Hili ni Aguko Kubwa kwa CCM!

Hili ni Aguko Kubwa kwa CCM!

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,270
Reaction score
549
Tulio wengi tunajua kuwa kulikuwa na uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 26 ambapo kata 4 za Arusha mjini uchaguzi huo ulihairishwa kufanyika kutokana na mlipuko wa bomu lililo pelekea watu wawili kufariki na wengine 70 kujeruhiwa.

Mimi katika uchaguzi huo nimeliona anguko la CCM katika maeneo yafuatayo:-

1. Chama kikongwe kinachoshika dola kimeweza kupoteza tena kata 5 ambazo kilikuwa kinazishikilia zimechukuliwa na CHADEMA huku CHADEMA wakitetea 2 za kwao walizokuwa wanazishikilia, hilo kwao ccm ni anguko, hawapandi bali wanashuka

2. Anguko la pili na baya zaidi ni lile la kuporomoka kwa maadili , sasa maadili hayapo tena ndani ya ccm, watu wanaropoka ovyo ovyo na kutukana matusi badala ya kujenga hoja kwa kueneza sera za chama chao, pia wameonekana wakitoa rushwa wazi wazi za chumvi, pesa n.k, na hiyo ikapelekea kuumbuka kwa Waziri Mary nagu kule babati walipokamatwa na yule Mbunge wa babati na vijana wa CHADEMA, hilo ccm wamelifanya maeneo mengi sana. Na watu nao katika kuripoti wakaandika Waziri Mary Nagu na Jeetuson yule Mbunge mwingine mwanaume wafumaniwa, niliposikia ghafla nikashituka na nilipofuatilia zaidi kumbe ilikuwa ni fumanizi la kutoa rushwa ya pesa na ndipo nikauzunika sana, nikajiuliza iko wapi ile miiko ya tanu maana kipengele Na. kinasema RUSHWA NI ADUI WA HAKI SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA


3. Kukosekana kwa uvumilivu wa kisiasa, ni hatari kubwa hilo wasipoliangalia vizuri taifa sasa linaenda kuhangamia kuelekea uchaguzi 2015, kwa waliosoma magazeti na wengine kushuhudia ccm wamekwisha kumwaga damu nyingi za watanzania wasiokuwa na hatia kwa kuwajeruhi kila kona kuliko kuwa na uchaguzi huu mdogo, kutegemea vitisho na kumwaga damu ili ushinde bila kufanya hivyo ushindi, hilo ni anguko pia


4. CCM imeaza kupoteza mvuto katika maeneo muhimu ambayo zilikuwa ndiyo ngome zao kuu, maeneo niliyoyashuhudia ccm ikipoteza mvuto huo wa kisiasa ni pamoja na Tanga, Morogoro, Singida n.k. Tanga ccm imeshinda kata zote mbili lakini shaka ninayoipata ni ile tafauti ya kura za ushindi, kata moja wamepishana na CHADEMA kwa kura 19, na kata nyingine wamepishana tena na CHADEMA kwa kula zisizoziidi 30

Kwa haya niliojaribu kuainisha kwa anayeweza kuyaangalia kwa kina bila kujali ushabiki wa kisiasa yanaashiria dalili mbaya mno kwa ccm kuelekea uchaguzi 2015.

Watanzania naomba tukumbushane kitu kimoja , Kitakwimu ccm maeneo ya mijini na majiji kwa sasa haishindi kirahisi, mfano halisi ni katika matokeo haya ya chaguzi hizi ndogo. Hebu jaribu kuangalia kata walizoshinda ccm ni za vijini karibu zote. Kitawimu nimejaribu kuaangalia matokeo ya sensa ya mwaka huu karibu wilaya zoze angalau zaidi ya nusu ya wakazi katika Wilaya yoyote ile. utakawakuta wanaishi aidha katika makao makuu ya wilaya na wengine katika miji midogo iliyopo ndania ya Wilaya.


Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kufuatilia kwa nini majimbo mengi ambayo CHADEMA na NCCR Mageuzi walishinda walishindwa kuwa na madiwani wengi na kuunda uongozi kuendesha halmashauri hizo. jibu ni kwamba ushindi wao kwa kiasi kikubwa ulibebwa na kata zile chache zenye watu wengi wanaoishi maeneo hayo niliyoyataja


Kwa kuhitimisha CCM hamko salama kabisa kuelekea 2015, mtakuja kushangazwa na msiamini kitakachokuja kutokea, maana nyinyi mmezoea siasa za majitaka pasipokufanya utafiti wa kina
 
Kwa hisani yako mkuu hebu tunaomba utuorodheshee hizo kata zote Cdm ilikoshinda ili tujue vizuri make humu kuna taharifa nyingi zinachanganya ili tupate rekodi sahihi
 
Dah ngoja nipite na nifanye uchunguzi wangu binafsi, maana mimi ni zaidi ya Tomaso
 
Mkuu umenena jambo la msingi sana japo najua ama kwa kutokujua au kwa kujipa matuamini CCM wataona hicho walichopoteza si kitu ila kiukweli wanazidi kupungukiwa huku chadema wakiongezekewa, na dalili za nyumba kuanguka ni kuwa na nyufa huku duka linalofilisika lenyewe fremu zinakuwa na mapengo taratibu mpaka zinaishiwa kabisa......hongereni CDM mdogo mdogo mpk tutafika....
 
