Hili tusi la Siku hii ya Valentine limenitafakarisha

Mkuu ukikuta baba akiwa mzee hana kiwanja wala nyumba jua kabisa kuwa nae hajawahi kumtunza mzee wake

Sasa wewe usipo pambana na upande wako basi nawe utasubiri watoto waje wakutunze
Acha kukazania kuwa hana kiwanja wala nyumba, kwani alikuzalia porini.Chukulia anamekuzalia kwenye nyumba yake amekutunzia hapo,amekusomesha ,umepata msimamo halafu shukrani yako unasema hayo yote alikuwa anatimiza wajibu wake unamwacha hapo unaenda jenga huko unamwambia apambane na hali yake ,hiyo imekaaje Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kukazania kuwa hana kiwanja wala nyumba, kwani alikuzalia porini.Chukulia anamekuzalia kwenye nyumba yake amekutunzia hapo,amekusomesha ,umepata msimamo halafu shukrani yako unasema hayo yote alikuwa anatimiza wajibu wake unamwacha hapo unaenda jenga huko unamwambia apambane na hali yake ,hiyo imekaaje Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umejiuliza kama mzazi wako wakati anapambana usome wazazi wake alowasaidia au ndio tabia yakusubiri kutendewa wema wakat wewe hukutenda wema

Mimi napenda nione wazazi wangu wameanzisha jambo ndio niwape sapot sio nijifanye naanza mimi
 
Kama huna hela lazima kuona kila kitu ni kigumu na kashfa kibao.kwa mwenye hela Uzi huu hakuna maana
 
Lakini haya mambo ya kukaa kizembe unasubiri eti watoto waje wakujengee haijakaa vizuri! Umetangulia kuliona jua alafu unasubiri dogo aje akujengee? Utasuburi sana! Huu ni ubwege uliopitwa na wakati. Mzazi umridhisha mtoto na sio mtoto kumridhisha mzazi!
Hivi huyu mama anayegonga mawe na kuuza ili apate pesa za uniform na chakula cha kila siku nacho hakitoshi, hangaika yote kuwatafutia maisha mazuri ya baadae watoto wake, atapata wapi pesa ya kujenga? Mwenye wajibu wa kumfuta jasho ni Nani kama sio wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watoto wa kiumeni mara nyingi tunazikosa baraka za Mungu kupitia wazazi wetu kwa mambo mengi yanayofanana na hayo.

1. Wazazi wana nyumba mboovu lakini ukweni umewajengea.

2. Wazazi hawana kitanda kizuri ila mtoto mjini anaitwa Pedezsee la mjini.
Kitanda cha toka unazaliwa!
Godoro la tokea alizaliwa bibi, hadi mjukuu analitumia!

3. Chakula ndiyo usiseme kabisa!
Wazazi wanakula mlenda na mchicha kila siku ila mtoto wao mjini hadi chakula kinamwagwa!



Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu atusaidie
 
Nshawahi kuona daladala imeandikwa "MANENO YA KUHONGA TUNAYO ILA PESA TUNA KAZI NAZO "
Wana MMU hongereni kwa kuona siku ya valentine ya 2020! Nikiwa natoka kwenye mihangaiko ndani ya Costa...Kuna mama jirani alikuwa na mtoto wa kiume mwenye mwaka Kama 1 na nusu hivi maana alikuwa ananyonya...na alikuwa akilia kwa muda mrefu huku akiwa anafurukuta Kama vile anashindana na mama yake...

Tukiwa tunaendelea na Safari na kelele za dogo mithili ya mtoto aliyechomwa sindano na nesi mage, konda wa Costa akamtazama mtoto Kisha akaropoka kwa nguvu" muone jinsi unavyomsumbua mama yako...halafu ukikua uende kuanza kujenga ukweni" watu wote tukaanza kucheka Hadi mama mtoto nae akacheka...

Konda akaongeza sie wanaume shida Sana unahangaika na mama yako ukifanikiwa kupata pesa unaanzisha ujenzi ukweni kabla ya kwenu...

Halafu Kila siku unampiga tarehe mama yako kuwa kuwa nitakujengea Mambo yakiwa mazuri" mwisho wa nukuu,

Nimetafakari Sana Jambo hili siku hii ya Valentine's day of 2020
 
Wabongo bhana, watu simple, maisha yetu simple tu, kila kitu kina jibu simple tu, sasa mtoto analia unasema anamsumbua mama yake, kama anaumwa je? Kulia ndo njia pekee mtoto anaweza kuitumia kuelezea hisia zake kwani hawezi kuongea kama wewe na mimi.
Hoja sio kulia ,hoja maneno yaliyotelewa na kondakta
 
Sio tu watoto wa kiume, mimi nilijipendekeza kufanya finishing ukweni utafikiri kwetu shida zimeisha....wakati huo mahaba yamenitia upofu. Nilipoona true colours za walimwengu na matukio niliyopigwa nilifyata mkia kama mbwa mgonjwa nikarudisha kihere here changu kwetu.
Sasa wamekosa mwana na maji ya moto wanaishia kuntangaza kwa ubaya.Mwenzao nimepiga hatua mtoto wao karudisha mpira kwa kipa kaoa mke wanaishi hapo hapo ukweni.
Nimeamini baraka ya mtoto iko kwa wazazi wake na sio ukweni!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee Kuna lililo kusibu ee
 
Back
Top Bottom