Hisia za ukabila za shibuda juu ya chedema haziwakilishi mawazo ya wasukuma.

Wakuu.
Nimekutana na hoja za huyu bwana anaye onekana amekerwa na hisia za ukabila wa Shibuda juu ya chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) na ameamua kufunguka na kuweka msimamo wake kama jinsi anavyosomeka hapa chini. NImeona si vibaya nika washirikisha na nyinyi mumsome mawazo yake...

Nimesikitishwa na kukasirishwa sana na taarifa iliyo kwenye gazeti moja la leo juu madai ya Shibuda kwamba anasakamwa ndani ya Chadema kwa sababu yeye ni Msukuma. Kwanza sikuamini kama Shibuda (katika akili timamu) anaweza kutamka maneno ya namna hiyo. Pili siamini kama kweli maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma halisi kwa maana ya kabila, tabia, na mtazamo. Hata hivyo baada ya kutafakari kauli za nyuma za Mh. Shibuda tangu mwaka 2005 hadi alipohamia Chadema mwaka 2010, nimejiridhisha kuwa maneno yale kweli huenda yametamkwa na yeye. Pengine kitu kigumu kabisa kwangu ni kuishawishi akili yangu ikubaliane na wazo kwamba maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma akiwa hajalewa, hana kichaa (kwa kisukuma "lusalo") au ugonjwa mwingine wa akili. Nitafafanua.

Kwanza, kama inavyofahamika kwa wengi, Wasukuma ndiyo kabila kubwa kuliko yote hapa nchini. Jamii ya wasukuma imeenea sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa hasa Mwanza, Shinyanga na Tabora. Kwa tabia na aina ya shughuli zao za kiuchumi, wasukuma wamesambaa pia katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Katavi, Tanga, na Pwani. Takwimu za idadi ya watu katika sensa ya mwaka 2002 zinaonesha kuwa kulikuwa na Wasukuma karibia milioni 8 kati ya watanzania milioni 36 wa wakati huo. Kwa kutambua wingi wao hapa nchini, Wasukuma wamejijengea tabia ya kujiamini na kutotishwa na uwepo au mafanikio ya kabila jingine mahali popote.

Haijawahi kutokea Msukuma halisi akalalamika juu kuingiliwa na kabila jingine au kutishiwa na mafanikio ya kabila jingine. Wasukuma ni wapole, wavumilivu, wenye busara, na hawana wivu na mafanikio ya mtu au kabila jingine. Ndiyo maana hata katika ngazi mbalimbali za uongozi, watu wa makabila mengine ni rahisi sana kukubalika na na hata kupigiwa kura kuwa viongozi katika maeneo ya wasukuma bila kujali wanakotoka. Kwa ujumla, linapokja suala la kutohisi au kujali ukabila, wasukuma wamestaarbika muda mrefu sana pengine kuliko kabila jingine lolote hapa nchini. Wengine wanaona huo ni ujinga. Sisi wasukuma tulioenda shule vizuri na kuona yanayotokea kwingine duniani tunaita huu ni ustaarabu. Hili la ustaarabu wa wasukuma hata Shibuda mwenyewe analijua, na kwa bahati mbaya nalo limekuwa likimsumbua. Ndiyo maana napata taabu kuelewa aina ya wasukuma anaowawakilisha Shibuda katika baadhi ya matamshi yake.

Pili, kwa hulka halisi ya Kisukuma (hasa wale wa Mwanza; Shibuda ni Msukuma wa Shinyanga) si rahisi kumkuta baba mzima wa kisukuma akilialia kuonewa au kubaguliwa na mtu au kabila lolote. Wasukuma ni watu wa kujiamini. Wanajiona ni wengi, wenye nguvu, mali nyingi, na kama baba wa 'vikabila' vingine vyote hapa chini (situmii neno 'vikabila" kwa maana ya kudharau makabila mengine bali ni namna tu ya msemo wa kisukuma wenye kuonesha hali ya kutotishwa: kumbuka neno 'vijisenti'?). Ukisikia mwanaume mzima wa kisukuma analalamika; iwe kumlalamikia mtu mwingine au kundi au kabila jingine ujue huyo ni msukuma aliyechanganyikiwa au kushindwa maisha (kwa kisukuma "balemelwa").

