Hili tukio la ajabu sana kulishuhudia

Hili tukio la ajabu sana kulishuhudia

Meja M

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
628
Reaction score
560
Habarini za mida hii wakuu..!!

Natanguliza pole kwa mihangaiko ya siku nzima ili mradi tu mkono uende kinywani..!!

Ilikuwa mwaka 1999 nikiwa shule ya msingi likizo ilinibidi nikamtembelee bibi na babu kizaa mama angu huko kijiji cha Nyakagomba Butundwe wilayani Geita, katika kijiji hiki watu waliishi maisha ya ujamaa sana.

Wiki ya kama ya pili hivi nikiwa kwa bibi yangu nakumbukuka ilikuwa siku ya Jumapili jioni kama saa kumi na mbili hivi alikuja mgeni ambaye alikuwa ni rafiki ake babu wa muda mrefu walikaa na kuzungumza mambo yao kama mnavyojua watoto hatukuruhusiwa kusogea karibu watu wakubwa wakiwa wanazungumza.

Walizungumza stori zao mpaka mida ya kama saa moja hivi ki giza kilianza kuingia, yule mgeni aliiga na kuondoka kama ilivyo desturi babu alimsindikiza mgeni wake lakini kitu cha ajabu babu hakurudi, ilipofika mida ya kama saa nne hivi wasiwasi ukatawala pale nyumbani.

Wajomba zangu walimtafuta sana mpaka kwa yule rafiki ake lakini rafiki ake alidai kwamba waliagana na alirudi nyumbani, juhudi za kumtafuta ziliendelea kwa kushirikiana na wanakijiji wengine lakini hakuna lililofanikiwa.

Siku ya pili baada ya babu kutoweka ilibidi tu tuweke msiba na kuamini amefariki kama ilivyokawaida huko kijijini walitengeneza kaburi kama ishara ya kuwa alifariki.

Baada ya siku kama sita hivi tangu ametoweka ilikuwa ni usiku mida ya kama saa mbili hivi tukiwa tunakula tulisikia hodi alitoka mjomba wangu na alipofungua alikuta ni babu, mjomba yule alikimbia kwani wote tulimuogopa lakini babu alitusihi tusimuogope aliomba maji ya kunywa kisha akaomba akapumzike.

Siku ilifuata asubuhi alituita wote na kuanza kutusimulia ilivyokuwa. Anasema alipokuwa anatoka kumsindika huyo rafiki ake alijikuta anatokea katika njia ambayo hakuielewa japo alidai ilifanana na njia aliyopita akimsindikiza mgeni wake lakini kitu cha ajabu alijikuta ametokea sehemu ambayo haikuielewa kabisa japo kulikuwa na watu waliokuwa wanamshangaa sana kwa jinsi alivyokuwa pia alidai walikuwa wanazungumza lugha ambayo hakuielewa kabisa hawakuwa tofauti na binadamu wa kawaida ila kwa jinsi alivyodai ilionesha kama walikuwa hawaamini kama kuna binadamu kama wao.

Mwisho alidai hakukumbuka ilikuaje mpaka akajikuta yupo kijijini kwake tena. Baada ya kutusimulia alifariki siku iliyofuata.

Mpaka leo nikiwa mtu mzima sielewi kabsa tukio hili. !!
 
Nilivyoona hamna picha tu, sijasoma hata herufi moja kwenye uzi wako.
Haya rudi usome.
IMG-20180711-WA0046.jpg
 
Habarini za mida hii wakuu..!!

Natanguliza pole kwa mihangaiko ya siku nzima ili mradi tu mkono uende kinywani..!!

Ilikua mwaka 1999 nikiwa shule ya msingi likizo ilinibidi nikamtembelee bibi na babu kizaa mama angu huko kijiji cha Nyakagomba Butundwe wilayani Geita, katika kijiji hiki watu waliishi maisha ya ujamaa sana.
Wiki ya kama ya pili hivi nikiwa kwa bibi yangu nakumbukuka ilikua siku ya Jumapili jioni kama saa kumi na mbili hivi alikuja mgeni ambaye alikua ni rafiki ake babu wa muda mrefu walikaa na kuzungumza mambo yao kama mnavyojua watoto hatukuruhusiwa kusogea karibu watu wakubwa wakiwa wanazungumza.

Walizungumza stori zao mpaka mida ya kama saa moja hivi ki giza kilianza kuingia, yule mgeni aliiga na kuondoka..kama ilivyo desturi babu alimsindikiza mgeni wake lakini kitu cha ajabu babu hakurudi..ilipofika mida ya kama saa nne hivi wasiwasi ukatawala pale nyumbani.
Wajomba zangu walimtafuta sana mpaka kwa yule rafiki ake lakini rafiki ake alidai kwamba waliagana na alirudi nyumbani, juhudi za kumtafuta ziliendelea kwa kushirikiana na wanakijiji wengine lakini hakuna lililofanikiwa.
Siku ya pili baada ya babu kutoweka ilibidi tu tuweke msiba na kuamini amefariki kama ilivyokawaida huko kijijini walitengeneza kaburi kama ishara ya kua alifariki.
Baada ya siku kama sita hivi tangu ametoweka ilikua ni usiku mida ya kama saa mbili hivi tukiwa tunakula tulisikia hodi alitoka mjomba wangu na alipofungua alikuta ni babu, mjomba yule alikimbia kwani wote tulimuogopa lakini babu alitusihi tusimuogope aliomba maji ya kunywa kisha akaomba akapumzike.
Siku ilifuata asubuhi alituita wote na kuanza kutusimulia ilivyokua..anasema alipokua anatoka kumsindika huyo rafiki ake alijikuta anatokea katika njia ambayo hakuielewa japo alidai ilifanana na njia aliyopita akimsindikiza mgeni wake lakini kitu cha ajabu alijikuta ametokea sehemu ambayo haikuielewa kabsa japo kulikua na watu waliokua wanamshangaa sana kwa jinsi alivyokua pia alidai walikua wanazungumza lugha ambayo hakuielewa kabsa hawakua tofauti na binadam wa kawaida ila kwajinsi alivyodai ilionyesha kama walikua hawaamini kama kuna binadam kama wao.
Mwisho alidai hakukumbuka ilikuaje mpka akajikuta yupo kijijini kwake tena..baada ya kutusimulia alifariki siku ilifuata.
Mpaka leo nikiwa mtu mzima sielewi kabsa tukio hili. !!
Mmmhh umeniacha njia panda kabisa mkuu"" hii issue nikweli ""!? isije kuwa ni chai "!?
 
Mmh..... Huyo alichukuliwa msukule.....

Akakimbia kukimbia huo usukule

Lakini kwa Bahati mbaya sana, hakuaga pale alipokuwa, kwa hiyo "wataalamu" wakamdedisha jumla!
 
Nimeshasoma kisa kama hichi ninaamini visa kama hivi ni vya kweli.
 
Aise kama ni kweli mbona pole sana ila mliwahi kuweka msiba hako karafiki kababu mngekachapa
viboko mpaka kaseme kamempeleka wapi
 
Back
Top Bottom