Historia ya neno Msela na Baharia

Historia ya neno Msela na Baharia

Baharia ni marufuku kutumia chumvi laini tunatumia ya Mabonge tu tena muda mwingine inakuwa mboga
 
#Baharia, pia "mwanamaji" ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha usafiri majini, hasa baharini kama vile boti, mashua, jahazi au meli. "Mwanamaji" hutumiwa mara nyingi kwa kutaja mabaharia wa kijeshi.

Kuna kazi nyingi tofauti zinazotekelezwa na mabaharia.
Mkuu wao ni nahodha au kapteni wa chombo.

Katika mashua au jahazi ndogo mabaharia wote wanafanya kazi pamoja ambapo kazi zinazoonekana ngumu zaidi hupewa kwa wale walio vijana.
Kadri meli inavyokuwa kubwa zaidi, shughuli mbalimbali za melini zinagawiwa kwa mabaharia wenye ufundi fulani.

Meli kubwa zinaweza kuwa na idara tofauti zinazohitaji mabaharia wenye fani mbalimbali.

---------
sasa wavuta bhangi wa bongo hivi karibuni wameamua kuichafua tasnia ya "ubaharia" kwa kuihusianisha na wazinzi wa kiume,

wenye nia ya kuwachezea na kuwaharibu wanawake kihisia pasi na kujali lolote kuhusu wanawake hao.


tanbihi:

#ubaharia ni tasnia halali kama zilivyo zingine,

na sio uhuni kama ambavyo hupotoshwa na vijana siku hizi.


tamati:

hata hivyo,

lugha ina tabia ya kuwa na misimu inayoshika hatamu katika kipindi fulani,

hivyo "baharia" laweza kutumika kama msimu katika muktadha fulani.
 
huu ni msimu tu na wote tunaelewa hivyo maana ndio kiswahili kilivyo. Mabaharia hands up!!
 
Baharia hatakiwi kufanya mambo yafuatayo kutokanaa na katiba ya mabaharia ibara ya Kwanzaa sura ya Kwanzaa imeeleza baharia haruusiwi

.kuoga oga kila Mara hizo ni tabia za kike unaoga sana ili iweje uwe na ngozi ya nyororo kama demu? Baharia anaoga Mara moja kwa siku au haogi kabisa

Kula chips au ice cream pamoja na ukwaju kufanya hivyo kunatupa wasiwasi na jinsia yako

Kukaa au kuwa na demu mmoja tu hii inaashiria wazi kuwa utakuwa na upungufu wa nguvu za kiume baaharia lazima uwe na mademu wengi ukishindwa gonga sepa ukae nae sana kwani ndugu yako huyo

Baharia alii wala halalamiki hovyo hata ukimuumiza au kumchana na kitu kikali au uungue hata na moto ni kosa baharia kulia na nyongeza baharia lazima uwe na kovuu mwilini

Baharia wote wamoja haiwezekani atokee jinsia nyingine au mshangazi amletee za kuleta mwana au hata muhuni yeyote lazma tuungane kukuharibu

Baharia inabidi ufanye juu chini ulale hata lock Up au huishi hata miezi jela hili ni la muhimu Sana ukishindwa hakikisha umepigwa hata na police au umefanya vurugu

Baharia huruhusiwi kusafisha getho labda zarura pale patokeapo mechi pia ni marufuku kufua fua boksa kila saa umekua demu kwani soksi sharti zivaliwe wiki zinuke ni muhimu baharia kunuka mguu

Imetolewa na mwenyekiti anaemalizia mda wake chama cha mabaharia

Wizara ya wahuni na ustawi wa wasela na wana na mabaharia

Mwenyekiti kanda maalumu
S. L. P 3000

CC.@mlevimmoja
 
usikariri mkuu neno moja linaweza kuwa na maana nyingi sana

Sisi tutabaki kuwa MABAHARIA na wewe endelea na ubaharia wa melini

ila karibu kwenye jumuiya yetu mkuu
tapatalk_1566936620377.jpeg
 
#Baharia, pia "mwanamaji" ni mtu anayefanya kazi kwenye chombo cha usafiri majini, hasa baharini kama vile boti, mashua, jahazi au meli. "Mwanamaji" hutumiwa mara nyingi kwa kutaja mabaharia wa kijeshi.

Kuna kazi nyingi tofauti zinazotekelezwa na mabaharia.
Mkuu wao ni nahodha au kapteni wa chombo.

Katika mashua au jahazi ndogo mabaharia wote wanafanya kazi pamoja ambapo kazi zinazoonekana ngumu zaidi hupewa kwa wale walio vijana.
Kadri meli inavyokuwa kubwa zaidi, shughuli mbalimbali za melini zinagawiwa kwa mabaharia wenye ufundi fulani.

Meli kubwa zinaweza kuwa na idara tofauti zinazohitaji mabaharia wenye fani mbalimbali.

---------
SASA WAVUTA BHANGI WA BONGO HIVI KARIBUNI WAMEAMUA KUICHAFUA TASNIA YA "UBAHARIA" KWA KUIHUSIANISHA NA WAZINZI WA KIUME,
WENYE NIA YA KUWACHEZEA NA KUWAHARIBU WANAWAKE KIHISIA PASI NA KUJALI LOLOTE KUHUSU WANAWAKE HAO.

TANBIHI:
#UBAHARIA NI TASNIA HALALI KAMA ZILIVYO ZINGINE,
NA SIO UHUNI KAMA AMBAVYO HUPOTOSHWA NA VIJANA SIKU HIZI.

Tamati:
HATA HIVYO,
LUGHA INA TABIA YA KUWA NA MISIMU INAYOSHIKA HATAMU KATIKA KIPINDI FULANI,
HIVYO "BAHARIA" LAWEZA KUTUMIKA KAMA MSIMU KATIKA MUKTADHA FULANI.

[emoji1378][emoji469][emoji469][emoji469][emoji469][emoji469]
Yaaniii! Kwa lugha mpaka sauti mnafanana na shibuda!
 
Back
Top Bottom