Historia ya neno Msela na Baharia

Kikawaida mimi huwa sibebwi na mawimbi ya vimisemo vya ajabu ajabu vya msimu...huwezi nikuta natumia hii misemo kwenye mdomo wangu..
Sijui....KAMA LOTE....WATAPATA TABU SANA...etc
Na sasa naona kila mahalî BAHARIA...
Mkuu hii misemo tu huja na kuondoka kama kelele za mlango. Isikupe taabu, wenyewe wanajipa raha kwa haya.
 
Siyo wote mimi hata sijui maana yake na sijawahi kujiita hivo
Leo kuna sehemu nilikutana na kijana anamuuliza mtu fulani kama namfahamu akawa ananiita baharia ananikimbilia nikamwambia umekosea mimi siyo akasema wewe mwenyewe ni baharia nauliza kwa mzee fulani?
Nikamwelekeza
Basi uwe unatembelea MMU na Chitchat kule huwa naona Me kibao wanajiita Mabaharia.
 
 
Huyu ni baharia mkongwe.
Injinia wa meli Le Mutuz.
MNAMPA KIKI za bure tu unafikiri mtu akifikia level za kuwa engineer kwenye meli anaweza kubali kuja kuvaa mapensi bongo....lemutuz alikua oiler tu ila anajigamba alikua engineer ni uongo mtupu anawajaza watz.......over
 
Msela = Sailor

Hilo lilitokana na meli na majahazi ya zamani ya mizigo na abiria kutumia matanga "sailing". Mfanyakazi wa hizo meli na jahazi za matanga ndio "sailor" kwa Kiswahili wakamuita "msela",

Baharia = Seaman

Meli na majahazi ziliposita kutumia matanga na kutumia nishati zingine mbadala ndiyo ikawa hao wafanyakazi humo huitwa mabaharia au Seaman kwa kuwa hawa "sail" tena.
ninkwendera ekyo!
 
Back
Top Bottom