Historia ni Albamu ya Zamani, Hata hii ya Marekani kukamata Marais wa nchi nyingine si picha ngeni

Historia ni Albamu ya Zamani, Hata hii ya Marekani kukamata Marais wa nchi nyingine si picha ngeni

Fascinating

Member
Joined
May 14, 2025
Posts
93
Reaction score
224
Historia ni kama albamu ya zamani; hakuna kitu kipya, ni picha zinazojirudia. Hata kukamatwa kwa Nicolás Maduro na Marekani wala si suala geni kihivyo.

Kurasa zote za habari hivi sasa zinafuatilia kilichotokea Venezuela. Wengi wameliona tukio hili kama la kushangaza baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza kuwa vikosi vya nchi hiyo vimemkamata Maduro kufuatia shambulio la ghafla mjini Caracas mnamo Jumamosi, Januari 3, 2026. Lakini ukiitazama albamu ya historia, utagundua kuwa Marekani imekuwa ikifanya hivi kwa zaidi ya karne moja.

Viongozi Waliokamatwa na Marekani:

Hii ni orodha ya viongozi wa mataifa mbali mbali ambao Marekani iliwatia Mbaroni:

Nicolás Maduro (Venezuela, 2026):
Baada ya kuiongoza Venezuela kwa takriban miaka 12, Maduro sasa amekamatwa na kusafirishwa kuelekea New York.​
Anakabiliwa na mashtaka mazito ya "narco-terrorism" na kuhusika na biashara ya dawa za kulevya, jambo ambalo Marekani imelitumia kama uhalali wa operesheni hiyo ya ghafla licha ya Kuibuka kwa mijadala mingine inayotaja utajiri wa mafuta wa nchi hiyo na sera ya utaifishaji wa sekta hiyo miaka 1970.​
IMG_3144.jpeg
Saddam Hussein (Iraq, 2003):​
Picha hii inatukumbusha uvamizi wa Iraq. Saddam alitafutwa kwa miezi kadhaa hadi alipokamatwa akiwa amejificha kwenye shimo (spider hole).​
Marekani ilimkabidhi kwa serikali mpya ya Iraq ambapo alihukumiwa na kunyongwa, tukio ambalo lilibadilisha sura ya siasa na usalama wa Mashariki ya Kati hadi leo hii.​
IMG_3143.jpeg
Manuel Noriega (Panamá, 1990):​
Huyu alikuwa dikteta na mtawala wa kijeshi wa Panama. Marekani iliamua kuivamia nchi hiyo kumkamata kwa makosa ya kusafirisha mihadarati na utakatishaji fedha.​
Noriega alichukuliwa kama mfungwa wa kivita na kufungwa gerezani nchini Marekani, Akiwa mfano wa mapema sana wa kuonesha jinsi Marekani inavyoweza kuingia nchi nyingine kumng'oa kiongozi.​
IMG_3145.jpeg
Emilio Aguinaldo (Ufilipino, 1901):​
Hapa ndipo albamu inapoanzia. Aguinaldo, Rais wa kwanza wa Ufilipino, alikamatwa na vikosi vya Marekani wakati wa vita kati ya nchi hizo mbili.​
Kukamatwa kwake kulimaliza tofuti rasmi kati ya nchi hizo na kuimarisha utawala wa Marekani nchini humo kwa miongo kadhaa.​
IMG_3141.jpeg

Rais Trump amesema kuwa Marekani "itaisimamia" Venezuela kwa muda hadi mabadiliko ya uongozi yatakapofanyika. Hata hivyo, Umoja wa Mataifa (UN) na wachambuzi wa sheria za kimataifa wameingiwa na hofu; je, huu ni mwisho wa uhuru wa mataifa madogo?

Kesi inayomkabili Maduro kwa kwasasa inaweza kuchukua sura mpya kama atarejeshwa Venezuela, kipindi utawala wa nchi hiyo umeshabadilika na umekuja ule unaofungamana na sera za Marekani. Mabadiliko ya utawala yanaweza kuja na shtuma za uvunjifu wa haki za binadamu, kitu kichoweza kupelekea yamkute kama ya Saddam Hussein, kama ukurasa wa uhalifu utafunguliwa.
 
Back
Top Bottom