Historia ya neno Msela na Baharia

Salamu.

Kwa mujibu wa Kamusi la Kiswahili Fasaha, Toleo la Kwanza (2010) lililochapishwa na Baraza la Kiswahili la Zanzibar neno 'baharia' lina maana ya "mfanyakazi wa chombo cha majini; =mwanamaji".

Hayo ya kitaaluma si lengo la uzi huu, kwanza yanachosha na ni kuanza kueleweshana ni kutoana kwenye malengo ya jukwaa hili. Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni umaarufu wa karibuni uliolipata neno hili, likinasibishwa na uanaume flani wa kuwaweza wanawake na janja janja zao za kuwatoa upepo na kuwa washindi siku zote kwenye mahusiano, kuanzia 'kimamama' hadi uzeeni karibu na kufa huko.

Imekuwa fasheni kukuta majamaa wanaitana mabaharia kwa kujiamini na mbwembwe nyingi, ila inaleta ukakasi kidogo ukizingatia historia ya ubaharia hasa kwenye ukanda wetu huu wa Pwani ya Afrika Mashariki.
  • Mabaharia wengi walikuwa na stori za kuruka na warembo kila bandari ambako walitia nanga, ila hawakuwa wanatueleza ukweli wa kilichokuwa kinawapata pindi wanapogundulika kuwa wamezamia meli. Rejea stori za Meli ya Wagiriki, na ukizingatia ukweli kuwa 'mabaharia' wengi wa kwetu huku walianza kwa kuzamia.
  • Kukaa siku nyingi baharini mkiwa wanaume watupu si kazi rahisi, wenye roho nyepesi walikuwa wakitoana hamu. Hili halisemwi sana kwenye stori zao nyingi zile japo ndio ukweli mchungu. Simulizi maaraufu la 'Muwa Uliozamisha Meli' linashadadia hoja yangu hii, kwa mujibu wa mkuu Interest, muwa unaodaiwa kuwanogea 'mabaharia' hadi kufikia hatua ya chombo kuzama haukuwa muwa dhahiri, bali muwa dhahania. Sema ndio vile kulingana na maadili simulizi likawekwa kwa mafumbo.
  • Kava la Kitabu cha Sheria na Kanuni za 'Mabaharia' linalosambaa sana mtandaoni linajumuisha neno 'kuokoana' kama malengo mamojawapo ya 'undugu' huo. Sasa kumuokoa mwenzio si mpaka azame kwanza, sasa anazama wapi? Ndugu yangu mmoja ndiye aliyenistua kuhusu huu ukakasi wa 'mabaharia' na 'kuokoana', nashukuru sana kwa mchango wake.
  • Hii ndio funga kazi. Hapo zamani kidogo nilikuwa muumini wa dini moja hivi, miongoni mwa hizi zilizoletwa kwa mitutu, mashoka na mapanga. Kilichostua ukiacha janja janja nyingine za kawaida ni ukweli kuwa kwa mujibu wa maandiko, mtume mkuu wa dini ile (wengine hudai ni Mungu) hakuwahi kuoa, kuwa na demu wala mtoto, hata skendo ya ngono hakuwa nayo, tofauti kabisa na watangulizi wake ambao walioa, walizini na kufanya matendo mengine ya kibinadamu. Sasa cha mno kuwa miongoni mwa wafuasi wake kulikuwemo 'mabaharia', aliwaokotaga hukoo wakitoka kuvua samaki, na mmoja alikuwa kipenzi kweli kweli kiasi kwamba alimtunuku funguo za mbinguni na wapi kwingine sijui (rekodi imenitoka kidogo). Wakati wakiwa kwenye safari zao za kuhubiri 'kweli' ilikuwa inafika wakati mtume mkuu na mitume wengine kadhaa wanajitenga kidogo kwenda kuomba huko juu kilimani, wakiwaacha wengine wakilala fofofo.Kama kawaida, yule mtume 'baharia' alikuwa hakosi kwenye wateule wachache. Haya mambo yalinifikirisha sana, ukizingatia matukio mengi ya nyakati hizi yanayohusiana na taasisi za dini ile. Enewei...

Kisakale kimoja kuhusu habari za majini, au 'kimai' kama wataalamu wanavyouita utanzu huu wa fasihi kinasimulia kuwa; Hapo zamani za kale alitokea 'baharia' mmoja kwenye merikebu iliyokuwa ikielekea safari ya mbali. Baharia huyu alikuwa ndio anasafiri kwa mara ya kwanza safari ya umbali mrefu vile, ilikadiriwa kuwa wangedumu takribani majuma kumi na mawili wakiwa majini, bila kutia nanga bandari yoyote. Majuma manne ya kwanza hali ikawa ngumu kwa baharia, vyakula vikavu vya chumvi nyingi, hali ya hewa mbovu, maji ya kunywa yakitolewa kwa resheni na zaidi ile hali ya kujisikia vibaya kutokana na mchafuko wa bahari. Kilichomsumbua zaidi 'baharia' ni hamu ya tendo la ndoa, kwani siku ishirini na zaidi si mchezo kwa mwanaume yoyote rijali. Akaona amshirikishe baharia mwenzake kadhia hii... Baharia mwenzie, ambae alikuwa mzoefu kidogo kwenye merikebu ile akamwambia hilo ni jambo dogo sana, alitakiwa kwenda kwenye ghala la merikebu, huko angekuta pipa la machungwa lenye kitundu kidogo ubavuni, amalizie hapo haja zake. 'Baharia' akafuata maelekezo vizuri na haja zake zikatimia. Akarudi kwa mshauri na 'mwokozi' wake kumfikishia mrejesho na shukrani zake nyingi. 'Baharia' mkongwe akamuambia asiwe na wasiwasi, kwani anaruhusiwa kwenda pipani kumaliza haja zake muda wowote, siku yoyote isipokuwa siku ya Jumanne, kwa siku nzima.
'Baharia' mgeni akahamaki na kuuliza kunani siku ya Jumanne hadi iwe marufuku kwenda pipani? 'Baharia' mkongwe akamjibu kwa upole "Itakuwa zamu yako kuwa ndani ya pipa..."

Kwa hiyo ndugu zangu 'mabaharia' wa JF na kwingineko, sina ubaya na nyie kujipa hiki cheo na kutembea vifua mbele, hilo ni lenu na vizazi vyenu. Rai yangu ni kuwa muwe makini na hii misimu na fasheni mpya ambazo ujio wake ama una ukakasi, ama una ajenda ya kiroho kubwa zaidi ya 'ubaharia' wenu wa kubumba. Kama tu ambavyo majamaa walifurahia na kuona ni usasa kuvaa 'mlege' hadi walipogundua kuwa ile ilikuwa ni 'code' ya mambo fulani ya 'kibaharia' iliyoasisiwa kwenye jela za Amerika huko, zamani hizo.

Uzi tayari!
 
"Kuokoana"
Unamaanisha mabaharia wanadukuana?
Siku zote husema mimi sio baharia wa kuzamia kila bahari
 
Kila zama na kitabu chake. Mabaharia wa kizazi hiki kwenye fuso tu tupo na milupo kama yote, sembuse kwenye meli
 
Ina maana wale Me ambao huwa naona humu munajiita mabaharia huwa hamjui maana.
Siyo wote mimi hata sijui maana yake na sijawahi kujiita hivo
Leo kuna sehemu nilikutana na kijana anamuuliza mtu fulani kama namfahamu akawa ananiita baharia ananikimbilia nikamwambia umekosea mimi siyo akasema wewe mwenyewe ni baharia nauliza kwa mzee fulani?
Nikamwelekeza
 
Back
Top Bottom