwenda kwenye politics kitu ambacho awakielewi ila wanajua kuna wizi.

  It all comes to a simple explanation the government doesnt do enough to improve peoples' lives. Therefore it is 100% to blame.
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,450
  Likes Received: 5,841
  Trophy Points: 280
  Tuliambiwa ''Ardhi,Siasa safi na Uongozi bora'' na Mwalimu badala ya ''Ardhi,Nguvukazi,Mtaji na Ujasiriamali(Land,Labour,Capital and Entrepreneurialism)'' ambayo wachumi duniani kotwe wame advocate.Ndio imetufikisha hapa tumebaki na ardhi tu(amabayo Wakenya wanainyemelea hata humu JF) siasa safi na uongozi bora mumuulize JK vimeenda wapi.Mimi sivioni tena labda walivizika na Mwalimu kule butiama sijui MWITONGO.
   
Loading...