Kwa asili na historia yao, wasukuma hawajawahi kulalamika kubaguliwa mahali popote na mtu yoyote nchini. Hata inapotokea kweli wakadhulumiwa, wakanyanyaswa, au kutumiwa (kama ilivyofanya CCM kwa zaidi ya mika 50) wasukuma huvumilia huku wakijipanga. Na muda unapofika huonesha msimamo wao kwa vitendo (rejea yaliyotokea Nyamagana na Ilemela uchaguzi 2010). Ni wasukuma wachache sana (wa aina ya Shibuda) wanaoweza kudekeza vijembe na vijimaneno vya ushwahilini kwa lengo la kutafuta huruma ya watu. Tangu lini kabila kubwa lenye uwezo, mali, na historia ya kujiamini kama wasukuma likaanza kupiga kelele ya kuonewa na watu wa makabila madogo? Hicho ni kilio cha Shibuda na tumbo lake na si kilio cha wasukuma.

Mwisho, nataka Mh Shibuda aweke wazi kuwa matatizo yake na Chadema si matatizo ya wasukuma na Chadema. Kama anahisi kubaguliwa na Chadema kwa sababu ya 'aina ya usukuma wake' basi atambue pia kuwa anabaguliwa hata na wasukuma wenzake ambao sasa wamejaa ndani ya Chadema. Na mimi nataka kusisitiza kuwa kama anafanya vurugu zote hizi kwa lengo la kuitisha Chadema au kuvuta hisia za wasukuma na huruma zao ili wampe urais kwa kigezo cha ukubwa wa kabila lake basi ajue ameaumia. Wasukuma hawako tayari kuwakilishwa na mtu wa aina ya Shibuda (labda wale wa jimboni kwake tu). Kuna wasukuma wengi wasomi, waelewa, wastaarabu, na wenye hekima mara elfu kumi ya Shibuda. Kwa ujumla, karata ya ukabila haichezeki uskumani. Hata kama itatokea waaamue kuicheza, hawatakuwa tayari kuunga mkono mtu wa kuwaharirisha mbele ya makabila mengine (madogo) nchini kama Shibuda. Ndani ya wasukuma kuna majembe ya ukweli yanayoweza kugombea urais na kufanikiwa lakini si jembe butu na lililochoka kama Shibuda.

Kama Msukuma mwenzake na mwelewa wa tabia na mtazamo wa kabila langu, namwomba kaka yangu Shibuda asizidi kutuaibisha na kututengenezea taswira tusiyokuwa nayo miongoni mwa watanzania. Asitulazimishe kukubaliana na hisia zake za kipuuzi zinazotokana na msukumo wa wake wa kimaslahi na kutafuta sifa za kijinga na pengine huruma ya wapiga kura wake atakaporudi kugombea tena kwa tiketi ya chama chake halisi yaani CCM. Na kama anataka kweli kutumia karata ya ukabila kulazimisha kugombea urais kupitia Chadema basi akaanzie jimboni kwakwe alikotokea ili tuone kama kweli anaweza kuwazidi akili wasukuma wote wa huko hata kuwafanya waingiwe na hisia potofu zisizotokana na hulka halisi za Kisukuma.

