Sina ulimbukeni wala chuki na mtu isipokuwa nakerwa na hii mila potofu ya ukeketaji ambayo ni ukatili mkubwa wa watoto wa kike hasa ambao wana umri wa miaka chini ya 18 wanaokamatwa kinguvu na kwenda kufanyiwa tohara
Madhara ya Ukeketaji Watoto wa kike:
Ø Kuzimia kutokana na maumivu makali
Ø Kutokwa na Damu nyingi na pengine kusababisha kifo
Ø Kupata uambukizo (Infection)
Ø Kuambukizwa VVU
Ø Kuambukizwa homa ya manjano (Hepatitis B)
Ø Maumivu makali Kidonda kutopona mapema
Ø Kuoza kwa jeraha
Ø Kupata Tetanus
Ø Maumivu ya Kisaikolojia
Ø Kutofurahia tendo la kujamiana kiufasaha
Ø Maumivu wakati wa kukojoa
Ø Kuziba kwa njia ya mkojo
Ø Kuchanika vibaya wakati wa kujifungua
Ø Kuchelewa kujifungua
Ø Vifo wakati wa kujifungua kutokana na uke wa mzazi kushindwa kutanuka kunakosababishwa na makovu yaliachwa baada ya kukeketwa.
Kwa madhara haya inabidi tupige vita kwa nguvu zote ujima huu hasa kwa mji civilized kama Dar