Hili tukio la ajabu sana kulishuhudia

Hili tukio la ajabu sana kulishuhudia

Habarini za mida hii wakuu..!!

Natanguliza pole kwa mihangaiko ya siku nzima ili mradi tu mkono uende kinywani..!!

Ilikuwa mwaka 1999 nikiwa shule ya msingi likizo ilinibidi nikamtembelee bibi na babu kizaa mama angu huko kijiji cha Nyakagomba Butundwe wilayani Geita, katika kijiji hiki watu waliishi maisha ya ujamaa sana.

Wiki ya kama ya pili hivi nikiwa kwa bibi yangu nakumbukuka ilikuwa siku ya Jumapili jioni kama saa kumi na mbili hivi alikuja mgeni ambaye alikuwa ni rafiki ake babu wa muda mrefu walikaa na kuzungumza mambo yao kama mnavyojua watoto hatukuruhusiwa kusogea karibu watu wakubwa wakiwa wanazungumza.

Walizungumza stori zao mpaka mida ya kama saa moja hivi ki giza kilianza kuingia, yule mgeni aliiga na kuondoka kama ilivyo desturi babu alimsindikiza mgeni wake lakini kitu cha ajabu babu hakurudi, ilipofika mida ya kama saa nne hivi wasiwasi ukatawala pale nyumbani.

Wajomba zangu walimtafuta sana mpaka kwa yule rafiki ake lakini rafiki ake alidai kwamba waliagana na alirudi nyumbani, juhudi za kumtafuta ziliendelea kwa kushirikiana na wanakijiji wengine lakini hakuna lililofanikiwa.

Siku ya pili baada ya babu kutoweka ilibidi tu tuweke msiba na kuamini amefariki kama ilivyokawaida huko kijijini walitengeneza kaburi kama ishara ya kuwa alifariki.

Baada ya siku kama sita hivi tangu ametoweka ilikuwa ni usiku mida ya kama saa mbili hivi tukiwa tunakula tulisikia hodi alitoka mjomba wangu na alipofungua alikuta ni babu, mjomba yule alikimbia kwani wote tulimuogopa lakini babu alitusihi tusimuogope aliomba maji ya kunywa kisha akaomba akapumzike.

Siku ilifuata asubuhi alituita wote na kuanza kutusimulia ilivyokuwa. Anasema alipokuwa anatoka kumsindika huyo rafiki ake alijikuta anatokea katika njia ambayo hakuielewa japo alidai ilifanana na njia aliyopita akimsindikiza mgeni wake lakini kitu cha ajabu alijikuta ametokea sehemu ambayo haikuielewa kabisa japo kulikuwa na watu waliokuwa wanamshangaa sana kwa jinsi alivyokuwa pia alidai walikuwa wanazungumza lugha ambayo hakuielewa kabisa hawakuwa tofauti na binadamu wa kawaida ila kwa jinsi alivyodai ilionesha kama walikuwa hawaamini kama kuna binadamu kama wao.

Mwisho alidai hakukumbuka ilikuaje mpaka akajikuta yupo kijijini kwake tena. Baada ya kutusimulia alifariki siku iliyofuata.

Mpaka leo nikiwa mtu mzima sielewi kabsa tukio hili. !!
Tatizo mlisha mzika sasa angebaki vipi. .
 
Uzushi tu wa kitoto toto,yaani MTU kupotea sikumoja tu munafanya mazishi?Anyway na kama pia ni kweli basi tambua mzee babu alikuwa kwa mchepuko tu
 
Kama tukio lilitokea Kanda ya Ziwa Lazima nitaamini kwa 99%, nimeishi na wasukuma kwa miaka 20, wakuu kule usumani kuna mambo ya kutisha kuna meneo ukipita utajua tu kama hapa kuna kitu... Natamani nitele mikasa mingi but acha niyaache mama yalivyo...
Mkuu lete tujifunze. ..
 
Kuna mengi yanayoendelea katika ulimwengu wa GIZA.
Wakati nasoma pale Dodoma, maeneo ya chuo cha Mipango nilimtokea demu alikuwa mfanya usafi chuo cha Madini. Akawa ananiahidi lakini chenga nying! Siku moja akanambia nikitoka niende tunaonane AK Garaden ipo pale karibu na maili 2 darajani.
Tukakaa kidogo pale mi nikanywa bia 2 ila yeye alikataa akasema anataka Fanta na chipsi ataenda kula nyumbani ila siku hio akaninyima mzigo. Sikuona tabu cuz nilijua ningempata tu, nikaamua nimsindikize kwani yeye alikuwa anaishi chang'ombe. nakumbuka tulifika mpaka maeneo zinapaki hiace na kisha tukaachana. Cha ajabu nilipotea njia ya kurudi chuo na nilizurura porini na maeneo mengine nakutana na mabwawa ya kina kirefu, Jinsi niliovaa ilichakaa na miiba na hatimaye mida ya saa saba usiku (toka saa 1 hivi jioni) ndio nikaona kanyumba katika kuzurura huko nikabisha hodi akatoka mzee hivi na kijana wake nikauliza njia ya kwenda chuo cha mipango, wakanionyesha kanjia kadogo ndipo nikanyoosha na kuweza kuifikia barabara kuu ya kuelekea chuoni. Nilipata tabu sana na sikujua nini kilitokea wakati nimekaa dodoma miaka mingi toka nasoma Mazengo
Mambo ya giza yapo aisee!
Kazi kweli kweli..haya saa nyingine ni ngumu kuamini mpaka ya kukute.
Pole sana mkuu
 
Pole sana mkuu...haya mambo yapo
 
ha ha ha hawa walikuwa wanastahili viboko maana x kwa kula kande ambazo hawamjui mpishi[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Je zingekua na sumu...[emoji1] [emoji1]
 
Uzushi tu wa kitoto toto,yaani MTU kupotea sikumoja tu munafanya mazishi?Anyway na kama pia ni kweli basi tambua mzee babu alikuwa kwa mchepuko tu
Sio siku moja mkuu..soma vizur
 
Kawaida ukiona kitu cha ajabu au ukiona mtu katika pita pita zako ambaye amekufa siku zilizopita usije kusimulia nawe lazima ufe au wale wavuvi ukiona vibwengo mtoni basi kaa kimya usisimulie ndugu utakufa..
 
Mmmh kazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom