Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,734
Binadamu wa kwanza katika historia ya Dubai aliishi hapo takriban miaka 3000 BCE (Before Christian Era) wakati huo waliishi watu wa jamii ya nomadic watu ambao ni wafugaji na wawindaji na hawakuishi katika sehemu moja.
Katika karne ya tatu katika (Christian Era) sehemu hii ilitawaliwa na Ufalme wa Sassanid Persia ya kati ambayo ni Irani ya sasa, utawala huo ulidumu mpaka karne ya saba, ambapo Khalifa Umayyad alitwaa madaraka na kuingizi dini ya Kiislam katika sehemu hii.
Eneo hili lilikuwa maarufu kwa uvuvi, pia watu walitafuta pearl kutoka kwenye samaki aina ya oyster kwa maelf ya miaka. Kumbukumbu za kwanza za mji ni mwaka 1799 wakati ukoo wa Bani Yas ulipoiweka kama sehemu tegemezi ya Abu Dhabi.
Dubai ilikuwa falme iliyojitenga ya Sheikh mwaka 1833, wakati Al-Maktoum aliyetokea ukoo wa Bani Yas (wenye asili yao Abu Dhabi) alipolichukua eneo kwa amani.
Kugundulika kwa pearl za kutengeneza na kuyumba kwa uchumi wa dunia 1929 kulisababisha kuanguka kwa soko la pearl la kimataifa, matokeo yake Sheikh Saeed aliangalia njia nyingine za kuinua uchumi wa Dubai, na na kuifanya moja ya bandari zinazoongoza kwa kusafirisha mizigo duniani.
Mwaka 1966 mafuta yaligundulika Dubai, hii ilibadilisha nchi kupita maelezo na kuifanya Dubai kuwa nchi ya kisasa na kituo cha biashara cha dunia.
Mfanya biashara wa pearl 1849
Watafutaji wa pearl.
Ukoo wa Maktoum ambao ndio watawala wa Dubai.
Kyalow