Historia ya mtende, umaarufu wa matawi 🌴🌴

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,663
4,875
Mitende ni miti mikubwa ya jenasi Phoenix katika familia Arecaceae. Matunda huitwa matende.
Mitende ni maarufu katika utamaduni wa Waisraeli na Waarabu. Yoh. 12:12-19 inataja matawi ya miti hiyo kwamba yalitumika kumshangilia Yesu alipoingia Yerusalemu kwa mara ya mwisho. Ndiyo sababu hadi leo matawi hayo yanatafutwa sana na Wakristo kwa maandamano ya Jumapili ya matawi, wiki moja kabla ya Pasaka

Sifa za mtende

Tabia ya mitende ya Palestina. Inafafanuliwa kuwa inasitawi” ( Zaburi 92:12 ), cant. 7:7 ndefu “iliyonyooka” ( Yeremia 10:5 ) . Matawi yake ni ishara ya ushindi (Ufu. 7:9 Ilichorwa kwenye nguvu ili kupamba. Eze. 40:13-16, 20, 22.
Na kwenye kuta pia. Fal.6:29, 32, 35.

Mtende ni mti unaobeba alama ya mafanikio na ushindi. Kwa miaka mingi matawi yake yametumika kuonyesha alama ya ushindi furaha na Amani.Mara nyingi katika Neno la Mungu kila mahali matawi ya mitende yalipo tumika yalihusianishwa na ushindi.

Mfano Kwenye hekalu la Sulemani Tunaona mitende ilikuwa ni moja ya michoro iliyokuwepo kwenye hekalu la Sulemani ikiashiria ushindi. Matawi ya Mitende tunaona yakitumika kumshangilia na kumwimbia Yesu alipokuwa anaingia Yerusalemu.

YOHANA 12:12-13

Siku iliyofuata umati mkubwa uolikuwa umekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Yesu angekuja Yerusalemu. Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana! Amebarikiwa Yeye ajaye kwa Jina la Bwana! Amebarikiwa Mfalme wa Israeli!’’

UFUNUO 7:9-10 tunaiyona mitende ikitajwa na ikieleza vil Watakatifu walio vaa mavazi meupe wakiimba kwa ushindi mkuu wakiwa wameshika matawi ya mitende mikononi mwao wakiashiria Ushindi.

“Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao;”

Una manufaa sana Kikristo

Mti huu katika Maandiko Matakatifu umetajwa kama moja ya miti Maarufu sana ambao hutumika kuelezea Ushindi, amani na Ustawi. Katika Israel mti huu huhesimika sana na unatumika kama moja ya nembo ya Taifa ukihusihwa na Taa ya vinara Saba. Maandiko Matakatifu yanautaja mti huu kwa sababu ya mafundisho kadhaa

1. Ushindi na amani na Ustawi Kutoka 15:27 watu wa Mungu waliburudika baada ya Ushindi
2. Ni Malimbuko ya Canaan Mji wa kwanza kupewa na Mungu kwa Israel Yeriko ulikuwa na mitende mingi sana na uliitwa mji wa mitende Kumb. 34:1-3, Waamuzi 1:16
3. Mtende unazungumzia Faraja na furaha na kurejeshwa 2Nya. 28:15
4. Katika Biblia kama mtende umekauka ilihesabika kuwa Furaha imeondokwa kwa wanadamu Yoeli 1:10-14 na ilihitajika maombi na toba kurejesha furaha hiyo
5. Mitende ilitumika kama mapambo na sifa ya uzuri 1Falme 6:28,32, wimbo bora 7:7
6. Ni alma ya Ushindi wa sasa na ujao Yohana 12:12-12, Ufunuo 7:9-10

Jinsi ya Kustawi kama Mtende

Zab.92:12-15
.
Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni

1. Ishi maisha ya Haki, unaweza kujiuliza mtu wa haki ni Mtu wa namna gani
a. Hawana muda wa Kuaibisha wengine Mt. 1:19
b. Hukaa katika maagizo ya Bwana bila lawama Luka 1:5-6
c. Anakuwa Mcha Mungu Luka 2:25
d. Utamtegemea Mungu katika hali zote ziwe njema au mbaya na hatima yako ni ushindi
Warumi 8:33-39.

Yesu alipoingia Yerusalem alishangiliwa kwa matawi ya miti ya mitetende kumaanisha Ushindi, utawala na Amani ya Mungu wa Kweli Mt.21:8-9
Mwisho wa Yote, Utaishi Maisha Marefu, ukiwa na Matunda wakati wote, na hutayumbishwa na upepo wakati wote bila kujali ukame au mvua utazaa matunda na haya ndio mafanikio ya Mtende.

🌴 🤲 TUMTUKUZE, TUMWIMBIE, TUMSIFU, TUMSHANGILIE NA KUMWADHIMISHA. 🌴 🤲

A.r.S
 
Back
Top Bottom