Hip hop Facts Thread

Mkimaliza za marekani, tujadili na zetu wenyewe
Au ndio mke wa maskini, kuwadi mumewe
Nani anashika usukani, nani ni baridi
Kati ya Joh makini, na ngosha Fid
Ama mbishi na zaeed, sio tu 50 na did
Inapendeza mnapoeleza hip hop na miiko
Wapi na lini ilikuwa chimbuko,
Mtiririko wa list ya maandiko
Sio twist ni mziki wenye wenye mashiko

Noted...!!

Maybe nianze kwa kukutajia baadhi wasanii na makundi ya mwanzo ya Hiphop Bongo,...... Fresh XE, BBG, Adili Kumbuka, Salehe Jabir, KBC, Samia X, The BIG, Rymson, 2 proud (Sugu), makundi ni kama vile, Kwanza Unit, Deplowmatz, HardBlasterz, Gang Stars With Matatizo (GWM), Wagumu Weusi Asilia, Young Da Mob, Afro Reign, Jungle Crewz Pose, Bantu Pound, Hardcore unit kwa kutaja machache.

Nani alikuwa anafanya hiphop ya kweli na nani anabaki kusimama kama nembo ya kuutambulisha utamaduni wa hiphop bongo ilo kila mtu ana mtazamo wake.
 
Mashindano ya Michano

Kwenye miaka ya 88/89 kulikuwa na mashindano mengi ya mabreka, udijei na baadae mashindano ya kucheza disko — chini ya Maumba na Lundenga (huyu wa miss Tanzania). Kulikuwepo mashindano ya michano Kimara Studio 2000 Discotheque, chini ya DJ Mac Japhet, ambaye pia alikuwa anachana, kule Kimara Safari Resort.
Vikundi na watu wengine walioshiriki ni kama Villain Gangstar, Hard Core Criminal, Rankim Ramadhani na wengineo. Kwenye mashindano michano ya Lang’ata, mwaka 88, ushindi akapewa Dika Sharp.
Msisimko mkubwa wa mashindano ya michano uliimarika mwaka 91/92 — kulikuja mashindano ya michano yaliyoitwa Yo! Rap Bonanza. Jina hilo lina uakisi wa kioo kikubwa cha Hip Hop cha zama za dhahabu (1990-1995 au miaka ya jirani na hapo); ni jina linaloshabihi kipindi cha runinga cha MTV kilichojulikana sana kama Yo MTV Raps (huko Marekani). Mashindano haya yaliandaliwa na marehemu Kim, ama Abdulhakim Magombelo (M.A.P.), ambaye alikuwa mwandaaji matamasha mashuhuri.
 
Kwenye moja ya mashindano Yo! Rap Bonanza (yalifanyika mwaka 1992, ghorofa ya saba New African Hotel), alipewa ushindi jamaa anaitwa Saleh Jabir, na wa pili alikuwa KBC ama K-Singo. hapo tayari KBC na baadhi ya watu wa KU wanachana toka mwaka 1988. Huyo mshindi (Saleh) mwaka huo huo miezi michache nyuma alikuwa ni mcheza shoo (sio mchanaji), na kwenye maonesho yetu Lang’ata (Kinondoni karibu na American Chips pale) alikuwa akiingia na kufanya shoo za uchezaji wa MC Hammer na Vanilla Ice na jamaa zake wa Ilala. Nimedokeza hilo ili upate mwanga kidogo kuhusu mchanaji na MC hapo.
Shindano lililofuatia walishinda Kwanza Unit. Hili la pili haliongelewi sana, lilifanyika Empress Cinema, jengo la pili kwenye kona ya sanamu la bismini (Mnara wa Askari), kulia kwenye mtaa wa Samora, mwaka 1993
 
II-Proud (siku hizi Sugu, ambaye alitokea mkoani Mbeya) alileta kash kash kidogo kuona kama alionewa kwenye matokeo, ilifikia hadi watu karibu washikane lakini ikatulizwa getini. Watu wa vyombo vya habari wakaanza kuvutiwa na wingi wa watu na uchangamfu wa hayo mashindano. Na kwa uchache wa ufahamu wao wa fani ya Hip Hop, wakaanza kuandika wanachokijua. Na hakukuwa na juhudi sana za kutuhoji kuhusiana na mantiki mbali mbali za Hip Hop zaidi ya kukebehi kwamba jamaa wanaigiza “Umarekani”.
 
Michano ya ‘Kinyamwezi’

Kipindi hiki cha miaka kati ya 88 hadi 93 watu (wengi waliojumuika na kuunda Kwanza Unit) walikuwa wanashinda na kanda za nyimbo za Hip Hop za New York, na ni kawaida kichwa akajua nyimbo hata kumi zote za santuri moyoni. Na ni kipindi ambapo disco la Clouds pia lilikuwa linapata kila santuri na single kutoka Marekani.

Na Kwanza Unit (baadhi, kabla haijawa KU Crew) walikuwa mara nyingi wanashinda Mawingu, hata kabla hakujawa studio ya kurekodi. Vilinge hivi vilijumuisha uangaliaji wa video za muziki na filamu za Marekani, soultrain video, kanda za redio kama zile za Tim West Wood (DJ maarufu sana wa Hip Hop na mtangazaji wa redio), n.k. Hizi kanda watu wanazo hadi leo.

Uwezo wa kuchana wa hawa watu wa karibu ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kama wanachana nyimbo ya mtu inafanyika kama ambavyo unaisikia kwenye CD leo na zao za kuandika. Kifupi Kwanza Unit walikuwa na uwezo wa kuchana kama wanyamwezi wenyewe.


 
Vilinge

Vilinge mahususi vilianzishwa wakati wa disco siku za Ijumaa New African Hotel, baada ya kufungwa kwa disco la Motel Agip (palikuwa panaitwa ‘Shimoni’), bila kusahau disco la Twiga (Mtaa wa Samora). Bonny Luv alikuwa akisimamisha disco kwa kama dakika 20 hivi na kumwachia K-Singo achane; miaka ya 89-90 au jirani ya hapo. Bonny alikuwa anamfahamu KBC na anaujua uwezo wake. Baada ya hapo wakajitokeza kundi la Riders Posse (Nigga One, James Wamba, DJ Wiz). Wiz alikuwa mbaya sana wa midundo-kinywa (beatbox), mtindo ambao leo watu hawafanyi kabisa Bongo. Hili ndio kundi ambalo waliungana na KBC na kuwa wamoja kama Raiders Posse.
 
Umahiri wa Michano

Mjadala nani alikuwa mkali wa michano enzi izo nawaachia wengine ila nitadokezea vitu muhimu vya kuzingatia unapompima mkali wa michano.

Miundo-vina
  1. Mitambao — mitambao inajengwa na mistari yenye vina.
  2. Vina ni maneno yenye silabi zinazoshabihiana mbili au tatu za mwisho kwenye tenzi (shairi). Msisitizo ni sauti na zinavyosikika na sio zinavyoonekana kimaandishi. Kwa lugha ya kigeni vina wanaita ‘rhymes’
Mitambao kwenye uchanaji unategemea na:
  1. Mianguko ya kifundi sana juu mdundo ambayo huwa inakaa sambamba ndani ya hesabu ya nne-nne. Hizo hesabu ndio kutoka mkito kwenda mlio wa snea (snare). Kawaida mstari huwa na urefu wa mkito hadi snea.
  2. Kasi ya mchanaji
  3. Mirindimo inayoingiliana, na jumla ya yote hayo juu
  4. Mtiririko na wa kupanda na kushuka kwa sauti
  5. Lafudhi; inayohusisha rhythm na enunciation (utamkaji)
 
kwanza-unit2bc.jpg


Kwanza Unit 1994:Kutoka kushoto kwenda kulia Eazy -B, D-Rob (RIP), Rhymson(now Zavaara),Fresh-G and Y-Thang.



KBC member wa KU akiojiwa na mtandao wa Bongo Celebrity anasema

'' First and foremost let me start by giving Thanx to All the Kwanza Unit supporters All over the world,from the early days till now..

Kwa kweli tumeshuhudia mijadala mingi kuhusu historia ya Kwanza Unit lakini tatizo watu wengi huitazama Kwanza Unit kama kundi la muziki tuu..while Kwanza UniT is/was a MOVEMENT. That’s bigger than Music…bigger than the number of Emcees in it..

The Movement started in 1992.Malengo yalikuwa ni kwanza kutambulisha na kuelimisha jamii kuhusu utamaduni huu wa HipHop..Pili ni kutumia Hiphop kama chombo au kitendea kazi cha kuelimisha na kuangazia mazuri na mabaya yanayotokea katika jamii zetu za TZ..Long story short EDUTAINMENT..''
 
Kwanini uamini Billboard?
Wewe unaamini hiyo list imekamilika?
Kwanini infuential rapper kama 2PAC hawajamweka?
Kwanza hiyo list inaonekana ipo biased sana.
Nilitegemea mtu kama 2pac awepo,nilitegemea NWA wawepo.
Kwa sababu mimi ninaamini kuwa mc mkali lazima uwe CHANGE AGENT. Sasa kwa mtu kama Kendric Lamar ambaye hana hata miaka 5 kwenye peak ya muziki huu unakuja kusema ni mc mkali?
Sikatai kuwa Kendric ni mkali lakini hiyo ya kusema mcs wakali kuwahi kutokea duniani.
Mtu kama common hayupo
 
Das EFX na ile kitu ya Real hiphop kuna nguzo nyingi za hiphop mule ndani balaa! Hafu kuna Mr. Cheeks wa LB na Method man wa Wu_Tang Clain nawakubali sn ktk flow style zao. Easy sn kumfunika mtu wale jamaa!
 
hip hop kwa mtazamo wangu ni mziki unaoelezea maisha halisi ya mtu mweusi.ukipata kumsikiliza mtu kama common kwa hakika utaelewa nini ninachomanisha.pia kwa kiasi kokubwa uhuru wetu sisi watu weusi umechangiwa pia na mziki huu kwa kutufungua macho na kufahamu haki zetu.hip hop ni mziki unaoweza kusikilizwa na kila rika na kusiwepo na uvunjaji wa maadili ya kiafrika.pia ni mziki unaofurahisha kwa maneno yake yaimbwayo ndani.hip hop ni mziki unaofurahisha na kuelimisha.
 
Michano ya ‘Kinyamwezi’

Kipindi hiki cha miaka kati ya 88 hadi 93 watu (wengi waliojumuika na kuunda Kwanza Unit) walikuwa wanashinda na kanda za nyimbo za Hip Hop za New York, na ni kawaida kichwa akajua nyimbo hata kumi zote za santuri moyoni. Na ni kipindi ambapo disco la Clouds pia lilikuwa linapata kila santuri na single kutoka Marekani.

Na Kwanza Unit (baadhi, kabla haijawa KU Crew) walikuwa mara nyingi wanashinda Mawingu, hata kabla hakujawa studio ya kurekodi. Vilinge hivi vilijumuisha uangaliaji wa video za muziki na filamu za Marekani, soultrain video, kanda za redio kama zile za Tim West Wood (DJ maarufu sana wa Hip Hop na mtangazaji wa redio), n.k. Hizi kanda watu wanazo hadi leo.

Uwezo wa kuchana wa hawa watu wa karibu ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kama wanachana nyimbo ya mtu inafanyika kama ambavyo unaisikia kwenye CD leo na zao za kuandika. Kifupi Kwanza Unit walikuwa na uwezo wa kuchana kama wanyamwezi wenyewe.

Nimeskiliza 'run tingz' ya KU. Bado najaribu kuelewa unavyosema "walikuwa na uwezo wa kuchana kama wanyawezi wenyewe". Stick to the facts, Chief, not opinions.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom