Hillary Clinton adai Urusi inamuandaa mgombea wa kike kumsaidia Trump ashinde uchaguzi wa urais 2020

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Mgombea wa zamani wa chama cha Democrat nchini Marekani Hillary Clinton amesema kwamba Urusi inamuandaa mgombea wa kike wa chama cha Democrat katika uchaguzi wa 2020.

Amesema kwamba taifa hilo linataka mgombea huyo kuwania kama mgombea wa tatu ili kugawanya kura na kusaidia kuchaguliwa tena kwa rais Trump.

Bi Clinton hakumtaja mgombea huyo, lakini anaaminika kuzungumzia kuhusu mbunge Tulsi Gabbard. Bi Gabbard alidaiwa kutaja madai ya bi Clinton kama ya 'uoga'.
Katika mahojiano na makao makuu ya mshauri wa rais wa zamani Barrack Obama David Plouffes, Bi Clinton ambaye yeye mwenyewe ni mwanachama wa Democrat alisema kwamba Urusi inamlenga mtu ambaye kwa sasa anaendelea na kampeni zake na kwamba wanamuandaa kuwa mgombea wa tatu.

"Anapigiwa upatu na Urusi,'' bi Clinton alisema, bila ya kumtaja. Wana mitandao chungu nzima na njia nyengine za kumuunga mkono kufikia sasa.

Hatahivyo Bi Gabbard alijibu akimshutumu bi Clinton kwa kuanza kampeni za kumharibia sifa yake.

Alimpatia changamoto mgombea huyo wa zamani kujiunga katika kinyanganyiro cha Ikulu badala ya kujificha nyuma ya wengine.
Bi Gabbard ni mwanajeshi mkongwe na mgombea ambaye ameitaka Marekani kutojifanya kama polisi wa duniani.

Katika mjadala wa moja kwa moja akishirikiana na wagombea wengine 11 siku ya Jumanne, alisema kwamba madai ya vyombo vya habari vya Marekani kwamba anasukumwa na Urusi hayafai hata kidogo.

Bi Clinton pia alimshutumu mgombea wa chama cha Green Party Jill Stein kwa jina kwa kuwa msaliti.

Alizua uwezekano wa kwamba bi Stein anaweza kugombea kama mtu wa tatu kwa kuwa pia naye anasukumwa na Urusi.

''Ni kweli yeye anatumika na Urusi ,namaanisha kaabisa'', aliongezea Clinton. ''Wanajua kwamba hawawezi kushinda bila kuweka mgombea wa tatu''.

Siku ya Ijumaa , Bi Stein alimjibu bi Clinton akisema kwamba anajaribu kuukabili upinzani.
 
Marekani ikifika uchaguzi inaanza kuiota Urusi mbona Urusi hailalamiki dhidi ya Marekani pindi inapokuwa kwenye uchaguzi
 
Back
Top Bottom