Watu hujiuliza wana uhusiano na Waisilamu,Waisilamu Wanafuga Majini?
Majini ni viumbe wa Mwenyezi Mungu wameumbwa miaka 2000 iliyopita kabla ya kuumbwa mwanadamu,wao wanatuona sisi hatuwaoni,Jini ameumbwa kutokana na moto binadamu ameumbwa kutokana na mchanga na maraika wameubwa kutokana na nuru na kuna tofauti kati ya jini na shetani,jini akiwa mbaya anaitwa shetani
Majini huka wapi?majini wanapenda kuishi sehemu tulivu ambazo hawakai watu,vilevile wanapenda kukaa katika misitu mikubwa na majabali,vilevile wanaweza kukaa pamoja na watu majumbani mwao. Wengine wanapendelea kukaa chooni, lakini hawakai chooni wale majini waisilamu bali ni wale makafiri wachafu ambao wanapenda vitu najisi vichafuvichafu. Ndiyo maana kwa Waisilamu kuna dua huwa inafundishwa ambayo unapoingia chooni inabidi uisome ili usipatwe na jini, na sehemu za baharini majini wanapendelea sana kuishi
Na kuna aina tatu ya majini aina ya kwanza majini wenye mabawa na wanaweze kuruka,
aina ya pili ni wale ambao unaweza kuona joka au ng'e,. Aina ya tatu ni wale ambao wana hamahama kwenda maumbile mengine na majini nao wana sheria ambazo zinawabana kama binadamu. Mfano wanapaswa kumtii Mungu na kuswali. Wanapaswa kumtii mtume kama vile binadamu tunavyofanya, kwenda Makka kama sisi tunavyofanya, kama vile Muisilamu inavyobidi kufanya na majini nao inabidi kufanya hivyo
Majini wanawagopa sana binadamu tofauti na binadamu wanavyowagopa, na ukiwaogopa unawapa kichwa, na ndiyo maana katika Uisilamu kuna dua za kujikinga na majini, na wana tabia kama unavyoziona za wanadamu. Kuna majini wacha Mungu, wezi, malaya mashoga, na hata washirikina. Yaani kila tabia uliyonayo mwanadamu basi na majini wanayo