Imeandikwa na Ikwalal M. Ikwalala
Wa Mwanza.

shibuda ntombanva
 
Huo ni mtazamo wako na una haki zote kuamini hivyo ila nikukumbushe tu usidhani unajua kila kitu,jifunze kwa wengine pia la sivyo utabaki hapohapo.Huyu ni mtu wa pili (ktk viongozi wa chadema) anayehisi hivo,Chacha Wangwe alitangulia kusema au naye Mura amekosa sifa kama msukuma Shibuda!
Suala la ukabila na ukanda CHADEMA liko wazi na wameshindwa kulifanyia kazi.Kama chama chenye demokrasia, suala la mtu kutangaza nia sidhani kama lingekua agenda kiasi hicho, hio ni nia tu sio kwamba ishakua. Alishawahi kufanya hivyo CCM kabla ya 2010, sasa mnajuaje kama hatajitoa kabla ya mambo.
You are loosing track, u better stick to matatizo ya wananchi ILA assignment kwa chama chenu 'Ukabila na Ukanda muufanyie kazi'. Zito hamumuwezi kwa umakini wake ila mngeshamwondoa ila ni hazina kubwa msiichezee.
 
Shibuda ni mtu wa aina yake hata angetoka kabila dogo hakuna asiyejua huyu mzee ni mlaku.
 
Huo ni mtazamo wako na una haki zote kuamini hivyo ila nikukumbushe tu usidhani unajua kila kitu,jifunze kwa wengine pia la sivyo utabaki hapohapo.Huyu ni mtu wa pili (ktk viongozi wa chadema) anayehisi hivo,Chacha Wangwe alitangulia kusema au naye Mura amekosa sifa kama msukuma Shibuda!
Suala la ukabila na ukanda CHADEMA liko wazi na wameshindwa kulifanyia kazi.Kama chama chenye demokrasia, suala la mtu kutangaza nia sidhani kama lingekua agenda kiasi hicho

mkuu mpaka leo hujaelewa kwa nn watu wanampinga shibuda? Ukivua gamba utaelewa.
 
Ingekuwa Shibuda hayuko ndani ya CHADEMA huyo Ikwalala ndio angesema ni hisia. Mpaka sasa Shibuda kadhihirisha ukweli ambao wengi tuliopo nje ya CHADEMA tulikuwa tukiuhisi. Na Nassari alihitimisha.
 
Huo ni mtazamo wako na una haki zote kuamini hivyo ila nikukumbushe tu usidhani unajua kila kitu,jifunze kwa wengine pia la sivyo utabaki hapohapo.Huyu ni mtu wa pili (ktk viongozi wa chadema) anayehisi hivo,Chacha Wangwe alitangulia kusema au naye Mura amekosa sifa kama msukuma Shibuda!
Suala la ukabila na ukanda CHADEMA liko wazi na wameshindwa kulifanyia kazi.Kama chama chenye demokrasia, suala la mtu kutangaza nia sidhani kama lingekua agenda kiasi hicho, hio ni nia tu sio kwamba ishakua. Alishawahi kufanya hivyo CCM kabla ya 2010, sasa mnajuaje kama hatajitoa kabla ya mambo.
You are loosing track, u better stick to matatizo ya wananchi ILA assignment kwa chama chenu 'Ukabila na Ukanda muufanyie kazi'. Zito hamumuwezi kwa umakini wake ila mngeshamwondoa ila ni hazina kubwa msiichezee.

Naungana na wewe, kwanza mleta hoja anajifanya msemaji wa Wasukuma, anakosea mimi simtambui, bora ya Shibuda!
 
Hongera uongozi wa CDM taifa kwa jinsi mnavyoshughulikia jambo la Shibuda, mpo juu mnatisha. Mpaka atapike nyongo ndoo apewe pole
 
Ni kweli wasukuma ni watu wa kujiamini na sio watu wa kuombaomba kuhurumiwa.Pia ni watu wavumilivu hata wakiwa wananyanyaswa au kuonewa lakini ni wenye msimamo,na huwa wanauonyesha muda muafaka unapopatikana.Rejea mkoa wa shinyanga ndio wenye wabunge wengi wa upinzani(CHADEMA) kuliko mkoa wowote nchini.Ni wachapa kazi hodari na sio watu wa kuombaomba misaada kama ilivyo kwa baadhi ya mikoa.Kuna baadhi ya mikoa watu wanadai hadi kujengewa nyumba pindi wanapopata tatizo dogo tu.Kwa wasukuma sio hivyo.Wasukuma ndio watu wa kwanza kukubali mageuzi pale walipochagua upinzani huko Bariadi mwaka 1994 na hivyo UDP kugawana viti 13-13 vya udiwani.MHWALA NG'WABEJA PYE ABOSE
 
