Ningependa Kuweka Kwa Ufupi Tu Historia Ya Disco Tanzania

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Wakuu Nimefanya utafiti sana wa jambo hili ningependa kuweka kwa ufupi tu historia ya Disco Tanzania.

Wakuu Richie Dillon alianza u’DJ 1984 Mwanza Alshars Tikkha Disco ndiyo DJ wa kwanza bongo kufanya mixing ya beat to beat miaka ya 1990 akiwa huko Mwanza na kuwapiga bao ma’DJ wa Dar.

Muziki wa Disco ulianza US katikati ya miaka 60 wakati huo ukijumuisha funk,soul,pop na salsa,mashabiki makubwa walikuwa jumuiya ya wanyamwezi (black Americans) walatino na Psychedelic (Mateja) na walikuwa wanajumuisha pia na live performance mfano wa disco ni Soul Train.

Mwanzo wa Disco ni New York chini ya DJ David Manuso ambapo alianzisha klabu ya wanachama tu nyumbani kwake na baadhi ya wanamuziki walipata umaarufu wa kuburudisha diskoni kwanza kama LaDonna Adrian Gaines maarufu kama Donna Summer ambaye alijulikana pia kama Queen of Disco na First Lady of Love.

Disco lilienea duniani na Tanzania hatukubaki nyuma kama Disco lilianza rasmi miaka ya 70 hususan mwaka 1971 ambapo maDj wa mwanzo wengi walikuwa wanamuziki kama Francis Bundala aka Dj Sweet Francis alikuwa muimbaji katika bendi aliyoianzisha mwaka 1964 ya The Screemers na Adam Salehe Mwambile aka Addy Sally(RIP)

Disco Tanzania lilianza katika hoteli ya Africana likijulikana kama GoGo Disco na DJ wa kwanza alikuwa Bhoka Wilson toka Southern Rhodesia wakati huo sasa ni Zimbabwe alikuwa pia muimbaji wa Cabbaret pale Simba Grill hoteli ya Kilimanjaro.

Mwaka 1972 Dj Sweet Francis naye akawa DJ hapo mpk mwaka 1973 ampako akaja DJ mwanamama toka South Afrika Dj Judy Kingui ambaye alikuwa mke wa mwanamuziki Kingui wa bendi ya The Rifters ambapo alihudumu mpaka mwaka 1975.

Mwaka 1972 likaanzishwa Disco la Sansui pale SeaView hotel chini ya Dj McTwist hakudumu sana na Addy Sally akawa Dj hapo.

Na mwaka huo 1975 Addy Sally alikuwa DJ Mlimani Park enzi za bumping.

Mwaka 1976 Addy Sally akaenda Arusha kuanzisha disco Arusha by Night na wakapata Cave Disco chini ya Dj Sweet Francis.

Kukawa kuna kushindana fulani kati ya hawa madj wawili kiasi cha kuweka wacheza show na mmoja wa wacheza show alikuwa Choggy Sly ambaye alikuja kuwa Dj maarufu pia.

Mwaka 1977 kukawa na mfumuko wa madisco kama Keys hotel Mbowe ambapo Dj Sweet Francis alikuwa hapo na kumfundisha kazi Dj Jerry Kotto.

Mwaka 1978 akaibuka Dj Luke Joe wakati huo akiwa sekondari na golikipa mzuri sana wa soka kwenye disco la Stereo ambapo lilipata umaarufu baada ya kuhamia hoteli ya Kunduchi

Miaka ya 80 ndiyo utitiri wa madisco uiibuka na madj wakali kama Niga Jay Saydou na Kalikali, Richie Dillon ambaye alianzia KUfanya Udj.wake Mwanza akaenda Nairobi Boomerang na kuja Dar Valentino Continental 7th Floor Bilicanas.

Wakuu Niishie hapa kwa leo nikija tena tutaanzia miaka ya 80.

Karibuni Kwa Mjadala

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Noma sana.

