Hisia na hamasa za Maandamano nchini: Mapokeo, Mitazamo na Uhalisia (Viongozi na Wananchi)

Mimi ni mwana CCM Damu. Nilimchagua Rais Magufuli na pia ni kiongozi mkubwa tu ndani ya Chama. Ila, lazima nitashiriki maadamano ya Amani kwa sababu zifuatazo.

1. Hali ya uchumi imefikia Pabaya. Mimi nina Restaurant, maize yameshuka kutoka laki 6 kwa siku, hadi laki moja au hata elfu sabini
2. Wadogo zangu wawili wamemaliza chuo, mwaka wa pili sasa hawana kazi
3. Kodi zisizo na kichwa wala miguu. Yaani kodi hazitamaniki, ni kubwa mno.
4. Hali ya usalama imekuwa mbaya, watu wanatishwa, wanatekwa, na hata kuuwawa. Rafiki yangu ndani ya Chama juri katishwa kuuwawa kwa sababu alihoji Bashite anapata wapi madaraka ya kuwabugdhi watumishi
5. Polisi wamekuwa adui wa raia, kuanzia traffic police hadi polisi wa kawaida. Wanawatesa wananchi bila sababu za msingi
6. Sababu kubwa zaidi, ni nafsi zetu kutawaliwa. Tunalazimishwa kuishi kama wanyama, tunalaimishwa kufuata "CCM NI PORI LA WAJINGA"
kuna kila dalili kuwa 95% ya wanaccm wameathiriwa na matatizo ya uchawi, ujinga, upumbavu. na huenda Wote ni majizi. kwa wale wanaccm waliofika walau form ii wamesomea umuhimu wa multipartism ndani ya nchi kwamba ndio kioo cha serikali yaani ndio mbadala wa serikali yo yote duniani. nchi za ujerumani na uingereza tunasikia vyama vinaungana kuunda serikali, hii imekwishafanyika kenya, zanzibar na kwingineko lakini cha kushangaza kwa akina Mungu magufuli tunaona wapinzani wamekuwa wahaini hawaruhusiwi kuikosoa serikali.
ujinga ni pale ccm inapodhani kuwa nchi ni ya kwao hawajui wao ni wahuni tu na wauaji fulani tu na mkataba wao pia umeisha ni muda ambao nao watajutia mambo hayo waliyoyafanya.
kama watu wana PhD wakati uelewa ni wa CHEKECHEA inamaanisha wana mawazo mgando kama vima.
there are men and women in chadema BUT boys and girls are found in ccm .
for our brothers and sisters you shed their innocent bloods, TIME WILL TELL
R.I.P akwilini,john, .., ..., ..., ...,
Amin bila kuhoji.
 
Mimi ni mwana CCM Damu. Nilimchagua Rais Magufuli na pia ni kiongozi mkubwa tu ndani ya Chama. Ila, lazima nitashiriki maadamano ya Amani kwa sababu zifuatazo.

1. Hali ya uchumi imefikia Pabaya. Mimi nina Restaurant, maize yameshuka kutoka laki 6 kwa siku, hadi laki moja au hata elfu sabini
2. Wadogo zangu wawili wamemaliza chuo, mwaka wa pili sasa hawana kazi
3. Kodi zisizo na kichwa wala miguu. Yaani kodi hazitamaniki, ni kubwa mno.
4. Hali ya usalama imekuwa mbaya, watu wanatishwa, wanatekwa, na hata kuuwawa. Rafiki yangu ndani ya Chama juri katishwa kuuwawa kwa sababu alihoji Bashite anapata wapi madaraka ya kuwabugdhi watumishi
5. Polisi wamekuwa adui wa raia, kuanzia traffic police hadi polisi wa kawaida. Wanawatesa wananchi bila sababu za msingi
6. Sababu kubwa zaidi, ni nafsi zetu kutawaliwa. Tunalazimishwa kuishi kama wanyama, tunalaimishwa kufuata mkumbo bila kuhoji. Tunauwawa hovo hovyo, tunatekwa. Hadi lini?