Wakuu.
Nimekutana na hoja za huyu bwana anaye onekana amekerwa na hisia za ukabila wa Shibuda juu ya chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) na ameamua kufunguka na kuweka msimamo wake kama jinsi anavyosomeka hapa chini. NImeona si vibaya nika washirikisha na nyinyi mumsome mawazo yake...

Nimesikitishwa na kukasirishwa sana na taarifa iliyo kwenye gazeti moja la leo juu madai ya Shibuda kwamba anasakamwa ndani ya Chadema kwa sababu yeye ni Msukuma. Kwanza sikuamini kama Shibuda (katika akili timamu) anaweza kutamka maneno ya namna hiyo. Pili siamini kama kweli maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma halisi kwa maana ya kabila, tabia, na mtazamo. Hata hivyo baada ya kutafakari kauli za nyuma za Mh. Shibuda tangu mwaka 2005 hadi alipohamia Chadema mwaka 2010, nimejiridhisha kuwa maneno yale kweli huenda yametamkwa na yeye. Pengine kitu kigumu kabisa kwangu ni kuishawishi akili yangu ikubaliane na wazo kwamba maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma akiwa hajalewa, hana kichaa (kwa kisukuma "lusalo") au ugonjwa mwingine wa akili. Nitafafanua.

Kwanza, kama inavyofahamika kwa wengi, Wasukuma ndiyo kabila kubwa kuliko yote hapa nchini. Jamii ya wasukuma imeenea sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa hasa Mwanza, Shinyanga na Tabora. Kwa tabia na aina ya shughuli zao za kiuchumi, wasukuma wamesambaa pia katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Katavi, Tanga, na Pwani. Takwimu za idadi ya watu katika sensa ya mwaka 2002 zinaonesha kuwa kulikuwa na Wasukuma karibia milioni 8 kati ya watanzania milioni 36 wa wakati huo. Kwa kutambua wingi wao hapa nchini, Wasukuma wamejijengea tabia ya kujiamini na kutotishwa na uwepo au mafanikio ya kabila jingine mahali popote.

Haijawahi kutokea Msukuma halisi akalalamika juu kuingiliwa na kabila jingine au kutishiwa na mafanikio ya kabila jingine. Wasukuma ni wapole, wavumilivu, wenye busara, na hawana wivu na mafanikio ya mtu au kabila jingine. Ndiyo maana hata katika ngazi mbalimbali za uongozi, watu wa makabila mengine ni rahisi sana kukubalika na na hata kupigiwa kura kuwa viongozi katika maeneo ya wasukuma bila kujali wanakotoka. Kwa ujumla, linapokja suala la kutohisi au kujali ukabila, wasukuma wamestaarbika muda mrefu sana pengine kuliko kabila jingine lolote hapa nchini. Wengine wanaona huo ni ujinga. Sisi wasukuma tulioenda shule vizuri na kuona yanayotokea kwingine duniani tunaita huu ni ustaarabu. Hili la ustaarabu wa wasukuma hata Shibuda mwenyewe analijua, na kwa bahati mbaya nalo limekuwa likimsumbua. Ndiyo maana napata taabu kuelewa aina ya wasukuma anaowawakilisha Shibuda katika baadhi ya matamshi yake.

Pili, kwa hulka halisi ya Kisukuma (hasa wale wa Mwanza; Shibuda ni Msukuma wa Shinyanga) si rahisi kumkuta baba mzima wa kisukuma akilialia kuonewa au kubaguliwa na mtu au kabila lolote. Wasukuma ni watu wa kujiamini. Wanajiona ni wengi, wenye nguvu, mali nyingi, na kama baba wa 'vikabila' vingine vyote hapa chini (situmii neno 'vikabila" kwa maana ya kudharau makabila mengine bali ni namna tu ya msemo wa kisukuma wenye kuonesha hali ya kutotishwa: kumbuka neno 'vijisenti'?). Ukisikia mwanaume mzima wa kisukuma analalamika; iwe kumlalamikia mtu mwingine au kundi au kabila jingine ujue huyo ni msukuma aliyechanganyikiwa au kushindwa maisha (kwa kisukuma "balemelwa").

Kwa asili na historia yao, wasukuma hawajawahi kulalamika kubaguliwa mahali popote na mtu yoyote nchini. Hata inapotokea kweli wakadhulumiwa, wakanyanyaswa, au kutumiwa (kama ilivyofanya CCM kwa zaidi ya mika 50) wasukuma huvumilia huku wakijipanga. Na muda unapofika huonesha msimamo wao kwa vitendo (rejea yaliyotokea Nyamagana na Ilemela uchaguzi 2010). Ni wasukuma wachache sana (wa aina ya Shibuda) wanaoweza kudekeza vijembe na vijimaneno vya ushwahilini kwa lengo la kutafuta huruma ya watu. Tangu lini kabila kubwa lenye uwezo, mali, na historia ya kujiamini kama wasukuma likaanza kupiga kelele ya kuonewa na watu wa makabila madogo? Hicho ni kilio cha Shibuda na tumbo lake na si kilio cha wasukuma.

Mwisho, nataka Mh Shibuda aweke wazi kuwa matatizo yake na Chadema si matatizo ya wasukuma na Chadema. Kama anahisi kubaguliwa na Chadema kwa sababu ya 'aina ya usukuma wake' basi atambue pia kuwa anabaguliwa hata na wasukuma wenzake ambao sasa wamejaa ndani ya Chadema. Na mimi nataka kusisitiza kuwa kama anafanya vurugu zote hizi kwa lengo la kuitisha Chadema au kuvuta hisia za wasukuma na huruma zao ili wampe urais kwa kigezo cha ukubwa wa kabila lake basi ajue ameaumia. Wasukuma hawako tayari kuwakilishwa na mtu wa aina ya Shibuda (labda wale wa jimboni kwake tu). Kuna wasukuma wengi wasomi, waelewa, wastaarabu, na wenye hekima mara elfu kumi ya Shibuda. Kwa ujumla, karata ya ukabila haichezeki uskumani. Hata kama itatokea waaamue kuicheza, hawatakuwa tayari kuunga mkono mtu wa kuwaharirisha mbele ya makabila mengine (madogo) nchini kama Shibuda. Ndani ya wasukuma kuna majembe ya ukweli yanayoweza kugombea urais na kufanikiwa lakini si jembe butu na lililochoka kama e.

Kama Msukuma mwenzake na mwelewa wa tabia na mtazamo wa kabila langu, namwomba kaka yangu Shibuda asizidi kutuaibisha na kututengenezea taswira tusiyokuwa nayo miongoni mwa watanzania. Asitulazimishe kukubaliana na hisia zake za kipuuzi zinazotokana na msukumo wa wake wa kimaslahi na kutafuta sifa za kijinga na pengine huruma ya wapiga kura wake atakaporudi kugombea tena kwa tiketi ya chama chake halisi yaani CCM. Na kama anataka kweli kutumia karata ya ukabila kulazimisha kugombea urais kupitia Chadema basi akaanzie jimboni kwakwe alikotokea ili tuone kama kweli anaweza kuwazidi akili wasukuma wote wa huko hata kuwafanya waingiwe na hisia potofu zisizotokana na hulka halisi za Kisukuma.

Imeandikwa na Ikwalal M. Ikwalala
Wa Mwanza.

Hapa umehalibu mada yote, unataka kutuambia kama sisi tuliomchagua ni tofauti na wasukuma unaowaongelea!!!Haya ni matusi ya rejareja. Na kama ndivyo, basi ungeongelea tu wasukuma wa sehemu yako. Please, Don't include all sukuma if you think we are different from you. Demokrasia inakuruhusu kupingana na kauli zake, lakini jamii ya wana Maswa waliompigia kura haitoruhusu kuitwa hivyo unavyoiita.
Nafikili mada yako imetawaliwa zaidi na hisia za kisiasa badala ya ukweli wa mila na desturi za Kisukuma na mambo yalivyo ndani ya CDM.
Mtu makini ni yule anayetafuta ukweli kabla ya kuongea, na Kama wewe ni msukuma halisi, nafikili ungekuwa na busara kwa yale uliyoyandika kwa kutafuta ukweli badala ya kutawaliwa na munkali.
 
Kwa hili Shibuda amejichanganya na unafiki wake! Wasukuma wala hilo la ukabila analolisimamia halina nafasi! wanaomtumia wanadhani anaweza kuwashawishi wasukuma kirahisi kwa hoja legevu kama hiyo!!! kwa nguvu zote tunasema; i-CCM ubise abasukuma twilema kwingila ng'waka 2010!. Bravo CHADEMA, kwa kazi nzuri ya kulikomboa taifa.
 
Wakuu.
Nimekutana na hoja za huyu bwana anaye onekana amekerwa na hisia za ukabila wa Shibuda juu ya chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) na ameamua kufunguka na kuweka msimamo wake kama jinsi anavyosomeka hapa chini. NImeona si vibaya nika washirikisha na nyinyi mumsome mawazo yake...

Nimesikitishwa na kukasirishwa sana na taarifa iliyo kwenye gazeti moja la leo juu madai ya Shibuda kwamba anasakamwa ndani ya Chadema kwa sababu yeye ni Msukuma. Kwanza sikuamini kama Shibuda (katika akili timamu) anaweza kutamka maneno ya namna hiyo. Pili siamini kama kweli maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma halisi kwa maana ya kabila, tabia, na mtazamo. Hata hivyo baada ya kutafakari kauli za nyuma za Mh. Shibuda tangu mwaka 2005 hadi alipohamia Chadema mwaka 2010, nimejiridhisha kuwa maneno yale kweli huenda yametamkwa na yeye. Pengine kitu kigumu kabisa kwangu ni kuishawishi akili yangu ikubaliane na wazo kwamba maneno hayo yanaweza kutamkwa na Msukuma akiwa hajalewa, hana kichaa (kwa kisukuma "lusalo") au ugonjwa mwingine wa akili. Nitafafanua.

Kwanza, kama inavyofahamika kwa wengi, Wasukuma ndiyo kabila kubwa kuliko yote hapa nchini. Jamii ya wasukuma imeenea sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa hasa Mwanza, Shinyanga na Tabora. Kwa tabia na aina ya shughuli zao za kiuchumi, wasukuma wamesambaa pia katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Katavi, Tanga, na Pwani. Takwimu za idadi ya watu katika sensa ya mwaka 2002 zinaonesha kuwa kulikuwa na Wasukuma karibia milioni 8 kati ya watanzania milioni 36 wa wakati huo. Kwa kutambua wingi wao hapa nchini, Wasukuma wamejijengea tabia ya kujiamini na kutotishwa na uwepo au mafanikio ya kabila jingine mahali popote.

Haijawahi kutokea Msukuma halisi akalalamika juu kuingiliwa na kabila jingine au kutishiwa na mafanikio ya kabila jingine. Wasukuma ni wapole, wavumilivu, wenye busara, na hawana wivu na mafanikio ya mtu au kabila jingine. Ndiyo maana hata katika ngazi mbalimbali za uongozi, watu wa makabila mengine ni rahisi sana kukubalika na na hata kupigiwa kura kuwa viongozi katika maeneo ya wasukuma bila kujali wanakotoka. Kwa ujumla, linapokja suala la kutohisi au kujali ukabila, wasukuma wamestaarbika muda mrefu sana pengine kuliko kabila jingine lolote hapa nchini. Wengine wanaona huo ni ujinga. Sisi wasukuma tulioenda shule vizuri na kuona yanayotokea kwingine duniani tunaita huu ni ustaarabu. Hili la ustaarabu wa wasukuma hata Shibuda mwenyewe analijua, na kwa bahati mbaya nalo limekuwa likimsumbua. Ndiyo maana napata taabu kuelewa aina ya wasukuma anaowawakilisha Shibuda katika baadhi ya matamshi yake.

Pili, kwa hulka halisi ya Kisukuma (hasa wale wa Mwanza; Shibuda ni Msukuma wa Shinyanga) si rahisi kumkuta baba mzima wa kisukuma akilialia kuonewa au kubaguliwa na mtu au kabila lolote. Wasukuma ni watu wa kujiamini. Wanajiona ni wengi, wenye nguvu, mali nyingi, na kama baba wa 'vikabila' vingine vyote hapa chini (situmii neno 'vikabila" kwa maana ya kudharau makabila mengine bali ni namna tu ya msemo wa kisukuma wenye kuonesha hali ya kutotishwa: kumbuka neno 'vijisenti'?). Ukisikia mwanaume mzima wa kisukuma analalamika; iwe kumlalamikia mtu mwingine au kundi au kabila jingine ujue huyo ni msukuma aliyechanganyikiwa au kushindwa maisha (kwa kisukuma "balemelwa").

Kwa asili na historia yao, wasukuma hawajawahi kulalamika kubaguliwa mahali popote na mtu yoyote nchini. Hata inapotokea kweli wakadhulumiwa, wakanyanyaswa, au kutumiwa (kama ilivyofanya CCM kwa zaidi ya mika 50) wasukuma huvumilia huku wakijipanga. Na muda unapofika huonesha msimamo wao kwa vitendo (rejea yaliyotokea Nyamagana na Ilemela uchaguzi 2010). Ni wasukuma wachache sana (wa aina ya Shibuda) wanaoweza kudekeza vijembe na vijimaneno vya ushwahilini kwa lengo la kutafuta huruma ya watu. Tangu lini kabila kubwa lenye uwezo, mali, na historia ya kujiamini kama wasukuma likaanza kupiga kelele ya kuonewa na watu wa makabila madogo? Hicho ni kilio cha Shibuda na tumbo lake na si kilio cha wasukuma.

Mwisho, nataka Mh Shibuda aweke wazi kuwa matatizo yake na Chadema si matatizo ya wasukuma na Chadema. Kama anahisi kubaguliwa na Chadema kwa sababu ya 'aina ya usukuma wake' basi atambue pia kuwa anabaguliwa hata na wasukuma wenzake ambao sasa wamejaa ndani ya Chadema. Na mimi nataka kusisitiza kuwa kama anafanya vurugu zote hizi kwa lengo la kuitisha Chadema au kuvuta hisia za wasukuma na huruma zao ili wampe urais kwa kigezo cha ukubwa wa kabila lake basi ajue ameaumia. Wasukuma hawako tayari kuwakilishwa na mtu wa aina ya Shibuda (labda wale wa jimboni kwake tu). Kuna wasukuma wengi wasomi, waelewa, wastaarabu, na wenye hekima mara elfu kumi ya Shibuda. Kwa ujumla, karata ya ukabila haichezeki uskumani. Obheja sana Ng'wanangwa.Aise bhasuguma bha Mbeya tuitogilwe sana eCHADEMA ise.Tutahaile gete ukwenhelwa bhanu bhasaji ne ccm guti J.Shibhuda
 
Shibuda aachwe aendelee na siasa zake hatimaye atapoa tu kwani aina ya siasa yake si ya kizazi au wakati huu.Hatuhitaji nahau au misemo tunahitaji mtu mwenye sera za kumkomboa mtanzania toka hapa alipo kuelekea kwenye mafanikio,hili sio saizi ya Shibuda.
 
Back
Top Bottom