Source ni kumbukumbu zako ?
Source ni kutoka kwa Rafiki yangu anaitwa Ruff Yuko USA.
.
Yeye kazi yake ni mtayarishaji wa vipindi vya TV kwa sasa anataarisha makala ya chimbuko la Disco dhidi ya muziki wa dansi na muziki wa Bongo fleva wapi ulianzia.
.
Ingawa watu wengi wanamtaja Jah Kimbute ndiyo alianzisha kukusanya vijana wa kufoka kabla ya mashindano ya Yooh Rap Bonanza hayajaanza bahati mbaya sana Kimbute mwenyewe ameshatangulia mbele ya haki na Dj Kim hali kadhalika so kuna watu wanachukuwa ujiko usio wao.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
ila zamani udj aukuwa unalipa siku hizi vijana masaa kadhaa wanavuta mpunga mrefu tuuu kijana wangu ommy kichaa anavuta mpaka 1m kwa usiku tuu
 
ila zamani udj aukuwa unalipa siku hizi vijana masaa kadhaa wanavuta mpunga mrefu tuuu kijana wangu ommy kichaa anavuta mpaka 1m kwa usiku tuu
Ila yule jamaa anajua kucheza na instruments zake alipokuwa EA radio The cruise ilikuwa inabamba sana
 
Ingawa watu wengi wanamtaja Jah Kimbute ndiyo alianzisha kukusanya vijana wa kufoka
Umenikumbusha mbali, Jah Kimbuteh alinitangulia shule, mimi nimesoma darasa moja na mdogo wake, David Kimbuteh
kabla ya mashindano ya Yooh Rap Bonanza hayajaanza bahati mbaya sana Kimbute mwenyewe ameshatangulia mbele ya haki na Dj Kim hali kadhalika so kuna watu wanachukuwa ujiko usio wao
Mimi ndiye nilikuwa MC wa kwanza wa mashindano ya Yooh Rap Bonanza, enzi hizo yalifanyika ukumbi wa Langata, Kinondoni. Tenda nilipewa na Abdul Hakeem Magomelo (DJ Kim-RIP). Miongoni mwa wadhamini wa Yooh Rap Bonanza, ni tajiri Alex Massawe, a.k.a Mzee wa A.M.
P.
 
Umenikumbusha mbali, Jah Kimbuteh alinitangulia shule, mimi nimesoma darasa moja na mdogo wake, David Kimbuteh

Mimi ndiye nilikuwa MC wa kwanza wa mashindano ya Yooh Rap Bonanza, enzi hizo yalifanyika ukumbi wa Langata, Kinondoni. Tenda nilipewa na Abdul Hakeem Magomelo (DJ Kim-RIP). Miongoni mwa wadhamini wa Yooh Rap Bonanza, ni tajiri Alex Massawe, a.k.a Mzee wa A.M.
P.
Mbona DJ FA Mbowe hatujamuona kwa list? kuna mdau alitishia kufukua kabuli lako la uMC wako sijui kwa grill gani kule Kilimanjaro Hotel, unalizungumziaje hilo?
 
Wakuu Nimefanya utafiti sana wa jambo hili ningependa kuweka kwa ufupi tu historia ya Disco Tanzania.akuu Niishie hapa kwa leo nikija tena tutaanzia miaka ya 80.Karibuni Kwa MjadalaSent
Kwenye na DJ wa zamani, umemsahau John Peter Pantalakis.
Na DJ wa zamani ambaye bado ana DJ mpaka leo ni Niger J, kwa sasa ni Mtangazaji maarufu wa redio akitumia jina jingine.
p
 
JD ni miongoni mwa maDj wa kuanzia miaka ya 80 mwishoni ambaye alipata umaarufu zaidi baada ya kuanzishwa kwa Radio binafsi mwanzoni mwa miaka ya 90.
.
Kundi lake ni kina Kwa fujo Djs,Rankim Ramadhani yeye akitokea Morogoro ambapo baada ya kambi ya Mazimbu kuvunjwa wakati huo yuko kidato akuendelea na shule.
.
Ni mmoja wa maDj wenye vipaji vikubwa vya hii kazi kafanya kazi vyombo vya IPP,Bilicanas na sasa anayo project yake mwenyewe ya The Legends.

DJ JD hakuanza uDJ miaka ya 80 wala hajawahi kuwa kwenye kundi la kwa fujo DJs. Get your facts right.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom