Historia ya Mitaa mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam

Mtaa wa Swahili.

hauanzii shimoni kariakoo unaanzia msimbazi kariakoo unaishia nkrumah gerezani
 
Jamaa kawauliza asili ya mitaa na si urefu Wa mitaa.ndio maana div 5 haziishi.mnajibu msichoulizwa
 
mtaa wa Lindi...
Mtaa huu ndio mrefu kuliko mitaa yote hapa Dar.

Mtaa wa Agrey...
Huu ni mtaa wa pili kwa urefu Dar.

Mtaa wa Congo...
upo Kariakoo.
Huu ni mtaa ambao una pilika na Tashtiti kuliko mitaa yote Tanzania.
Halahala, Mtaa huu ukijishaua kuzubaa tu unaibiwa.

Mtaa wa Sikukuu...
Mtaa huu ni mtaa unaouza madiko diko usiku kucha.
Nenda muda wowote mtaa huu utapata Chakula.
huu pia uko Kariakoo.

Mtaa wa Chui...
Pia nao upo Kariakoo.
Ni mtaa unaoaminika kuwa na walaji Mirungi kuliko mtaa wowote Dar es Salam.

Mtaa wa Pemba...
Upo Kariakoo.
Umelaaniwa, hauna Lami.
kwa taarifa yako mtaa huu unapita katikati ya soko kuu la Kariakoo.

Mtaa wa Swahili.
Huu mtaa upo Kariakoo.
Mtaa huu unaanzia Kariakoo Shimoni unaishia Gerezani.

Mtaa wa Twiga.
Upo Kariakoo.
Ndipo lilipo jengo la club yenye mafanikio zaidi hapa nchini.
Hapa naizungumzia club ya YANGA.

Itaendelea...
Mkuu naona Umebuni tu Mtaa Mrefu kuliko yote Dar nadhani ni Mtaa wa Uhuru Umeanzia city centre Clock Tower hadi Buguruni kwenye Mataa Lindi haufui Dafu labda Uhuru iitwe Barabara
 
Nnamdi Azikiwe alikuwa ni kiongozi wa kwanza wa Nigeria mara baaya uhuru wa nchi hiyo. Barabara yetu ile maarufu imepewa jina hilo kama kumbukumbu yake. Alifariki mwaka 1996.

Samora Machel naye, kama Azikiwe, alikuwa ni kiongozi wa Msumbiji aliyepinga utawala wa amakaburu wa Afrika Kusini. Alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1986. Mjane wake ndio mke wa Mandela wa sasa.

Hassan Omari Makunganya alikuwa kiongozi wa Wangindo (sina uhakika sana na kabila). Aliongoza watu wake kupigana na Wajerumani dhihi ya utawala wa Wajerumani. Alishirikiana na akina Kinjekitile Ngwale katika vita iliyojulikana kama Majimaji (1905 - 1907)

Umetusaidia katika misingi ya majina ya mitaa hiyo lakini umechanganya sehemu hii "makunganya hakushiriki vita ya majimaji maana alifariki mwaka 1894 kwa kuuawa na wajerumani.
 
Sio mwenyeji wa huu mji wa Dar na ninahitaji kupita sehem kadha wa kadha kutafuta hili na lile.
 
References za Dar es salaam ni vichekesho - Bar, Msikiti, Kanisa, Mwembe, Mnazi, Soko, Rangi ya nyumba, Mkaanga chips, Transforma ya Umeme, Duka, Ofisi ya ccm, Sheli nk.

Maelezo yaweza kuwa hivi:

Shuka kituo cha Malapa, Kata kona kwenye sheli hadi ukute minazi mingi. Ulizia Msikiti wa Mzee Nassoro. Fuata njia pembeni mwa Msikiti hadi Bar ya makuti inaitwa Kula Raha Bar. Ukifita hapo ni beep nikufuate.

Tuna miji isiyo na mipango miji.
 
