Historia: Tulipotoka na tulipo

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,543
14,451
Naanzia kushoto kwenda kulia
1) Salim Ahmed Salim
2) Joseph Sinde Warioba
3) Rashid Mfaume kawawa
4) Julius Kambarage Nyerere
5) Ali Hassan Mwinyi
6) Idrissa Abdul Wakiil
7) Maalim Seif Sharif Hamad

N: waliohai hapo ni wawili
Joseph Sinde Warioba
Salim Ahmed Salim

IMG-20240308-WA0005.jpg
 
IMG-20240310-WA0023.jpg

Mandhari ya eneo la bandari ya Dar es salaam mnamo mwaka 1975. Jengo hili upande wa kushoto ni la Mahakama Kuu. Hapo ndio Bititi na Kipaka na wengine walikuwa wanahojiwa mashtaka ya kupindua serikali. Wakili wao akawatetea ya kwamba hawakutaka kupindua Serikali bali wanataka kubadilisha uongozi. Siasa mchezo mchafu.
 
Naanzia kushoto kwenda kulia
1) Salim Ahmed Salim
2) Joseph Sinde Warioba
3) Rashid Mfaume kawawa
4) Julius Kambarage Nyerere
5) Ali Hassan Mwinyi
6) Idrissa Abdul Wakiil
7) Maalim Seif Sharif Hamad

N: waliohai hapo ni wawili
Joseph Sinde Warioba
Salim Ahmed SalimView attachment 2932486
kila zama na kitabu chake 🐒

maisha ni hadithi,
tujitahidi kila moja wetu kuwa na hadithi nzuri, kwa hao watako kuja kusimuliwa 🐒

Ramadan Kareem
 
IMG-20240312-WA0016.jpg

Huyu ni Sewa Haji.
Princess Margaret hospital ilifunguliwa 1959 baada ya kufungwa Kwa Sewa Haji Hospital ambayo ilipakana na gereza la rumande kabla ya hiyo gereza kuhamishiwa Keko Magurumbasi. Kituwo kikuu Cha Polisi mjini Dar ndipo hiyo gereza ilpokuwepo.

IMG-20240312-WA0018.jpg

Dar long time ago
Princess Margaret Hospital ambayo baadaye ilikuja kuitwa Muhimbili Hospital.
Kazi Kwa vitendo
 
IMG-20240312-WA0013.jpg


1923 wapagazi wakiwasili Kigoma.
Safari ilikuwa ndefu Sana toka mikoa ya kanda ya Kati.Nadhani wengi walipoteza maisha njiani


NOTE: Porters Kwa Kiswahili ni wapagazi
 
Ni maeneo ya Posta mpya jijini Dar es salaam. Pichani jengo hilo lenye mnara ni kanisa la Anglican la Mt Albano miaka ya 1950. Barabara hiyo yenye mshale ( ni Ghana Evenue kwa sasa.) inatoka Mtaa wa Azikiwe ina kwenda moja kwa moja mpaka Wizara ya mambo ya ndani ya nchi na inakutana na mtaa wa OHIO. Mbele kidogo ya hilo gari sikuhizi pamejengwa jengo maarufu la EXIM TOWER. Kweli tumetoka mbali sana.

Sasa kama posta ilikuwa hivyo hebu fumba macho kisha waza Buza hakukuwa na Simba kweli 🤣🤣🤣

Kipindi hicho ukienda Tabata kuna uwezekano ukaliwa na fisi 🤣🤣🤣🤣
IMG-20240315-WA0007.jpg
 
IMG-20240320-WA0042.jpg


Yaani hapo wengine mnakaa huku , wengine mnakaa upande mwingine na wote mnaona tena picha kubwa tu kama ambazo sasa hivi inaitwa Projector

Daaah hizi muvi zilibamba sana enzi hizo mpaka wajinga wakaamini kuwa huyo ni yesu Yaanj mpaka wasiojielewa wanasema huyo ni yesu daaaah Mungu awasamehe
 
Meli ikiingia bandarini Jijini Dar es salaam, miaka ya 1970. Sehemu hiyo penye mshale ndiyo Kivukoni ambapo siku hizi tunapandia Pantoni kwenda Kigamboni.
IMG-20240320-WA0048.jpg
 
Kama ulikuwa hujui,

Picha inaonesha Mwaka 1972, Dar es Salaam Rais Jaffery Nimeiry wa Sudan akikagua wachezaji wa Taifa Stars waliokuwa vifua wazi. Kapten Abrahaman Juma akimtambulisha kwa Omary Zimbwe, Mohamed Chuma, Kitwana Manara na Abdalla KIbadeni. Rais J. K. Nyerere alikuwa Jukwaa Kuu. Inasemekana, Jezi za Taifa Stars zilikuwa zimepelekwa kwa Mganga wa Kienyeji ili ishinde siku ya mechi. Meneja wa Taifa Stars alizifuata lakini bahati mbaya hakumkuta Mganga nyumbani kwake, Kwakuwa alikwenda na basi la timu, ilibidi wachezaji waende uwanja wa Taifa kwa miguu toka Hosteli ya Jeshi la Wokovu, Kurasini. Meneja wa taifa stars alikuwa ni Chambanga H. Dyamwale mnamo 1972. Kutokana na fedheha hiyo kubwa, inasemekana Rais Nyerere alisusa kukanyaga tena mpirani.

Tulianza na mkosi toka zamani 😎🙌⚽

IMG_20240416_154245_231.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom