Historia ya Mwanamziki Jolie Detta kutoka Congo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia ya Mwanamziki Jolie Detta kutoka Congo

Discussion in 'Entertainment' started by igwana123, Oct 16, 2012.

 1. igwana123

  igwana123 Senior Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wanajamvi na wanahistoria naomba historia ya huyu mwana Mama Diva Jolie Detta aliyefanya kolabo ya wimbo Masuu na Lwambo. Mwanamziki huyu alikuwa na kipaji cha pekee na anastahili kuenziwa kazin yake.Ahsante sana
   
 2. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Jolie Detta alijiunga na TP OK Jazz mwaka 1986 na mwaka huohuo alishiriki kurekodi kibao "Massu" kilichompatia umaarufu mkubwa sana ndani na nje ya Congo. Jolie Detta ni mwanamke pekee kupewa nafasi kuongoza uimbaji (lead) katika TP OK Jazz. Hii inaonyesha ni jinsi gani gwiji Luambo Luanzio Makiadi alikithamini na kukikubali kipaji chake. Kuna wakati bendi ilikuwa na waimbaji wengine wa kike Nyota Yondo, Nana Akumu na Baniel Mbambo, lakini hawa walikuwa ni waitikiaji tu. Jolie Detta hakudumu sana TP OK Jazz na mwaka 1987 alijiunga na bendi ya Anti Choc ya Bozi Boziana. Hapa Jolie Detta anaimba live kibao "Massu" mwaka 1986 akishirikiana na Nyota Yondo, ambaye ni pacha wa Kusala Yondo, anayejulikana zaidi kama Yondo Sister.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2013
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Mimi penda sana hii wimbo, mwanzo nilidhani umeimbwa na Vicky Longomba...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. M

  Masuke JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2013
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Huo wimbo nikiusikiliza huwa naona kama ananiimba mimi ila hataki tu kumalizia jina langu, hivi kwenye ule wimbo wa Layile ile sauti ya kike ni ya nani?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2013
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Kwa kuongezea. Joli alitokea bendi ya Afro International chini ya Mimi Ley aliyekuwa bendi ya Afrisa International ya Tabu ley. hakudumu sana pale Afro International kwani Ben Nyamabo alimchukua kwenda Choc Stars bendi iliyokuwa na Bozi Boziana, Defao. Then mwaka 1986 mwishoni Joli akatoka OK Jazz akaenda kujiunga na bendi mpya ya Bozi mpaka mwishoni wa miaka ya 80. Kwa sasa yupo anaishi Angola baada ya kifo cha mumewe Ndeko aliyefariki kwa ukimwi. Joli kaokoka na anaimba nyimbo za dini kwa hivi sasa. Alitamba sana alipokuwa Anti Choc na nyimbo zake tamu kama Darse Likotino na nyinginezo.
   
 6. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35

  Hapa Jolie Detta anashirikiana na mwanamama mwingine Deesse Mukangi na Bozi Boziana katika kibao Zongela Ngai wakiwa na bendi ya Anti Choc. Jolie ni huyo anayeimba peke yake mwanzoni na katika chorus. Hii ilikuwa ni mwaka 1989. Nadiriki kusema sijawahi kusikia combination kali ya sauti za kike katika muziki wa Kiafrika kama Jolie Detta na Deese Mukangi.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hiyo sauti ya kike ni ya huyu tunayemjadili hapa – JOLIE DETTA
   
 8. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2013
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280

  Nakuunga mkono mkuu, ni kweli kwani kombo yao ilitisha sana licha ya kina Scola kuja pale Anti Choc ila origino ni origino tu. Binafsi namfagilia sana Mukangi si tu kuwa ni mswahili (mtoto wa Kisangani kwa Tantine Abeti Masikini) bali ana sauti tamu ile mbaya, nani anabisha?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Kweli Mukulu. Deesse ana sauti nzuri sana. Inanikumbusha marehemu Mpongo Love. Sauti zao zinafanana.
   
 10. Nyanidume

  Nyanidume JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2013
  Joined: Oct 24, 2012
  Messages: 2,156
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2013
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280

  Yes, lakini Mpongo katika wimbo na wimbo ila Mukangi bwana ile ni mashine kwani alichukuliwa na wanamuziki wengi sana kufanya kolabo kutokana na sauti yake kuwa tamu. Kwa wanaume namfagilia mswahili mwingine wa zimpopa pompa Bw. Luciyana Litemo Demingongo....hatariiiiiii. Alipotoka Viva La Musica Papa Wemba alilia.
   
 12. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Namkubali sana Luciana. Ukitaka kujua kipaji cha huyu jamaa sikiliza wimbo Princess Julia ambao ni utunzi wake akiwa na Nouvelle Generation. Mwimbaji mwingine wa kiume kutoka Congo ninayemvulia kofia ni Nyboma Mwandido. Hapa anaimba kibao Amba akiwa na Lipua Lipua mwaka 1974, wakati huo akiwa kijana mdogo wa miaka 21 tu.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2013
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280

  Mkuu kama unakuja katika zama hizi, nafikiri utakubaliana nami kuwa Nyboma alikuwa hafui dafu mbele ya Kilola Toko Diangani wa Lipua Lipua pia. Kilola ni yule aliyetunga wimbo wa 'Okomi Boye' na ni yeye ndiye aliyekuwa anaimba solo. Nyboma alikuwa anaimba sana ila bwana kuna watu walikuwa juu sana kipindi kile kama utakuja kwa Kiam kuna jamaa alikuwa anaitwa Bamueniko Adoli pamoja na Solola Sol (waimbaji sauti ya kwanza). Kama uliwahi kusikiliza wimbo wa Kiam 'Bomoto,' na ile sauti tamu ni ya Adoli nyembamba zaidi ni ya Solola Sol Sol.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. papag

  papag JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2013
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Sina la kusema. Mmenikuna vya kutosha.
   
 15. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu nakubali kuwa enzi hizo kulikuwa na waimbaji hatari sana huko Congo. Mwanzoni katika mjadala huu tulimzungumzia mwanamama Jolie Detta alipokuwa na TP OK Jazz, lakini inabidi pia tuwatendee haki waimbaji mahiri wa kiume waliopitia bendi hiyo iliyokuwa chini ya Luambo Luanzo Makiadi. Waimbaji wengi wazuri walipitia TP OK Jazz katika uhai wake kuanzia mwaka 1956 hadi 1993, lakini wanaochomoza zaidi ni Sam Mangwana, Youlou Mabiala, Ntesa Dalienst, Kiambukuta Josky, Djo Mpoyi, Madilu System, Carlyto Lassa na Malage de Lugendo. Huyu hapa Ntesa Dalienst na kibao Bina Na Ngai Na Respect (cheza na mimi kwa heshima) akiwa na TP OK Jazz mwaka 1981.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hapa Djo Mpoyi anaimba kibao Masikini akiwa na TP OK Jazz katika 'live show' katika studio za televisheni ya Zaire mwaka 1986. Hili ni onyesho lile lile alimoimba Jolie Detta katika video iliyotangulia.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2013
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280

  Mkuu Carlyto Lassa hakuwa O.K. Jazz, yaani huyu bwana (mlokole kwa sasa) alikuwa anaimba Zing Zong za kina Simaro Massiya na Mayaula Mayoni. Kabla hajaingia kabisa O.K. Jazz Ben Nyamabo (kiongozi wa Choc Stars) akamchomoa T.P. O.K. Jazz kwenda Choc Stars bendi aliyokuwa anaimbia Defao Matumona kabla hajaanza kuwika na Big Stars. Binafsi katika O.K. Jazz niliwapenda sana Wuta Mayi, Ntesa Nzitani Dalienst, Kiesse Diambu (mdogo wake Ntesa pia alikuwa Lipua Lipua), Pepe Ndombe, Djo Mpoyi, na Ninja Madilu. Sam mangwana sina mushikheri naye, sijuwi kwa nini. Kwa sasa wanamuziki wapo ila hawana sauti tamu kama za awamu ile, uwongo? Sawa, wako wachache kama kina Demingongo, M'piana hana sauti nzuri, anaimba tu ila sauti yake siyo issue kwani hata mimi naimba shinda yeye ila sijiusishi tu na muziki napenda kuimba nikiwa chooni ama chumbani kwangu kwa raha zangu mwenyewe.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Bingwaman

  Bingwaman JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2013
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu shukran kwa kunikumbusha Kiesse Diambu, Wuta Mayi na Ndombe Opetum, ambaye alifariki miezi michache iliyopita. Katika pekuapekua yangu YouTube nimenasa video hii adimu ya Choc Stars iliyorekodiwa 1984. Hapa tunawaona waimbaji (kutoka kushoto) Debaba, Nzaya Nzayadio na Carlyto Lassa. Itakumbukwa kuwa Nzaya Nzayadio alitamba sana miaka ya 1970 akiwa na Lipua Lipua. Katika solo yupo Roxy Tshimpaka 'Le Grand Niaou', ambaye alijiunga na Choc Stars akitokea Zaiko Langa Langa.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2013
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280

  Ben Nyamabo ni shabiki wa Zaiko na aliiunda Choc Stars ili kuleta upinzani kwa Zaiko kwani alichukua vijana wa kali wa wakati huo kama kina Djuna Djanana, Bozi Boziana, Paul Nzayadio (Nzaya), Carlyto, Roxy, Petit Prince, Defao, Sedjo, na wengine. Hawa jamaa walitisha sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...