Kwa hisani yako mkuu hebu tunaomba utuorodheshee hizo kata zote Cdm ilikoshinda ili tujue vizuri make humu kuna taharifa nyingi zinachanganya ili tupate rekodi sahihi

Nimekuwa natafuta pia kutaka kujua matokeo yakoje hasa na nimeambulia habari ifuatayo ambayo labda inatoa mwanga fulani:

Hadi hivi sasa inaonekana CHADEMA imeinyang'anya CCM viti kadhaa vya Udiwani na kutuma ujumbe kuwa ‘upepo umebadilika'. Baadhi ya Kata ambazo matokeo yake yameshajulikana ni kama hivi:
1. Makuyuni, Monduli (ARUSHA) – CCM
2. Minepa, Ulanga (MOROGORO) – CCM
3. Bashnet, Babati (MANYARA)- CHADEMA
4. Nyampulikano, Sengerema (MWANZA) – CHADEMA
5. Masanze, Kilosa (MOROGORO) – CCM
6. Ifakara, Ifakara (MOROGORO) – CCM
7. Tingeni, Muheza (TANGA) – CCM

8. Genge, Muheza (TANGA) – CCM
9. Iyela, Mbeya (MBEYA) – CHADEMA
10. Iseke, Singida (SINGIDA) – CCM
11. Manchira, Serengeti (MARA) – CCM


Habari hii nimeitoa kwenye blogu ya Mwanakijiji.
 
Nimekuwa natafuta pia kutaka kujua matokeo yakoje hasa na nimeambulia habari ifuatayo ambayo labda inatoa mwanga fulani:

Hadi hivi sasa inaonekana CHADEMA imeinyang'anya CCM viti kadhaa vya Udiwani na kutuma ujumbe kuwa ‘upepo umebadilika'. Baadhi ya Kata ambazo matokeo yake yameshajulikana ni kama hivi:
1. Makuyuni, Monduli (ARUSHA) – CCM
2. Minepa, Ulanga (MOROGORO) – CCM
3. Bashnet, Babati (MANYARA)- CHADEMA
4. Nyampulikano, Sengerema (MWANZA) – CHADEMA
5. Masanze, Kilosa (MOROGORO) – CCM
6. Ifakara, Ifakara (MOROGORO) – CCM
7. Tingeni, Muheza (TANGA) – CCM

8. Genge, Muheza (TANGA) – CCM
9. Iyela, Mbeya (MBEYA) – CHADEMA
10. Iseke, Singida (SINGIDA) – CCM
11. Manchira, Serengeti (MARA) – CCM


Habari hii nimeitoa kwenye blogu ya Mwanakijiji.
Tz bado sana aisee.
 
Kwa hisani yako mkuu hebu tunaomba utuorodheshee hizo kata zote Cdm ilikoshinda ili tujue vizuri make humu kuna taharifa nyingi zinachanganya ili tupate rekodi sahihi

Kata ni Nyampulukano- sengerema, Iyela-Mbeya, Ifakara mjini, Lugata, Dongobeshi-Mbulu, Bashnet -Babati, na Iseke- Singida hizo zimechukuliwa na CHADEMA, katika hizo zilizokuwa za CHADEMA mwanzo ni ile ya Mbulu na Sengerema , wametetea kata zao na Kuchukua hizo nyingine 5 zilizokuwa zinashikiriwa na ccm
 
Nimekuwa natafuta pia kutaka kujua matokeo yakoje hasa na nimeambulia habari ifuatayo ambayo labda inatoa mwanga fulani:

Hadi hivi sasa inaonekana CHADEMA imeinyang'anya CCM viti kadhaa vya Udiwani na kutuma ujumbe kuwa ‘upepo umebadilika'. Baadhi ya Kata ambazo matokeo yake yameshajulikana ni kama hivi:
1. Makuyuni, Monduli (ARUSHA) – CCM
2. Minepa, Ulanga (MOROGORO) – CCM
3. Bashnet, Babati (MANYARA)- CHADEMA
4. Nyampulikano, Sengerema (MWANZA) – CHADEMA
5. Masanze, Kilosa (MOROGORO) – CCM
6. Ifakara, Ifakara (MOROGORO) – CCM
7. Tingeni, Muheza (TANGA) – CCM

8. Genge, Muheza (TANGA) – CCM
9. Iyela, Mbeya (MBEYA) – CHADEMA
10. Iseke, Singida (SINGIDA) – CCM
11. Manchira, Serengeti (MARA) – CCM


Habari hii nimeitoa kwenye blogu ya Mwanakijiji.

