Historia mpaka ulipofikia

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
Habari wakuu:

Ninaomba ushirikiano wenu wakuu,,najua kuna wana jf wengi sana hapa ambao wamefanikiwa sana hasa katika nyanja ya biashara au tuseme ya kipato,,lakini kufika hapo mlianzia mbali sana.

Kwa niaba ya wale watakaopendezwa na post hii,ninaomba wana jf mliofanikiwa mtupe full mkanda mpaka mlipo fikia..vikwazo mlivyovipitia na jinsi mlivyokabiriana navyo,,tushirikishane ili tujifunze kutoka kwenu na sisi tufanye kitu fulani.

Maana mimi ninajua historia ya bill gate lakini sijui historia ya watanzania wenzangu waliofanikiwa katika mazingira ninayoiishi,,,najua historia zenu zitakuwa na mchango mkubwa sana kwa wanajamii hapa..

Natanguliza shukurani zangu wakuu.
 
Duh! password...au..interview?
Haya MLIOFANIKIWA, watu wanataka kupata Historia zenu!
 
Wengi wamepata pesa kwa njia zisizo halali.
Wengi ni wakwepa kodi na wasio waaminifu.
Kupata historia zao itakuwa ngumu sana.
 
Wengi wamepata pesa kwa njia zisizo halali.
Wengi ni wakwepa kodi na wasio waaminifu.
Kupata historia zao itakuwa ngumu sana.

Kwa hiyo una maana wana JF wote sio waadilifu hasa waliofanikiwa katika shughuli zao?
 
Ingekuwa vema kama ungeweka kwanza historia yako ya KUTOFANIKIWA mpaka hapo ulipo!
 
Habari wakuu:

Ninaomba ushirikiano wenu wakuu,,najua kuna wana jf wengi sana hapa ambao wamefanikiwa sana hasa katika nyanja ya biashara au tuseme ya kipato,,lakini kufika hapo mlianzia mbali sana.

Kwa niaba ya wale watakaopendezwa na post hii,ninaomba wana jf mliofanikiwa mtupe full mkanda mpaka mlipo fikia..vikwazo mlivyovipitia na jinsi mlivyokabiriana navyo,,tushirikishane ili tujifunze kutoka kwenu na sisi tufanye kitu fulani.

Maana mimi ninajua historia ya bill gate lakini sijui historia ya watanzania wenzangu waliofanikiwa katika mazingira ninayoiishi,,,najua historia zenu zitakuwa na mchango mkubwa sana kwa wanajamii hapa..

Natanguliza shukurani zangu wakuu.

Kipimo cha mafanikio ni kipi? kila mtu ana kiwango chake anachoamini kuwa ni mafanikio. Nilipotaka kupata shamba ili hali sina hela ilibidi nifanye kibarua kigumu sana wakati wa likizo. Nilikuwa nabeba nyanya za jamaa pale Image Iringa kila siku jioni kwa muda umbali wa kilomita tano, napiga trip tano. Nikakusanya kiasi kilichotosha kupata eka kumi za ardhi. Wenzangu tuliokuwa umri mmoja walianza kuona kama mimi nimefanikiwa, kumbe kwa kipimo changu ilikuwa bado. Njia/historia za kufikia mafanikio kwa tulio wengi ziko gizani, huwezi kuzipata kirahisi, zaidi sana utapewa hadithi feki. Ni wachache mno ktk jamii yetu wanaoweza kukupa ukweli.
 
Back
Top Bottom