Uoga basi, tutaandamana kwa Amani. Polisi hatuwaogopi tena, kufa ni mara moja. Maisha bora ya mwanangu ya bade ni bora kuliko mates ya sasa hivi

Hoja zako hazina mashiko. Hivi mauzo yako kushuka utaisingizia serikali kweli? hebu waone wataalamu wa biashara watakushauri kubadilisha strategies za biashara kwa kipindi kama hiki ambapo serikali inabana matumizi. Kuhusu ajira kwa wadogo zako pia sidhani kama ni ishu ya kuiblame serikali direct. Nenda popote duniani kwa ulimwengu huu, utakutana na hiyo changamoto ya ajira. Dunia imehamia kwenye machine saivi by any means ajira zitaendelea kupungua na kupungua. Na huenda hata ikiitishwa interview hawatafaulu kwa kukosa vigezo. Tafakari mzee. Serikali inaweza ikakuuzi kwa mambo fulani lakini tusiishambulie kwa vitu ambavyo sisi wenyewe tunavitengeneza.
 
Nisiku ambayo anga liligeuka ghafla na kuwa jekundu.

Mingurumo ilitamaraki kila eneo.

Siku ambayo mzee Mashati wa Gongo Lamboto alikimbia mpaka Mbezi ya Kimara.

Siku ambayo watu waliwatelekeza watoto wao na kubeba mbwa nakukimbia.

Naam siku hatari sana ya milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto.

Sijui mwenzangu ulikuwa wapi siku hiyo.
 
sioni uhusiano kati ya mabomu ya gongo la mboto na maandamano bila shaka mleta mada hauna akili kabisa
 
Kumekuwa na hamasa hamasa ya maandamano kwa kupitia Mitandao ya Kijamii, haswa kupitia Instagram na Telegram. Hamasa hii imeamsha hisia za kila aina kwa wale ambao wanafuatilia kwa karibu.

Hamasa hii imezaa makundi matatu:

Kundi la kwanza: Wale wanaoamini haya maandamano yana tija na yatafanikiwa.

Kundi la pili:
Wale wanaoamini maandamano haya yana tija ila hayatafanikiwa.

Kundi la tatu:
Wale ambao wanaamini haya maandamano hayana tija na wala hayatafanikiwa.​

Kwa wale wasiojua, taarifa za awali za kutaka kufanywa maandamano ni Bi. Mange Kimambi ambaye baada ya kumshambulia kwa posts kadhaa Rais Magufuli kupitia mtandao wa Instagram, aliamua kuwa sasa inatakiwa kuandamana akidai kuwa Upinzani nchini Tanzania hauna nguvu wala mipango thabiti inayoeleweka kuweza kuutoa au kuushinda uongozi uliopo aidha kwa haki (uchaguzi) au kwa kupindua.

Bado ni mapema sana kuzungumzia nini kinatarajiwa kutokea hapa karibuni, ikiwa bado ni Mwezi na nusu toka sasa hadi tarehe iliyopangwa maandamano hayo.

La msingi kuliko yote ni kwamba ni wazi Serikali imeyasikia na tumesikia viongozi mbali mbali wakitoa matamko au kuzungumzia juu ya hamasa hizo za maandamano. Mrejesho huo wa viongozo mbali mbali ikiwemo na rais wa nchi, inafanya kuibuka kwa mijala kwa upana zaidi kama vile, kukuzwa kwa maandamano haya, kukuzwa kwa jina la Mange Kimbambi na kumfanya awe relevant zaidi, kutopokelewa na kutenda sahihi tokana na hamasa hizo, na masuala mengine kede kede.

Kwa wale ambao hawajabahatika kusikia baadhi ya kauli za viongozi unaweza soma hapa chini:-

CP Nsato Marijani (Mkuu wa Operation na mafunzo):

Kuna kikundi ambacho kimetumia mtandao wa Telegram kuhamasisha maandamano nchi nzima kinyume cha sheria na kutaka kwenda ikulu na kufanya hayo wanayotaka kufanya. Naomba nirudie kusema kwamba lolote linalotaka kufanyika katika nchi hii, sisi kama jesi la Polisi tunawaasa wananchi walifanye kwa mjibu wa sheria. Swala la kufanya maandamano ukiwa na nia ya kuiondoa serikali ni uhaini. Hatua kali zitachukuliwadhidi ya watu watakaovunja sheria na tusije kulaumiwa kwa lolote

Rais John Pombe Magufuli:

"Wapo watu wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuwe barabarani tunaandamana, watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamana kule nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wanawatuma basi watakwenda kuwasilimulia vizuri, niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani na tunataka tujenge uchumi wa kweli ili Watanzania watajirike na hali ya Watanzania imeanza kwenda vizuri mwanzo ni mgumu lakini nataka niwaambie watanzania tupo kwenye wakati mzuri tuvumiliane ili tufike sehemu Tanzania iwe nchi ya asali"

Msome Rais Magufuli: Rais Magufuli: Ole wake atakayeandamana, kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri

Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar):

"Kuna kakundi hapa kanahangaika kweli usiku na mchana wengine wanahangaika kutumia mitandao ya kijamii kutukana viongozi, kuhamasisha sijui wanaita nini sijui maandamano nawapa pole sana, watafanya labda mimi nikiondoka nikiwa siyo Mkuu wa Mkoa kwenye huu Mkoa hiyo mipango mipango yao watafanya labda mimi nikiwa sipo lakini amani ya mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana"

IGP Simon Sirro (Mkuu wa Jeshi la Polisi):

"Wote tunajua kwamba maandamano Katiba imetamka na sheria za vyama vya siasa imetamka kwamba maandamano ni haki kwa raia lakini kuna utaratibu wa maandamano, sasa kuna maandamano ambayo ni halali na ambayo si halali. Maandamano ambayo si halali maanake yanaashilia uvunjifu wa amani ni maandamano ambayo yanaelekea kutenda uhalifu sasa kama ni maandamano yanakuja kwa njia ya uhalifu na jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kuzuia uhalifu maanake ni lazima tuhakikishe maandamano hayo hayafanyiki hivyo ni lazima juhudi ifanyike kabla ya hayo maandamano kufanyika"

Zaidi IGP anasema....

"Maandamano yakifanyika ambayo si halali uwezo wa kuudhibiti tunao sasa natoa tu salamu kwa wale ambao wanafikiri wataweza kufanya maandamano ambayo si halali ya kutaka kuleta vurugu ndani ya nchi ambao ni watu wachache wenye maanake ni lazima watapamba na jeshi la polisi ambalo linasimamia usalama wa nchi hii, lakini niwambie na wale vijana wadogo na wazazi, wazazi wajitahidi sana kulea watoto zao wajaribu kuwaambia watoto zao wasiingie kwenye kuvunja sheria kwani unaweza kuvunja sheria kirahisi ila madhara yake ni makubwa. Unaweza kuingia kwenye maandamano ambayo si ya halali halafu ukileta shida kubwa kwako na familia yako. Wanacheza na hiyo mitandao sijui tumefika mia moja, mia mbili siju elfu moja wajaze wanachosema lakini nasema nafasi hiyo hawataipata"

Msome zaidi IGP Sirro: IGP Sirro: Ole wake atakayeandamana bila kufuata sheria

Kamanda Lazaro Mambosasa:

"Kuna watu ambao wanaendelea kuhamasisha wananchi kuvunja sheria. Wanataka wajiandae kwa maandamano, tarehe wanazoendelea kutaja. lakini wanafanya hivyo wao wakiwa wamekaa sehemu salama. Wanataka kuwaingiza watanzania wengine kwenye shida,"

Msome Mambosasa: Polisi yawakamata wawili kwa mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA. Kamanda Mambosasa akataza maandamano ya mitandaoni

Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo naye akasema: Jenerali Mabeyo(JWTZ): Kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi. Hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo

Uhalisia wa Hamasa hizi za Maandamano:

Kila mmoja ana lake la kusema, lile analoliamini na wengi wanakuwa wanasimamia mawazo yao hayo kwa vigezo mbalimbali....

Naomba kufahamu toka kwenu wana JamiiForums, ni nini uhalisia (tokana na mtazamo wenu) juu ya hamasa hii ya maandamano na namna inavyochukuliwa na viongozi wa juu pamoja na wananchi huko mitaani?

Maoni ya wananchi (Kwa hisani ya Kwanza TV)



Nawasilisha!


Mimi mtazamo wangu ni huu:

1. Kuna kila dalili kuwa wengi wa viongozi wetu hawa ni waoga, hawajiamini na wana tatizo kubwa zaidi la UPUNGUFU WA MAARIFA

Kumbuka kuwa, ukikosa maarifa basi BUSARA na HEKIMA huyeyuka pia na mwisho utaishia kwenye MAAMUZI yasiyo sahihi ya aidha ktk kuzungumza kwako (kutumia mdomo wako) ama ktk kutenda kwako.

Miongoni mwa viongozi wote hawa kwa kuzipima kauli zao juu ya jambo hili, ingalau IGP kidogo busara na hekima hazikumponyoka japo naye mwishoni kabisa kamaliza vibaya. Wengine wote ni zero !!

2. Nimesema ktk No. 1 hapo juu kuwa, at least IGP kidogo alikuwa na ufahamu kidogo wakati akisemea kuhusu hili jambo.

Kwanza ieleweke kabisa kuwa hamasa ya maandamano haya iko ktk kusudio la maneno (intention) tu. Haijawa halisi kwa mujibu wa sheria kama alivyosema IGP..

Cha kufurahisha kidogo ni kuwa, kumbe IGP anatambua kuwa maandamano ni haki ya kisheria na kikatiba ya watu iwapo wana sababu za kuandamana...

Na zaidi sana, kumbe Mkuu wa Mapolisi (IGP) anajua kuwa zipo taratibu za kundi la watu wanaotaka kuandamana za kufuata ili shughuli ya kuandamana iwe hali...

Nilidhani kuwa, angeshauri wanaokusudia kuandamana awaambie kuwa wafuate uliowekwa na sheria zetu. Lakini kinyume chake tunaona kung'aka kwingi blindly kwa kisingizio cha kulinda amani...!!

Hizi kwangu mimi ndiyo hasa dalili za woga na kutojiamini kwa viongozi wetu. Haijulikani sawia kiini cha hofu zao ni nini haswa...

Lakini mtu anaweza kusema kuwa labda kiini chaweza kuwa namna walivyoyapata madaraka na mamlaka waliyonayo pamoja na matendo yao wakiwa madarakani.

Kwa sababu, "maandamano" maana yake ni mkusanyiko wa watu wanaotembea kwa pamoja na mwisho huishia kukusanyika eneo fulani aghalabu kwenye eneo la uwazi (kiwanjani nk) na viongozi wao wa maandamano hayo hutoa hotuba ku address kile ambacho they are protesting about....

Nadhani, hofu ya watawala ipo hapa. Kuogopa kukosolewa mbele ya umma unaomulikwa makamera ya TV, na vipaza sauti vikubwa kwa uwazi namna ile hata matendo yao yasiyofaa kuwekwa wazi...!!

Hiki ndicho kilichowapeleka kina Freeman Mbowe na wenzake mahabusu na Leo wako mahakamani !!
 
siku si nyingi mambo yatakua bayana, dalili zote za kuonyesha mabadiliko yanakuja zipo wazi

ni saa tu watanzania watajiongoza kwa uhuru wa kweli
 
Tangu wiki hii ianze naona kuna juhudi za Makusudi kabisa zinafanywa kuihusisha CHADEMA na maandamano yanayohamasishwa mitandaoni na mwana dada Mange Kimambi aliyeko Marekani kwa sasa.

Lakini Mange wakati anaondoka Tanzania alikuwa ni Mwana CCM na wala hajawahi kusema kwamba amejiunga CHADEMA. Mange kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa mitizamo yake mwenyewe alimpinga sana Mgombea Urais kupitia CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa.

Kama leo Mange Kimambi anaipinga serikali iliyoko madarakani na Rais Magufuli haitokani na yeye kuwa CHADEMA bali kwa mtazamo wangu inatokana na mtizamo wake binafsi kama aliokuwa nao dhidi ya Lowassa wakati wa Kampeni za Mwaka 2015.

Inawezekana kabisa kwamba kuna wana CHADEMA baadhi wanaunga mkono harakati za Mange Kimambi, lakini haibadilishi kwamba Mange ni Mwana CCM. Ni mjinga sana anayekaribia ujuha anayeweza kuamini hakuna viongozi wa CCM wanaounga mkono harakati za Mange.

Mange anaishi Marekani inakuwaje anapata habari za ndani kabisa za chama chake na Serikali kama hapewi na viongozi wa CCM wanaomsaidia Rais Magufuli kuongoza nchi? Kwa ivo ni kwamba CCM inajitafuna yenyewe ndani kwa ndani lakini inataka kuitoa Kafara CHADEMA kwa kusingizia kwamba ndiyo inayohusika.

Mange mara kadhaa kasema kwamba yeye anawakilisha maslahi mapana ya watanzania na siyo maslahi ya vyama vya siasa vilivyoko Tanzania. Kwa nini CCM inataka kumfanya mwanachama wao kuwa ni wa CHADEMA?
 
Heri ya Pasaka wana JF.
Nikiwa kama Mtanzania mzalendo ninayeipenda Tanzania napenda nitoe ushauri wangu kwa vijana na wazee wa kitanzania kuhusu maandamano ya wananchi ya tar 26 mwezi huu.

Nimezunguka mikoa mitatu ndani ya mwezi wa tatu Mbeya, Dar es salaam na Mwanza, muamko wa wananchi kuhusu maandamano hayo ni wa kiasi cha wastani.Yaani siyo mbaya wala mzuri sana.Nilichojifunza ni kuwa akitokea kichaa mmoja akaongoza watu kuingia barabarani hakuna mtu ataweza zuia maandamano hayo,lakini pia asipotokea mtu wa kuyapeleka maandamano barabarani basi hayatakuwepo.
Kwa uhalisia huo wa muamko wa maandamano nitoe ushauri kwa vijana hasa kuhusu suals la kwanza.YAANI MAANDAMANO YAKIINGIA BARABARANI YAKITOKA HUMU MTANDAONI.

1.Waandamanaji wanadai Tanzania iliyo bora hivyo basi siku ya maandamano TUSIHARIBU,KUVUNJA,KUCHOMA WALA KUIBA MALI YA MTU YOYOTE AWE MGENI AU MTANZANIA.Tusiharibu mali yotote ya serikali wala ya umma maana vyote ni mali yetu.Maandamano haya ni dhidi ya serikali dharimu na siyo dhidi ya nchi yetu pendwa Tanzania.

2.Polisi na jeshi kwa ujumla ni walinzi wa taifa letu na mali zetu.Tumewapa dhamana hiyo sababu wote tusingeweza kuwa polisi.TUSIWACHOKOZE WALA KUPIGA POLISI SIKU YA MAANDAMANO maana watakuwa kutimiza wajibu wao wa kulinda taifa na wananchi wake.UNLESS TUKIWAONA POLISI HAO WANALINDA WATAWALA NA CHAMA CHA MAPINDUZI SIKU HIYO BADALA YA KULINDA RAIA NA TAIFA LAO BASI TUWAJIBU KWA KIASI CHA NGUVU WATACHOTUMIA.

3.Maandamano haya siyo dhidi ya Tanzania wala watanzania wenzetu,bali ni dhidi ya viongozi wanaotaka kuiharibu Tanzania,siku hiyo tukumbuke kuwa TUNAANDAMANA KUILINDA TANZANIA DHIDI YA WATU WACHACHE WANAOTAKA KUIHARIBU.HIVYO TUWE NA DHAMIRA YA KUILINDA TANZANIA DHIDI YA MTU YOYOTE YULE AWE POLISI,MGAMBO,MWANA JESHI AU NANI.

4.La mwisho ni ushauri KWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA. Jeshi linaitwa jeshi la wananchi wa Tanzania,siyo jeshi la serikali ya Tanzania hivyo jukumu la jeshi ni kulinda wananchi dhidi ya adui, awe rais awe polisi awe adui kutoka nje au ndani ya nchi,JESHI LIJIKITE KULINDA RAIA SIKU YA MAANDAMANO NA SIYO KULINDA WATAWALA AU CHAMA.
Jeshi la polisi lina kazi ya kulinda raia na mali zao,siku ya maandamano lisiwekeze nguvu yake kuua na kupiga raia utakuwa ndo mwisho wa Tanzania tuliyoizoea.TULINDE RAIA.

MKIONA RAIA WAMEINGIA BARABARANI MJUE WAMEIKATAA SERIKALI.WATANZANIA WOTE HAWAWEZI KUWA VIBARAKA WA MABEPARI AU WAPIGA DILI KAMA VIJANA WAPAMBE WA WATAWALA WANAVYOIAMINISHA JAMII KUWA KILA ANAYEIPINGA NA KUIKOSOA SERIKALI NI MPIGA DILI AU KIBARAKA WA MABEPARI.
WANANCHI WAKIINGIA BARABARANI MJUE VIONGOZI WANAOWAONGOZA HAWAJAFIKIA MALENGO WANANCH WALIYOYATAMANI...HIVYO BASI POLISI JESHI NA USALAMA WA TAIFA KAZI YENU IWE KULINDA RAIA SIYO WATAWALA.

Mwisho.UKIWA JASIRI UTAKUFA,UKIWA MUOGA UTAKUFA.
UKIIPENDA SERIKALI UTAKUFA UKIICHUKIA SERIKALI UTAKUFA.
UKIPIGWA RISASI UTAKUFA,UKIUMWA MARALIA UTAKUFA.
UKIOGOPA POLISI UTAKUFA,USIPOWAOGOPA UTAKUFA.

Tunaishi ili tufe.KAMA IKIWA KUFA KWAAJILI YA TANZANIA NITAKUFA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Lazima tuandamane,tumechoka na mauaji
Hatujazoea kuuana kama kuku,tumechoka kusingiziwa
Polisi wamuue Akwilini alafu afungwe Lisu?hapana lazima mratibu bashite atoke na Malaika mkuu.
 
Back
Top Bottom