Historia ya nchi yetu iliyofichwa



Nikishajua itaniwezesha kupata mwanzo wa kutambua chanzo cha MFUMO KRISTO SERIKALINI(CHRISTIAN LEGACY)

Mwinyi kakaa miaka kumi plus kikwete miaka mitano hawafuti the so called Christian Legacy.
 
Islam has been in existence in East Africa since the eighth century. With Islam, emerged the lingua franca, Kiswahili, spoken throughout East and Central Africa and the Swahili culture which is mostly associated with Muslims. About two-thirds of East Africa’s Muslims reside in Tanzania which is the most populous of the East African countries i.e. Kenya, Uganda and Tanzania. According to the 1957 population census, Muslims outnumbered Christians at a ratio of three to two. This means Tanzania is a leading Muslim nation in the region. But the 1967 census the total figures for Tanzania Mainland are 32% Christian, 30% Muslim and 37% local belief. This shows Pagans as a leading majority. The 1967 census has not been able to show the reasons for the sudden decrease of Muslim population nor the growth of Paganism. This was the last population census showing religious distribution. It is widely believed that the figures for the 1967 census were doctored for political reasons to show Muslims were trailing behind Christians in numerical strength. This paper "lnsha Allah", will try to show the reasons behind such a move and many others.

Read more: ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA

sensa ya pwani
 
Hakika historia ya Tanzania imefichwa na inahitaji magwiji wa historia kukaa, kufanya utafiti na kuiandika upya. Mfano, tunapoambiwa kuwa Tanzania ilipata uhuru 9-12-1961 HII SI KWELI. Ni upotoshaji wa makusudi kabisa wa historia. Siku hiyo ilikuwa ni uhuru wa Tanganyika.

Pia historia ya uhuru wa Tanganyika inasisitizwa zaidi kuanzia mwaka 1954(ilipozaliwa TANU), nao ni upotoshaji wa makusudi. Nikiwa mzalendo na msomi wa kiwango cha kawaida kabisa, ningependa kujulishwa kwa nini historia haielezi nafasi ya dini zetu(UISLAM na UKRISTO) katika kupigania uhuru wa nchi yetu!!! Mfano, mchango wa UISLAMU na WAISLAMU ktk kupigania uhuru wa Tanzania ni zaidi ya 75%. Vita vya MAJIMAJI viliongozwa na WAISLAMU ambao ni Chifu SONGEA BIN RAUF na KINJEKITILE NGWARE. Pia wapo akina BWANA KHERI, ABUSHIRI BIN SALIM EL-HARITH kwa upande wa kaskazini. Katika mkoa wa Iringa yupo Chifu MKWAWA ambaye nae ni muislamu(mjukuu wake Adamu Sapi Mkwawa ni muislamu). MIRAMBO na ISIKE.

Katika zama za kati miaka ya 1940-1950s wapo akina MZEE BIN SUDI, ABDULWAHID SYKES, DOZA AZIZ, TEWA SAIDI TEWA, SULEIMAN TAKADIRI, AHMED RASHAD, MSHUME KIYATE, HAMIS DIWANI, SAADAN ABDU KANDORO, ALI MANENO, ZUBERI MTEMVU,IDDI FAIZ, RAJAB DIWANI, BIBI TITI MOHAMED, RAMADHAN CHAUREMBO, HAIDAR MWINYIMVUA etc



  • Mbona wamesahaulika? Wamesahaulika kwa makusudi au ni bahati mbaya?
  • Mchango wa makanisa ktk uhuru wa nchi yetu ni upi?
  • Mbona jamii ya kiislamu nchini ipo nyuma, nini kimesababisha hali hii?

Ni wakati muafaka kupeleka hoja binafsi CUF ili kuweza kudai Historia Mpya
 
Msihangaika na historia ya nchi. Historia ya nchi inaeleweka. Kisichoeleweka ni jinsi ya kujikomboa kutoka kwa ufisadi wa RA, JK na EL. Ukijua jinsi ya kuondokana na ufisadi huo utakuwa unaishi katika zama za utajirisho.
 
na kuna trial ya waliomuua karume mnaifahamu? na kuna mambo mengi sana yamefichwa nafikiri kina maggid wangetusaidia tu.
 
Kaumza, you are too biased there were prominent people such as Kirilo Japheth etc.
 
Tanganyika bahati mbaya aina ma Heroes zaidi ya Nyerere kila kìtu kafanya peke yake.,south africa siku ya uhuru wao uwa lazima wawataje ma Heroues wao..
1.Nelson Mandela
2.Walter max uliyate
3.Oliver Tambo
4.Joe slovo
wapo wengi kìna Albert Luthuli mshindi wa Nobel kina Steve biko..uku kwetu kuna baba wa la la Tanganyika mmoja Tu inatosha..
 
ningependa kujulishwa kwa nini historia haielezi nafasi ya dini zetu(UISLAM na UKRISTO) katika kupigania uhuru wa nchi yetu!!!


Ninajaribu kujibu hayo maandishi mekundu:


Historia ya uhuru wa nchi, ni historia ya nchi au Taifa na watu wake wote. Na si suala la makundi fulani ya kikabila au kidini.

Kwa kuongelea uhuru wa nchi yetu, nafikiri kwa watanzania wazalendo inatosha kuwaongelea watu waliohusika bila kujali dini zao au makabila yao. Ni imani yetu sisi wazalendo kuwa wananchi waliopigania uhuru HAWAKUPIGANIA UHURU WA WAKRISTO AU WA WAISLAM, AU WAPAGANI. WALIPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA. HII NI PAMOJA NA ASKARI WALIOPIGANA VITA YA 1978 DHIDI YA UGANDA, HAWAKUPIGANIA WAISLAM AU WAKRISTO. WALIPIGANIA NCHI. Hatuwezi tukaanza kunyumbulisha majina ya askari wa kiislam au kikristo walivyoshiriki eti kwa minajiri ya kuonyesha mchango wa dini fulani. Badala yake tunaonyesha kuwa Ni askari wa Tanzania ndio walioshiriki.

Kwa maana hiyo basi si lazima kila kitabu cha historia kiandike kuwa mpigania uhuru A na mpiganaji wa TPDF B aliyepigana uganda, alikuwa ni wa dini fulani. Kwenye historia inayojali utaifa, mambo kama hayo yanakuwa hayana tija.

Hata hivyo kwa uhuru walionao watu, hawakatazwi kwenye sehemu husika (kwenye mikutano yao ya dini) wakitaka kuwataja watu wote waliotoka kwenye dini zao.

Bottom line: Regardless ya dini na makabila ya waliopigania uhuru, wapiganaji hao walikuwa wanapigania uhuru kama WATANGANYIKA.

Excellent answer!
 
Poor Education!!!, :A S 109:
''GIGO''.
Computer rule, stating that the quality of the output is a function of the quality of the input; put garbage in and you get garbage out
 
Back
Top Bottom