Historia: Upasuaji wa Kwanza wa Moyo wafanyika Duniani

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
653
SIKU KAMA YA LEO

Mwaka 1967 kwa mara ya Kwanza Daktari Christiaan Barnard kutoka nchini Afrika Kusini aliandika historia ya Kuhamisha Moyo wa Binadamu kwenda kwa mwingine (human to human heart transplant) hii ilikuwa haijawahi tokea duniani.

Tukio hili lilifanyika Mjini Cape Town katika hospital ya Groote Schuur ambapo alishirikiana na Madaktari wengine 31 wakitumia masaa 5.

Moyo huo ulihamishwa kutoka kwa Binti wa miaka 25 aliyeitwa Denise Darvall ambaye alikufa kwa ajali mapema asubuhi, Kisha ukawekwa kwa baba yake Louis Washkansky mwenye miaka 51 ambaye alikuwa hapo hapo hospitali akiwa mgonjwa (Baba na Mwana)

Baba wa kijana aliyehamishiwa Moyo aliishi kwa moyo ule siku 18 tu na Kufa kutokana na ugonjwa wa mapafu (pneumonia)

Mgonjwa wa Pili kupokea moyo kutoka kwa mtu mwingine, Naye alikua South Africa, aliitwa Philip Blaiberg na aliishi kwa miezi 19.

Mbinu hii inatumiaka mpaka leo, Japo wagonjwa waliofanyiwa Hivi huishi mda mfupi, lakini mpaka sasa mgonjwa aliyepokea moyo mpya huishi mpaka miaka 5.

Christian Daktari aliyefanya upasuaji huo alizaliwa katika familia Maskini ya Muhubiri mkaburu huko Cape town, Akasoma Elimu ya Tiba katika chuo kikuu cha Cape town kisha kuendelea na Diploma ya Upasuaji chuo kikuu cha Minnesota huko Marekani.

Katika Picha ni Kumbukumbu ya Kitanda ambacho upasuaji huo ulitokea.

Polycarp Mdemu

FB_IMG_1701598762984.jpg
FB_IMG_1701598765335.jpg
FB_IMG_1701598767555.jpg
 
Kwa kawaida au mara nyingi ya hizi transpalnt,mwili hua unazireject na mgonjwa hufa,miili ya binadamu inatofautiana,
Organs zetu zinajuana hivyo ikiingia organ nyingine,mara nyingi organs zingine husitisha kufanya kazi na organ iliyoingia kwenye huo mwili,

Hii hali inaitwa Organ rejection,When the organ recipient's immune system recognizes the donor organ as foreign and attemp to eliminate it.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom