Wana jamvi naamini mu wazima wa afya
Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.
Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.
Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten
hivi mtu akiuudhi kununa ndo suluhisho? Mume hanuniwi ulikosea tangu mwanzo kama kakosa kaa nae chini mwambie 1,2,,3 sijapenda baada ya hapo kama anajirekebisha maisha yanasonga kama kawa na mwanaume asiechepuka hapa duniani ni moja ya kumi baada ya kugundua anachepuka usingenuna ungesuluhisha sidhani kama mngefika mahakamani
Jitahidi sana muyamalize kukuza watoto pekee yako si lelemama waweza chizika. Elimu, chakula,afya, malazi na mengineyo kwako utamudu?
Kama kaenda akikupa mimba nyingine useme pia usitufiche.
kwa maeelezo yako nimengudua wewe umbo lako ni mboge.!!
Ila una moyo dada yangu, yani kakuchiti msahama kashindwa kuomba, kanuna, mwisho wa yote kaamua kukutelekeza wewe na watoto na o bado unamuita mumeo? unasubiri nini kuivunja hiyo ndoa? au unataka yakimshinda huko arudi kuja kumalizia shida zake kwako?
Haya mambo ya kusema mtu kaondoka atarudi...atakuja ku propose upya kama ntakuwa available...ni talaka tu...
Wanarudigi wakisha ukwaa...nani akuudumie ukiwa mgonjwa na starehe umekula mwenyewe...
Mwanamke Mpumbavu huvunja nyumba yake mwenyewe kwa mikono yake,,huu usemi waliousema hawajakosea umeona ufahari kumfanyia visanga mmeo angalia unavyoivunja nyumba yako kwa maelezo yako kuna shoga yako unamuelezaga matatizo yako ya ndan anakushauri ujinga km huo ndoa ni kuvumiliana na kusamehane angalia sasa mpk hela ya kula unaenda kuidai mahakaman
Wana jamvi naamini mu wazima wa afya
Nimeolewa miaka nane iliyopita na tumebahatika kupata watoto watatu,tangu nimeolewa hiyo miaka naweza sema nimeishi na mume wangu miaka mitatu,namaanisha ki-ndoa.Maisha ya ndoa yetu naweza sema ni ya ajabu sana kwa jinsi nionavyo mimi.Mume wangu akinikosea huwa ninatabia ya kununa ili aniombe msamaha,na kwasababu mwanaume kuomba msamaha ni ngumu huwa nahitaji basi hata kutambua tu kosa lake.Lakini kwa mwenzangu imekua ni vigumu,nikinuna nae huwa ananuna.
Miaka mitano iliyobaki tumeishi maisha ya kununiana mpaka hivi leo hatuongei.Mnuno wa mwisho sababu yake nilimgundua anatembea na binti mmoja na kwa ushahidi,lakini hakujutia wala kuomba msamaha,badala yake nilinuna nae akanuna yapata mwaka mmoja sasa,tumelala kitanda kimoja hanigusi wala simgusi, mpaka sasa kakimbia nyumba,kaniacha mimi na watoto ikafikia hatua akakataa kutoa pesa ya chakula ikabidi nikamshitaki kwa wazee,ila ilishindikana,wazee wakaniambia nimpeleke mahakamani,hivi sasa anatoa ela ya chakula kwa amri ya mahakama ingawa hapendi.
Wanaume mkigombana na wake zenu muwahudumie watoto wenu maana ni wenu,baada ya kusema maneno haya kifua changu kimepumua na ninaamini kuanzia leo nitakula chakula vizuri na kuanza maisha mapya.Usitukane wala usidharau maana ni dukuduku langu la muda sasa nitarudi kutumia id yangu ya siku zote .Asanten
Ni kweli wakati mwingine inatubidi tuwe na moyo,namuita mume sababu hatujapeana talaka, ila hata yakimshinda hawezi maliza shida zake tena kwangu
Mkuu labda huko kwenu... Huku kuna mwanaume alifunga ndoa na mwanamke ana watoto 6, tena wawili tu ndio wa baba mmoja na waliobaki kila.mtu na baba yake. Walipendezaje??
wanaume wengine hawajui kubembeleza
pole dada angu ila elewa hawa wanaume sio binadamu ni watu