Hillary Clinton alizwa simu mbili -Tanzania

Hillary Clinton alizwa simu mbili -Tanzania

Wabongo bana hivi mnafikiri Mama Clinton anasafiri na South African Airways, Emirates au KLM? Maana kama ni wizi ina maana watakuwa ni wafanyakazi wa shirika la ndege husika ndiyo wako involved. Sasa one of the most powerful person in the world mnafikiri mizigo yake inakuwa handled kama mabegi yenu kwenye precision hahaha ahaha ahahah!!!!!!!!!!1
 
nadhani hiyo stori ameisikia kwa vilaza wenzake ktk vijiwe vya gahawa!
 
Kwa utaratibu wa usafiri anaotumia Waziri wa Nchi za Nje wa Marekani (ndege maalumu, staff kibao), si rahisi wenyeji wake ku handle mizigo yake, inakuwa handled na staff alinaosafiri nao. Hii stori iliyoletwa inatia shaka kuiamini mpaka itolewe taarifa rasmi vyombo husika, au mleta taarifa aukomaze ujumbe beyond reasonable doubt!!!
 

Attachments

  • 110611_clinton_musician_600_1.jpg
    110611_clinton_musician_600_1.jpg
    37.6 KB · Views: 119
Kibaya zaidi watu kuwa na simu zaidi ya moja nimeiona zaidi Tanzania....kila line na simu yake lol! Hata kwa waheshimiwa
 
Kweli wizi ni wizi tu aijalishi unamwibia nani,tulizani hali hii inawatokea abiria wa kawaida tu sekeseke limezuka uko airport
begi ya mh clinton mrs imekutwa imefunguliwa na simu mbili azionekani watu waliokuwepo woote wametangaziwa kuandika report anyway siwezi toa comments ila kwa mimi ningeanza na usalama kwanza...hawa wangejua wapi zilipo maana wakipokea mizigo hawa jamaa wanaangalia mpaka inapoingia kwenye gari zao..anyway tuwaachie wenye

mkweli atajulikana tukumbukane hata usalama nao ni binadamu na wana hamu na wanatamani...

Kama kweli imetokea basi ni ujinga wa wabongo. Simu zinazomilikiwa na makampuni ya simu ya marekani sidhani kama itafanya kazi makampuni ya Tanzania. Makampuni ya marekani yanamonopoly biashara na hakuna kuingilianaa makampuni mengine, kila kampuni simu zake zimekuwa locked. Ni simu chache ambazo unaweza zibadilisha zikafanya kazi kwenye makampuni mengine. Imekula kwao.
 
Kweli wizi ni wizi tu aijalishi unamwibia nani,tulizani hali hii inawatokea abiria wa kawaida tu sekeseke limezuka uko airport
begi ya mh clinton mrs imekutwa imefunguliwa na simu mbili azionekani watu waliokuwepo woote wametangaziwa kuandika report anyway siwezi toa comments ila kwa mimi ningeanza na usalama kwanza...hawa wangejua wapi zilipo maana wakipokea mizigo hawa jamaa wanaangalia mpaka inapoingia kwenye gari zao..anyway tuwaachie wenye

mkweli atajulikana tukumbukane hata usalama nao ni binadamu na wana hamu na wanatamani...

Secretary of State wa Marekani ni sawa na cheo cha waziri mkuu, maana yake ni head of secretaries, na ndio mwenye majukumu ya kimataifa kwa niaba ya taifa la Marekani. Anasafiri na ndege yake na watumishi na wasaidizi kadhaa licha ya wanaotangulia kuandaa safari yake wakiwemo idara mbalimbali za usalama. Hii hadithi nafikiri ni ya kutungwa maana kama watu wakufungua mizigo yake ni wanausalama wake (secret services). Jamani achaneni na habarai za kutunga. Someni habari hiyo hapo chini.

WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton aliwasili jana nchini kuanza ziara ya siku tatu. Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kipawa nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam akiwa na msafara wa watu wasiozidi 50, wengi wakiwa wanahabari, Waziri huyo alionekana kupagawishwa na kikundi cha ngoma alichoungana nacho kihisia kwa takribani dakika 13.

Akiwa na mwenyeji wake, Bernard Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Clinton kwa muda wote alionekana akitabasamu na kutikisa kichwa, huku mwili wake pia ukinesanesa. Waziri Membe ndiye aliyemshitua mama huyo na kuondoka eneo la wacheza ngoma, tayari kwa safari ya kwenda Hoteli ya Kempinski, katikati ya Jiji.

Mama Clinton, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton aliyewasili nchini saa 11:30 jioni na ndege ya Serikali ya Marekani (ubavuni 80002) akitoka Zambia alikohudhuria mkutano wa Mpango wa Soko Nafuu kwa Bidhaa za Afrika (AGOA), leo atakuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Waziri Mkuu wa Ireland, Eamon Gilmore.

Katika mazungumzo hayo yatakayofanyika katika Hoteli ya Kempinski, watazungumzia mradi wa ‘Siku 1,000 wa kutokomeza njaa Tanzania' na kisha baadaye atatembelea shamba la kilimo la Mlandizi, Kibaha, mtambo wa umeme wa gesi wa Symbion uliopo Ubungo na baadaye atakwenda Kituo cha Afya Buguruni.

Source: Habari Leo Jumapili
 
Unanikumbusha nyerere na kenyata wakati wanarudi nchini (kenya na Tanzania) baada ya kuhutubia mkutano wa umoja wa mataifa miaka hiyo, wakiwa juu wanaanza kutua kenyatta akamuuliza mwalimu " Vipi Julias tumeshafika home?" mwalimu akamwambia sidhani lakini naona tumefikia ngoja nitoe mkono njee nitakujulisha; basi mwalimu alivyotoa tu mkono nje saa yake mpya ya Circle 5 aliyonunua ungereza ikaporwa -- akachekaaa akamwambie kenyatta tumeshafika dar tayari.
 
Kudadadeki...........dsm kweli nouma ila safi saaana kama wamemchapa simu maana huyo bi mkubwa hana zaidi ya wizi,uonezi,na unyanyasaji tu kwa hilo saaafi ila msiwaibie WABONGO WENZENU tunarudishana nyuma.............
 
Huyu dada anaonesha anawazimia wapiga matarumbeta, si unaona hapa, hata mumewe anajulikana kwa kupuliza tarumbeta aina ya saksafon (saxophone).
attachment.php

​
 
Acha kusema Tanzania sema Dar es salaam,maana ndipo simu imeibiwa. Nyie watu wa Dar wezi sana hadi mnatia aibu.

Wewe huji kuwa wanaokukulipia padiemu ili uwepo humu wako Dar es Salaam? Ngoja wakusome ukione
 
Huyu dada anaonesha anawazimia wapiga matarumbeta, si unaona hapa, hata mumewe anajulikana kwa kupuliza tarumbeta aina ya saksafon (saxophone).
attachment.php

​

Acha uongo......huyo ni mpiga 'trumpet' siyo 'saxophone'....
 
Pengine waweza hisi hadithi lakini ndicho kituko kinachoongelewa kwamba kuna simu mbil za mh clinton azionekani
binafsi nijuavyo akuna ukweli halisi maana kama zimepigwa naamini uslama nao wamehusika na pia kuna kamera
inayoonyeshwa kila mzigo unapotolewa sasa kwa nini asiende kuangali na badala yake kuanza kutishana waandikiane barua
nafikiri ifike wakati tujithamini wenyewe

Any way tuwaachie wenyewe ..ifike wakati tujipende wenyewe..ni ngumu kuiibiwa mtu kama clinton sijui
wenye upeo na mizigo ya diplomats naomba tusaidiane kwa hilo

Hii ndo karibisha mgeni

Atalijua jiji mama Clinton
 
kama siyo sikukuu ya wajinga leo, lazima watu wa usalama wawajibike. simu ikifuatiliwa inawezekana kupatika hata kama ipo shimoni itakutwa.
 
Back
Top Bottom