GadoTz
JF-Expert Member
- Nov 20, 2014
- 350
- 567
- Thread starter
- #21
WATU NA VYANZO MBALIMBALI VILIVYOWAHI KUFAFANUA HIPHOP
Baadhi ya watu na vyanzo mbalimbali vya habari vimewahi kufafanua Hip Hop kwa nyakati tofauti tofauti kulingana na mapokeo. Wafuatao/vifuatavyo ni vyanzo na watu mbalimbali waliowahi kufafanua maana ya hip hop:-
AFRICA BAMBATAA
“Hip hop ni harakati za utamaduni mzima. Unapoongelea kughani (rap), kughani ni sehemu ya utamaduni wa hip hop. Ughanaji (emceeing), umanju (deejaying), uvaaji, lugha vyote hivi ni sehemu ya utamaduni. Wavunjaji (break dance), namna unavyotenda, unavyokwenda, unavyotazama (mambo) ni sehemu ya utamaduni na muziki wake hauna ubaguzi rangi. Muziki wa hip hop umetokana na weusi, udhulungi, njano, nyekundu, nyeupe……. ni sehemu za hip hop”.
DJ KOOL HERC
“Hip hop ni kemia (chemistry) ambayo imetoka Jamaika.. nilizaliwa Jamaika na nilikuwa nasikiliza muziki wa kiamerika nikiwa huko huko. Msanii niliyekuwa nikimpenda ni James Brown. Ndiye aliyenivutia mimi, nilikuwa nikicheza vibao vingi vya James Brown. Nilipokuja hapa (Bronx) nilijiweka katika mtindo wa kiamerika ili kuendana na mazingira. Niliweza kukata midundo na kuicheza kwa muda mrefu na watu wakaipenda, niliwapa ladha waliyoipenda……’’
DAVEY D
“Hip hop ni utamaduni ambamo ughanaji (rap) ndimo umeasisiwa. Mwanzoni ulikuwa na nguzo nne ambazo ni sanaa ya machata (graffiti art), mavunjanji (break dancing), umanju (dj) na emceeing (ughanaji). Hip hop ni mtindo wa maisha ambao una lugha yake, mtindo wa kuvaa, muziki wake na fikra zake hukua kila siku. Siku hizi machata pamoja mavunjaji havitiliwi maanani sana ndio maana neno “rap” na “hip hop” yanatumika kwa pamoja kumaanisha kitu kimoja lakini ikumbukwe kila nguzo zina umuhimu na zinaendelea kuwepo katika utamaduni”
Anaendelea kusema “tatizo ni kuelewa maana ya hip hop, mara nyingi huwa inatolewa na wazungu (whites) wenye vyombo vya habari au wale ambao huwa wanapata nafasi ya kuhojiwa katika vyombo hivyo. Huwa wanaelezea maana ya hip hop kwa manufaa yao na sio kwa manufaa ya uma na wale waliouasisi utamaduni huu wa hip hop”
COMMON
“Hip hop ni njia yetu ya kujieleza (expression). Niliipenda mapema zaidi pindi tu ilipotambulishwa (hip hop) kwangu. Nilisikia “the message” ya Melle Mel… nilipenda namna alivyowasilisha na nilipenda pia alichokuwa akikisema