Hahahaha,hii kali,ndio ile ya Mrisho Mpoto,maana hadi mama muuza mihogo ni ID
 
Sasa wewe sijui kama nikikuelekeza kama utafika home maana unaweza ukajikuta unakatiza Chooni na bafuni ili uje kwetu
 
Sio mwenyeji wa huu mji wa Dar na ninahitaji kupita sehem kadha wa kadha kutafuta hili na lile.

kama unatokea sea cliff masaki unaenda posta samora avenue tumia toure drive mpaka inapokutana na kenyatta then kata kushoto nenda na kenyatta mpaka inapokutana na ali hassan mwinyi road kata kushoto nenda moja kwa moja hadi inapokutana na ohio,nyoosha hadi inapokutana na azikiwe drive kata kushoto nenda mpaka round about ya bismini kata kulia kuingia samora avenue.

mkuu hata dar kuna mitaa na ina majina. msichukulie dar nzima ni kama mabondeni walipovamia na kujenga. kinondoni,temeke,ilala,magomeni,upanga,mwananyamala etc kote kuna mitaa uliza wenyeji mtaa unaoenda utaelekezwa.
 
sema uzuri hutapotea
Weee !! usije ukajaribu. Siku moja, tena mchana wa saa nne niliamua kutoka Soko la Kinondoni kwenda Kinondoni Moscow kule karibu na mto unaotenga Magomeni na Mkwajuni kwa mguu. Nilitaka nipite njia ya kule chini (kando kando ya mto unaotenga Muhimbili Hospitali na Kinondoni. Mpaka saa 12 jioni ndipo nilikuja kushituka nipo karibu kabisa na msikiti wa Kinondoni Moscow...!! siwezi kuisahu siku hiyo. Pia kilichonigharimu ni kuogopa kuuliza maana kipindi hicho kulikuwa na vibaka hatari tena wa rika (wazee kwa vijana)zote na jinsia zote (wa kike na wakiume)...Nikajua nikiuliza tu nimekwenda na maji!!

Na sisitiza Usijaribu !!!
 
Kama hujui tunaelekezanaje...usije Kigamboni, maeneo ya Tungi, utapotea!
 
Kama hujui tunaelekezanaje...usije Kigamboni, maeneo ya Tungi, utapotea!

hivi zile barabara kuu mbili za kigamboni zinaitwaje?? moja ile ukitoka ferry unanyoosha,ingine ukitoka ferry unakata kulia hadi kwenye gas station unakata kushoto kuelekea hospitali. zinaitwaje hizo??
 
Weee !! usije ukajaribu. Siku moja, tena mchana wa saa nne niliamua kutoka Soko la Kinondoni kwenda Kinondoni Moscow kule karibu na mto unaotenga Magomeni na Mkwajuni kwa mguu. Nilitaka nipite njia ya kule chini (kando kando ya mto unaotenga Muhimbili Hospitali na Kinondoni. Mpaka saa 12 jioni ndipo nilikuja kushituka nipo karibu kabisa na msikiti wa Kinondoni Moscow...!! siwezi kuisahu siku hiyo. Pia kilichonigharimu ni kuogopa kuuliza maana kipindi hicho kulikuwa na vibaka hatari tena wa rika (wazee kwa vijana)zote na jinsia zote (wa kike na wakiume)...Nikajua nikiuliza tu nimekwenda na maji!!

Na sisitiza Usijaribu !!!
haha hahahaha duh ,, pole
 
hivi zile barabara kuu mbili za kigamboni zinaitwaje?? moja ile ukitoka ferry unanyoosha,ingine ukitoka ferry unakata kulia hadi kwenye gas station unakata kushoto kuelekea hospitali. zinaitwaje hizo??

Mh! Hivi zina majina???
 
Weee !! usije ukajaribu. Siku moja, tena mchana wa saa nne niliamua kutoka Soko la Kinondoni kwenda Kinondoni Moscow kule karibu na mto unaotenga Magomeni na Mkwajuni kwa mguu. Nilitaka nipite njia ya kule chini (kando kando ya mto unaotenga Muhimbili Hospitali na Kinondoni. Mpaka saa 12 jioni ndipo nilikuja kushituka nipo karibu kabisa na msikiti wa Kinondoni Moscow...!! siwezi kuisahu siku hiyo. Pia kilichonigharimu ni kuogopa kuuliza maana kipindi hicho kulikuwa na vibaka hatari tena wa rika (wazee kwa vijana)zote na jinsia zote (wa kike na wakiume)...Nikajua nikiuliza tu nimekwenda na maji!!

Na sisitiza Usijaribu !!!

Mkuu umenichekesha sana.
 
Back
Top Bottom