Historia ya makabila nchini katika ramani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Historia ya makabila nchini katika ramani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quemu, Oct 7, 2009.

 1. Quemu

  Quemu JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Jun 27, 2007
  Messages: 986
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Nilifanikiwa kukumbana na ramani ya Tanganyika ya mwaka 1956 ikiwa imegawanywa kwa makabila.

  Historia inatuambia kuwa kuna makabila kama 125 nchini. Je twayajua yote?

  Kuna makabila mengi tu nilikuwa sifahamu kama yapo mpaka nilipokumbana na hii ramani.

  Mfano:
  Magharibi - Holoholo, Tongwe, Bende, Konongo, nk
  Kusini Juu - Wungu, Sangu, Nyamangwa, Nyima, nk
  Kaskazini - Nyambo, Subi, Simbwa, nk

  Kwa bahati mbaya atlas nilipotoa hii ramani ilikuwa kubwa mno. Kwa hiyo ilinilazimu kupiga picha kwa vipande vipande.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Hii ya makabila zaidi ya 120 naona kama ni stretch...
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Definition ya kabila hako fixed scientifically, kwa hiyo it is hard to say. Makabila ya Tanzania kama yanavyohesabiwa sasa yapo zaidi ya 120, mengi ya haya ni madogo na yasiyojulikana kama hayo hapo juu.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 7, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Okay chukulia kwa mfano Kisukuma. Wasukuma wa Ntuzu kisukuma chao kiko tofauti na Kisukuma cha Nzega, Mwanza, na Shyinyanga mjini. Sasa Kisukuma hichohicho na Kinyamwezi eti ni lugha tofauti kwa hiyo kufanya hayo makabila mawili kuwa tofauti.

  Kwa nini wote hao wasiwe kabila moja maana lugha yao ni karibia ile ile ukiachilia vitofauti vidogo vidogo vya misamiati, matamshi, n.k. Kama Kisukuma kina variaties mumo kwa mumo na bado ni Kisukuma basi nadhani hata Kinyamwezi na Wanyamwezi bado ni Wasukuma tu na hivyo kwa maoni yangu wote ni kabila moja.

  Halafu hayo makabila madogo ndio yepi hayo? Maana mimi sijawahi kukutana na watu wengi wanaotokea kwenye hayo makabila madogo.
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Makabila madogo ni derivatives ya kabila kubwa! Kwahiyo naugana na wazo lako kuwa Tanzania HAKUNA makabila 120! Yawezekana yapo si zaidi ya kumi.

  Mkoa wa Kagera: Wapo Wahaya, Wanyambo, Waangaza, Wasubi, Wakerebe na Waha.

  Tukishavuka Ziwa Victoria hawa wote wanaitwa Wahaya! Kwahiyo mkoa wa Kagera kuna kabila MOJA - ukiachilia tofauti ya utamshi wa maneno, parameters nyingine ziko sawa sawa (chakula, kilimo, ufugaji, ujenzi, e.t.c)
   
 6. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wa makabila madogo huwa hawajitambulishi kabisa,kama mkwere atakuambia yeye mzaramo,mkoto atakuambia mimi Msukuma au Mnyamwezi, msisi atakuambia mimi mdigo, mpetwele atakuambia mimi Mfipa,Mkahe atakuambia mimi mchaga, etc
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wakati huo kweli makabila hayo yalikuwepo lakini muda unavyozidi kwenda makabila yanatoweka shauri ya intermarriages, urban migration ya hali ya juu.Makabila yaho yalikuwepo yes mengine bado yapo mpaka sasa yapo lakini hayasikiki kabisa sababu hizo
   
 8. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  Hapo umechemsha Baba Enock, unaponganisha makabila ambayo source yake ni tofauti, mf wasubi walitokea maeneo ya burundi wakati wahaya inaaminika wametokea sehemu za uganda. haya ni makabila tofauti kabisa, linalofanya kabila moja lijulikane kuliko kabila jingine ni swala la maendeleo na umaarufu, mfano wahaya ni kabila lililoendelea kwanza kati ya makabila yote ya mkoa wa kagera ndo maana likachukua status ya mkoa wote, lakini si kweli kwamba watu wote wa kagera ni wahaya kwani ancestors wao hawakutoka sehemu moja!! Nadhani umeelewa. Kama vp muulize Mac De Melo utapata maelezo ya kina!
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Bongo kuna makabila lukuki, mengine ukisia hadi unashangaa.
  Mfano mkoa wa Mbeya ambao upo nyanda za juu kusini una makabila zaidi ya ya sita
  Kabila kubwa ni Mnyakyusa lakini kuna mnyiha, mnyika, mndali, msafwa,mmalila na mnyamwanga makabila haya yote lugha zinaingiliana.
  _ Ukija Kagera kabila kubwa ni mhaya, lakini utakuta kuna mwangaza, mnyambo, msubi na wakereke. Wote hawa lugha ni mwingiliano.
  _ Ukienda Iringa kabila kubwa kule ni muhehe, lakini kuna mbena, mkinga,mpangwa,mbena manga na mmanda hawa nao lugha zinaingiliana tu.
  Hivyo kwa namna moja au nyingine makabila ya kweli utakuta yapo 20, sema hayo mengine yamejitokeza kutokana na mambo ya migration.
   
 10. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  Muha si Mhaya...Au ni mhaya aliye pungukiwa.Lakini haimfanyi kuwa mhaya.Kigoma sio kagera...ndio maana pakawa na mikoa si muha sio mhaya wengine unaweza sema lakini sio muha.
   
 11. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni vizuri kama makabila yakaweza kuimarishwa badala ya kuyangamiza pia kuzienzi lugha za hayo makabila kwa ujumla .
   
 12. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Usipotoshe watu wakerewe wako ukerewe na kisiwa hicho kiko mkoa wa Mwanza, waha wako mkoa wa Kigoma na wala siyo Kagera. wanyambo(Karagwe, wahangaza na siyo waangaza(Ngara)wasubi (Biharamulo)ndo pekee wako mkoa wa Kagera.
   
Loading...