Hili Neno: Uchafu Una tabia Moja Mbaya Sana

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,240
Reaction score
44,486
Ukiona mji msafi au mtu msafi au mahali fulani pasafi sana unaweza kufikiria usafi ni tabia ya asili ya vitu. Viumbe vingi sana havina tabia ya asili ya usafi; vipo bila ya shaka viumbe ambavyo vinapenda usafi. Mwanadamu kwa asili yake si kiumbe msafi; tangu kutungwa kwake mimba hadi kuzikwa kwake mwanadamu anazungukwa na uchafu. Ukimwacha mtoto peke yake dakika chache utaona ukweli huu; ataenda kwenye uchafu hata pale anapotumia vitu ambavyo vinaweza kumfanya awe msafi!

Hata mtu mzima asipoamua kujisafisha haichukui muda mrefu kila mtu pembeni yake ataanza kuhisi kuwa huyu fulani ni mchafu. Kimsingi basi utaona uchafu ni zaidi ya tabia; ni hali. Ni hali ambayo si rahisi kuiondoa kwani inabidi uiondoe kwa kuleta hali nyingine ambayo si ya asili; usafi ni hali isiyo ya asili ya vitu vingi. Jambo jingine ambalo tunaweza kusema kuhusiana na uchafu ni kuwa ukizoeleka kwa muda mrefu usafi hautafutwi; mtu akizoea uchafu ni vigumu kumfanya aone umuhimu wa usafi. Hata ukisafisha mara moja usishangae mtu atarudi pale pale kwenye uchafu.

Ni ukweli huu wa pili unaonifanya niseme kuwa uchafu unatabia moja mbaya sana; hupenda kujirudia. Jana watu wengi walionekana wamehamasika kuanzia Ikulu hadi mitaani nchi nzima wakienda kushiriki kampeni ya usafi. Watu walivaa sare, walipiga picha na tushukuru mitandao wakajionesha kuwa kwa siku moja watu wamehamasika kusafisha mazingira yao - ambayo bila ya shaka wote walikuwa wanajua na waliyazoea katika hali yake ya asili - ya uchafu.

Tuliwaona watu wameshika mafagio, mafyekeo, mapanga, reki, mapipa ya kubebea takataka n.k wote wakihamasika na kuhamasishana kuwa "leo" ni siku ya usafi. Na kweli; walizibua mifereji na mitaro iliyoziba, walikusanya mifuko iliyochakaa ya plastiki (mojawapo ya vitu vinavyoharakisha uchafu wa mazingira kwa haraka) na kukusanya kila aina ya takataka zilizoweza kukusanywa na kuzichoma moto. Nchi nzima jana kulikuwa na harufu ya moshi karibu kila eneo kwa sababu watu waliamua kwa pamoja kufanya usafi na kuondokana na mazingira machafu. Kwa siku hiyo moja.

Kama nilivyosema uchafu una ile tabia mbaya sana ya kujirudia. Huwezi kuoga siku moja ukasema umeoga daima; huwezi kukata kucha mara moja ukasema hutokata tena; huwezi kujipangusa sehemu zile zisizotajika ukasema kesho hutajipangusa tena! Uchafu kwa asili yake hujirudia. Tatizo ni kuwa usafi hauna tabia ya kujirudia wenyewe! Usafi hurudiwa kwa uamuzi wa lazima.

Sasa watu wale wachafu; waliozoea uchafu; walioona uchafu na kuuvumilia; waliojua kuwa jamii yao ni chafu na wakaishi kana kwamba hawaoni wakaamua kuwa wasafi kwa siku moja kwa kweli wanastahili kupongezwa. Lakini hili halisemi kitu hasa kwani tunajua nini kitakachojirudia bila kulazimishwa; uchafu. Watu hawa ambao leo huko maofisini bila ya shaka wanasimuliana jinsi walivyoshiriki usafi wanaweza kabisa wakakuta mtu anatupa taka kwenye eneo walilosafisha lakini wasiseme kitu kwa sababu siku ya "usafi" imepita. Wale walioenda mahakamani kudai kulinda kura yao katika mita mia mbili; sidhani kama leo wanaweza kuona umuhimu wa kulinda maeneo yao waliyoyafanyia usafi hata kwa dakika mbili.

Uchafu utajirudia. Takataka zitatupwa kiholela, mifereji na mitaro itaziba tena, watu watatupa mabaki ya chakula ovyo, na kama ilivyokuwa juzi (siyo jana) watu wataanza kusahau umuhimu ule wa usafi na haja ya urudia rudia usafi kiasi kwamba hata watakapokuwa wamezungukwa tena na uchafu hawatojua. Hadi Magufuli akasirike tena na kuwakumbusha haja ya kuwa na usafi.

Ni kwa sababu hiyo naamini - na nina uhakika wengine wamependekeza vile vile - suala hili la kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa masafi kila wakati linahitaji uamuzi wa serikali kutangaza kuwa siku mbili ndani ya mweli ziwe ni siku za usafi katika jamii yote na Watanzania wote washiriki na bila ya shaka zisiwe tena siku za kazi na kuhakikisha kuwa kila ofisi inaweka utaratibu wa kutafuta siku hizi mbili za kuhakikisha mazingira yake - ndani ya mita fulani - hakuna uchafu wowote. Lakini zaidi ni lazima utafutwe utaratibu wa kudumu wa kushughulikia uchafu kwani kwa kadiri binadamu wapo uchafu utakuwepo.

Na hata ukiondoa leo kwa mbwembwe na heshima zote; uchafu utarudia tena.

Swali ni nini kitafanyika utakaporudi; siyo kama utarudia. Tunaposifia mahali, miji au jamii fulani kuwa ni safi tujue tu ni kwa sababu walirudia usafi kuliko kuacha uchafu ujirudie.

MMM
 
Wewe si upo zako US?

Us ni nchi ambayo iko mbali sana .. Ungetakiwa utuambia sisi tufanye nini ili usafi uendelezwe.

Ila usafi ni usimamizi.

Mfano mdogo tu, haiwezekani nchi kama Tanzania au jiji kama la dsm likose magari y kufanya usafi. Gari lenye tanki la maji linaweza kufungwa fagio mbele likapota bara barani. Manispaa zinashindwa kufanya haya?

Tatizo ni CCM. Chama chako brother. Ila mshauri John anaweza kutembelea manispaa yoyote na kuwaambia kuwa anataka aone kila manispaa ina gari hizi ndani sa masaa matatu.
Unadhani ndani ya hayo masaa matatu hizi gari hutaziona?
Kwa sasa kina mama ndio wanafahia bara bara chini ya jua kali tena asubuhi muda wa foleni.
Good day bro
 
Hapa nimechukua baadhi ya mambo.Ni ukweli mchungu lakini ndo hivyo kuwa,asilimia kubwa ya watu jana wamefanya mabo kinafiki kabisa kabisa.Uchafu unashonewa unifomu,selfie???

Hakuna kitufe cha like tu mwanangu, ila jana ndio niliona unafiki wa ajabu. Ile ilikuwa ni show off tu hata kama lilikuwa ni wazo zuri. Ngoja tuone kama itakuwa na jambo endelevu.
 
Kumbe!

Yani kama rada ilivyojirudia kwenye hati fungani?
Ina maana makontena yanaweza patikana halafu baada ya miaka mitatu yakapotea tena, kweli usafi inabidi liwe zoezi la kila siku. Ndio maana watoto wanashikawa hadi fimbo ili waoge nafikiri na hawa wengine wasiopenda usafi kama watoto nao washikiwe fimbo ili usafi usiwe zoezi la siku moja tu.
 
Huyu huyu aliyekuwa anahimiza usafi anatembelea hospitali kwa mbwembwe aliyemuaibisha wilson kabwe hadharani na bashite kwa. Ironically Leo katuliza na kutupiga kwa kulamba zaidi ya 1.5 T dah salam aleikum maamae.

Aungame, atubu na azirudishe atasamehewa
 
Narejea hoja ya Makonda juu ya usafi wa Jiji la Dar; watu wa Dar wamezoea uchafu
Au uchafu umewazoea watu wa dar,kesho ya siku ile ungewauliza wale wafanya usafi kutoka maofisini yalipo mafyagio na reki zao walizonunua kwa ajili ya show ile basi zaidi ya nusu wangekuwa wamesahau walipoyaweka!!
 
Duh.. good observation..
 
Sasa nyie mnaorudisha hizi nyuzi mnataka tuanze kupigishwa deki mitaani ...kama hatuna utaratibu wa usafi kuanzia level ya familia sahau mtaa, mji kuwa msafi.

Tatizo ni kuwa watu tunachukulia uchafu kama sehemu ya maisha yetu; kiasi kwamba tunakubali kuuona kwingine na kuuzoea. Angalia nyumba zetu kama ni safi - na sizungumzii uchafu nje; angalia kuta zake, angalia milango yake..
 
Ukiona mji msafi au mtu msafi au mahali fulani pasafi sana unaweza kufikiria usafi ni tabia ya asili ya vitu. Viumbe vingi sana havina tabia ya asili ya usafi; vipo bila ya shaka viumbe ambavyo vinapenda usafi. Mwanadamu kwa asili yake si kiumbe msafi; tangu kutungwa kwake mimba hadi kuzikwa kwake mwanadamu anazungukwa na uchafu. Ukimwacha mtoto peke yake dakika chache utaona ukweli huu; ataenda kwenye uchafu hata pale anapotumia vitu ambavyo vinaweza kumfanya awe msafi!

Hata mtu mzima asipoamua kujisafisha haichukui muda mrefu kila mtu pembeni yake ataanza kuhisi kuwa huyu fulani ni mchafu. Kimsingi basi utaona uchafu ni zaidi ya tabia; ni hali. Ni hali ambayo si rahisi kuiondoa kwani inabidi uiondoe kwa kuleta hali nyingine ambayo si ya asili; usafi ni hali isiyo ya asili ya vitu vingi. Jambo jingine ambalo tunaweza kusema kuhusiana na uchafu ni kuwa ukizoeleka kwa muda mrefu usafi hautafutwi; mtu akizoea uchafu ni vigumu kumfanya aone umuhimu wa usafi. Hata ukisafisha mara moja usishangae mtu atarudi pale pale kwenye uchafu.

Ni ukweli huu wa pili unaonifanya niseme kuwa uchafu unatabia moja mbaya sana; hupenda kujirudia. Jana watu wengi walionekana wamehamasika kuanzia Ikulu hadi mitaani nchi nzima wakienda kushiriki kampeni ya usafi. Watu walivaa sare, walipiga picha na tushukuru mitandao wakajionesha kuwa kwa siku moja watu wamehamasika kusafisha mazingira yao - ambayo bila ya shaka wote walikuwa wanajua na waliyazoea katika hali yake ya asili - ya uchafu.

Tuliwaona watu wameshika mafagio, mafyekeo, mapanga, reki, mapipa ya kubebea takataka n.k wote wakihamasika na kuhamasishana kuwa "leo" ni siku ya usafi. Na kweli; walizibua mifereji na mitaro iliyoziba, walikusanya mifuko iliyochakaa ya plastiki (mojawapo ya vitu vinavyoharakisha uchafu wa mazingira kwa haraka) na kukusanya kila aina ya takataka zilizoweza kukusanywa na kuzichoma moto. Nchi nzima jana kulikuwa na harufu ya moshi karibu kila eneo kwa sababu watu waliamua kwa pamoja kufanya usafi na kuondokana na mazingira machafu. Kwa siku hiyo moja.

Kama nilivyosema uchafu una ile tabia mbaya sana ya kujirudia. Huwezi kuoga siku moja ukasema umeoga daima; huwezi kukata kucha mara moja ukasema hutokata tena; huwezi kujipangusa sehemu zile zisizotajika ukasema kesho hutajipangusa tena! Uchafu kwa asili yake hujirudia. Tatizo ni kuwa usafi hauna tabia ya kujirudia wenyewe! Usafi hurudiwa kwa uamuzi wa lazima.

Sasa watu wale wachafu; waliozoea uchafu; walioona uchafu na kuuvumilia; waliojua kuwa jamii yao ni chafu na wakaishi kana kwamba hawaoni wakaamua kuwa wasafi kwa siku moja kwa kweli wanastahili kupongezwa. Lakini hili halisemi kitu hasa kwani tunajua nini kitakachojirudia bila kulazimishwa; uchafu. Watu hawa ambao leo huko maofisini bila ya shaka wanasimuliana jinsi walivyoshiriki usafi wanaweza kabisa wakakuta mtu anatupa taka kwenye eneo walilosafisha lakini wasiseme kitu kwa sababu siku ya "usafi" imepita. Wale walioenda mahakamani kudai kulinda kura yao katika mita mia mbili; sidhani kama leo wanaweza kuona umuhimu wa kulinda maeneo yao waliyoyafanyia usafi hata kwa dakika mbili.

Uchafu utajirudia. Takataka zitatupwa kiholela, mifereji na mitaro itaziba tena, watu watatupa mabaki ya chakula ovyo, na kama ilivyokuwa juzi (siyo jana) watu wataanza kusahau umuhimu ule wa usafi na haja ya urudia rudia usafi kiasi kwamba hata watakapokuwa wamezungukwa tena na uchafu hawatojua. Hadi Magufuli akasirike tena na kuwakumbusha haja ya kuwa na usafi.

Ni kwa sababu hiyo naamini - na nina uhakika wengine wamependekeza vile vile - suala hili la kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa masafi kila wakati linahitaji uamuzi wa serikali kutangaza kuwa siku mbili ndani ya mweli ziwe ni siku za usafi katika jamii yote na Watanzania wote washiriki na bila ya shaka zisiwe tena siku za kazi na kuhakikisha kuwa kila ofisi inaweka utaratibu wa kutafuta siku hizi mbili za kuhakikisha mazingira yake - ndani ya mita fulani - hakuna uchafu wowote. Lakini zaidi ni lazima utafutwe utaratibu wa kudumu wa kushughulikia uchafu kwani kwa kadiri binadamu wapo uchafu utakuwepo.

Na hata ukiondoa leo kwa mbwembwe na heshima zote; uchafu utarudia tena.

Swali ni nini kitafanyika utakaporudi; siyo kama utarudia. Tunaposifia mahali, miji au jamii fulani kuwa ni safi tujue tu ni kwa sababu walirudia usafi kuliko kuacha uchafu ujirudie.

MMM

Shida ni aina ya watu waishio TZ, wanataka maendeleo kama nchi nyingine lkn njia za kuyafikia hawazitaki, sasa sijui watafikaje wanataka waamke wakute nchi tajiri.

Leo hii ukisema walazimishwe wawe wasafi watalia udikteta watakuja na waraka wa makanisa n.k. angalia barabarani wakitozwa faini kuzuia ajali wanalia udikteta lkn wanasifia nchi za Kizungu ambazo hata wanatoza faini kali klk kwetu!
 
Ule uzalendo uchwara uliishia wapi? Mbona sasa hivi hamuendelei nao? Unafiki una shida zake. Ogopa wazo la mtu anayeona mwenge ni kitu cha maana. Nyie mliokuwa mnaona ni jambo la maana mbona mliacha, mngeendelea kuunga mkono sisi tulioona ni siasa nyepesi tungeona aibu.
 
Tatizo ni kuwa watu tunachukulia uchafu kama sehemu ya maisha yetu; kiasi kwamba tunakubali kuuona kwingine na kuuzoea. Angalia nyumba zetu kama ni safi - na sizungumzii uchafu nje; angalia kuta zake, angalia milango yake..

Huyo aliyeanzisha hilo wazo la usafi mbona hajaendelea nao mpaka leo? Au ndio mada yako ya juzi kwamba kauzoea uongozi imepata ushahidi. Nilitarajia wale waliokwenda kumuunga mkono wangehamasisha watu waendelee na usafi tujue kweli walienda kuunga mkono na sio kwenda kusaka tonge. Ila cha ajabu nao wamefika ofisini kama akina Katambi wanafanya siasa za majitaka za kutaja mafisadi walioko upinzani wakati miji ni michafu. Mshauri mkuu wote waliohongwa zile 1.5t kwenda kumuunga mkono wapewe mitaa waendeshe usafi mpaka awamu yake iishe.
 
Tatizo ni kuwa watu tunachukulia uchafu kama sehemu ya maisha yetu; kiasi kwamba tunakubali kuuona kwingine na kuuzoea. Angalia nyumba zetu kama ni safi - na sizungumzii uchafu nje; angalia kuta zake, angalia milango yake..
mkuu chahali analalamika hakulipwa milioni12.5 za kampeni ya ccm 2015,wewe ulilipwa? Au umeamua kulilia baharini machozi yaende na maji
 
Back
Top Bottom