Historia hii ya Wandali na Wanyakyusa imekaaje?

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,664
22,256
Habari wanaJF,

Naangalia Tanzania Safari Channel, msimulizi anasemaje Wandali na Wanyakyusa walitokea Kongo. Walipita Morogoro na milima ya Livingstone mpaka Rungwe, wajuzi wa historia hii imekaaje, ukizingatia Wamyakyusa na makabila ya kaskazini mwa Malawi yana uhusiano mkubwa wa lugha, mila na desturi kuliko Kongo?

Hebu tujuzane.

=====

1597309798336.png

1597309839842.png

1597309870557.png

Kuwa na mahusiano na Wamalawi haimaanishi kwamba hawakutokea Kongo.Tamaduni za watu huwa zinaathiliwa na mazingira pia kwa sababu hawa watu walikua wanasafiri na kama ujuavyo hizo safari zilitukua muda mrefu ,so ni rahisi kuathilika na tamaduni za mahali husika.
 
Wewe jua tu kwamba wapo Mbeya. Ukisikiliza masimulizi ya Wanyakyusa kuhusu asili ya ni uongo mtupu. Kila mmoja anasimulia ajuavyo, wengine wameshaanza kudai eti walitokea Lupaso.

Wengine wanadai walitokea Mexico, wengine Libya, wengine Kongo, wengine South Africa, wengine Morogiro, Wengine Sudan, wengine Zimbabwe, eengine Los Angels, wengine eti Birmingham.

Wengine wanadai walitokea Shanghai, wengine Guangzu, wengine Commoro, wengine Pemba, wengine et Dar es salaam, Wengine Madinna, wengine Tehran, wengine Florence, wengine, Abu ka Syria, wengine beiruti.
Usije ukawatilia maanani kabisa wanapoanza kusimulia asili yao.
 
Wewe jua tu kwamba wapo Mbeya. Ukisikiliza masimulizi ya Wanyakyusa kuhusu asili ya ni uongo mtupu. Kila mmoja anasimulia ajuavyo, wengine wameshaanza kudai eti walitokea Lupaso...
Hii inahusu TBC kurusha historia ambayo huenda si sahihi, italeta picha gani kwa nchi.
 
Mimi niliwahi kuhadithiwa na late babu yangu kwamba baba zake walitoka South Africa.
Kwahiyo wandali na wanyakyusa wametoka South,wakatua Rungwe,wengine wakaenda undali.
 
Hapana ni kijana wa kinyakyusa anajiita chifu, hapa hoja ni TBC kurusha jambo ambalo huenda si sahihi, msimulizi angesema wametokea kusini kupitia Malawi nisingekuwa na shaka sana.
Huyo kijana ni Mkongo, analazimisha wanyakyusa wote wawe wakongo kama yeye.
 
Hapana ni kijana wa kinyakyusa anajiita chifu, hapa hoja ni TBC kurusha jambo ambalo huenda si sahihi, msimulizi angesema wametokea kusini kupitia Malawi nisingekuwa na shaka sana.
Kama alivyosema mkuu proxy ni kuwa wanyakyusa kuhusiana na wamalawi kwa lugha au tamaduni haimaanishi kuwa wana asili moja, hayo yote huchangiwa zaidi na mazingira waliyofikia na kuadopt lkn origin yao inabaki pale pale.
 
Mimi niliwahi kuhadithiwa na late babu yangu kwamba baba zake walitoka South Africa.
Kwahiyo wandali na wanyakyusa wametoka South,wakatua Rungwe,wengine wakaenda undali.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ohoo! Nami niliwahi kuhadithiwa kuwa wana asili ya south sudan, mzee mwingine aliwahi kuniambia sijui wana asili na kabila flani kutoka nigeria nimelisahau. Sasa asili ya kweli ni ipi!
 
Kama alivyosema mkuu proxy ni kuwa wanyakyusa kuhusiana na wamalawi kwa lugha au tamaduni haimaanishi kuwa wana asili moja, hayo yote huchangiwa zaidi na mazingira waliyofikia na kuadopt lkn origin yao inabaki pale pale.
Wamalawi wa kaskazini na wanyakyusa walitoka kusini mwa Afrika, wamalawi waliishia Malawi na wanyakyusa waliendelea na safari na kusambaa Kyela mpaka Rungwe, vinginevyo tuaminiwalitoka Kongo?

Wakapita wapi mpaka Morogoro ambako note huko hawakuaacha manyoya mpaka wakapanda milima ya Livingstone na kufika Rungwe kisha wengine waliendelea mpaka Malawi! Bado ninahitaji kujua zaidi.
 
Wamalawi na wanyakyusa walitoka kusini mwa Afrika, wamalawi waliishia Malawi na wanyakyusa waliendelea na safari na kusambaa Kyela mpaka Rungwe, vinginevyo tuaminiwalitoka Kongo!?!?!?wakapita wapi mpaka Morogoro ambako note huko hawakuaacha manyoya mpaka wakapanda milima ya Livingstone na kufika Rungwe kisha wengine waliendelea mpaka Malawi! Bado ninahitaji kujua zaidi.

Mkuu embu check hii, inaonyesha wanatokea kwa wanubi huko

Nyakyusa people - Wikipedia
 
Sasa nimeamini kuwa walitoka Kongo, wanyakyusa ni waimbaji waziri na wanaongoza kwenye muziki wa Gospel nyuma ya wakongo.
 
Mwaseba ndo mke wa CHief pale Mwakaleli enzi hizo. Historia inasema huyu alitoka huko nilotian kipindi cha vita ni ukoo wa Queen Sheba,alitoroka na walinzi na walifika Morogoro,then wakateremka mdogo mdogo Songea, then safari ikaishia Mwakaleli.
Chief akaokota dodo akaoa.
Ndo wakaitwa Mwaseba,yaani watoto wa Sheba.wapo mpaka leo
Ndo mana Chief alikua mkali kweli kwa mabeberu wajerumani.
Mi ni wa ukoo huo. Kwenye vitukuu nimo
 
Heee! Kumbe humu JF of GT's wamo maprince! Wewe ni mtu mkubwa sana unahitaji walinzi tena waliobobea.
 
Back
Top Bottom