Wakuu,

Hizi bado ni kata 11 tu katika kata 22 zilizofanya uchaguzi Jana,Tunaoba matokeo zaidi kwa kata zilizosalia. Kuna taarifa Inaonyesha kuwa CDM tumechukua kata 5 zilizokuwa chini ya ccm na kutetea 2 zilizokuwa za CDM, Je kwa ujumla tumepata kata 7 sasa????

magamba sasa hivi hawana tena ushindi ila wana mipango ya kutupa mabomu toka uchina tu. Kiukweli nchi iko hatarini na watu hawa wamedhamiria kuua, hawana hofu tena hata na MUNGU.

Kuhusu Uchunguzi wa POLISI, natilia shaka kama kweli kuna lolote litajiri toka kwa watu wale wale.kanisani kulilipuliwa bomu na watu wakapoteza maisha, uchunguzi wa polisi ukaja na sinema mara ya waarabu, kisha alielipua ni mkristo na hadi sasa sidhani kama Final report ishatoka na kusomeka na watu wote kwamba hio ni taarifa rasmi ya polisi na inaakisi uhalisia.Kuna mlolongo wa matukio ambayo Polisi wamechunguza na waliishia kuja na sinema ukianzia tukio la kutekwa Dr. Uli, Mwandishi Kibanda,Kuuawa kwa wananchi kwenye mkutano wa CDM arusha miaka kadhaa iliopita,Kule Ndago, Igunga, Iringa na kulipuliwa kwa mabomu Mwandhishi mwangosi Kule Nyololo. Haya matukio yoe ccm na mawakala wao walihusika na ndio maana ripoti zake hukaliwa na hakuna mtu anayewajibika kwa unyama huu dhidi ya raia wema.

CHADEMA sasa tuseme Basi.
 
1. Makuyuni, Monduli (ARUSHA) – CCM
2. Minepa, Ulanga (MOROGORO) – CCM
3. Bashnet, Babati (MANYARA)- CHADEMA
4. Nyampulikano, Sengerema (MWANZA) – CHADEMA
5. Masanze, Kilosa (MOROGORO) – CCM
6. Ifakara, Ifakara (MOROGORO) – CCM
7. Tingeni, Muheza (TANGA) – CCM
8. Genge, Muheza (TANGA) – CCM

9. Iyela, Mbeya (MBEYA) – CHADEMA
10. Iseke, Singida (SINGIDA) – CCM
11. Manchira, Serengeti (MARA) – CCM
12. Iseke ,Singida - CHADEMA
13. Ifakara mjini, Ifakara -CHADEMA
14. Dongobeshi, Mbulu -CHADEMA
15. Lungata - CHADEMA
 
CCM inahitaji watu wapya (viongozi) ambao wanaweza kujaribu kujibu kiusahihi na kujenga hoja vizuri juu ya tuhuma mbalimbali zinazokikabili chama chao. CCM inazidi kupoteza mvuto kila siku. Halafu sura zilezile zilizohusika na kashfa na ufisadi ndizo zinasimama jukwaani kutetea chama! Ni vichekesho na chadema wakiendelea na moto wao hadi uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 basi maziko rasmi yatakuwa 2015. Hebu jaribuni kuachana na watu kama lowasa, sitta, membe, nape na mwigulu. Tafuteni majembe ya kweli kama zitto na lissu wa chadema ili muongeze siku zenu za kuishi
 
1. Makuyuni, Monduli (ARUSHA) – CCM
2. Minepa, Ulanga (MOROGORO) – CCM
3. Bashnet, Babati (MANYARA)- CHADEMA
4. Nyampulikano, Sengerema (MWANZA) – CHADEMA
5. Masanze, Kilosa (MOROGORO) – CCM
6. Ifakara, Ifakara (MOROGORO) – CCM
7. Tingeni, Muheza (TANGA) – CCM
8. Genge, Muheza (TANGA) – CCM

9. Iyela, Mbeya (MBEYA) – CHADEMA
10. Iseke, Singida (SINGIDA) – CCM
11. Manchira, Serengeti (MARA) – CCM
12. Iseke ,Singida - CHADEMA
13. Ifakara mjini, Ifakara -CHADEMA
14. Dongobeshi, Mbulu -CHADEMA
15. Lungata - CHADEMA

Kwa hiyo ni CCM 8 CHADEMA 7, Siajabu waliamua kurusha bomu Arusha! Kwa matokeo haya lazima waliozoe ushindi wa Tsunami wachanganyikiwe na kupata kichaa.
 
Hakika hay ni mabadiliko tuendelee kutoa elimu kwa wananchi zaidi waikatae ccm na hata wakiona dalili waikimbie ni hatari sana hawa jamaa na ni zaidi ya UKIMWI bora ukimwi kuliko CCM, MUNGU ibariki Tanzania
 
Kama CCM tunayafanyia kazi maneno yako. Sisi hatutukani wala kupuuza kama cdm
 
Ccm ni janga la taifa la tz. Mungu tusaidie ktk juhudi zetu za kuiondoa laana hii. Wote wenye mapenzi mema na nchi hii na mwitikie ameeeen
 
Back
Top Bottom