srinavas
JF-Expert Member
- Jun 5, 2011
- 4,025
- 3,588
Mtanisamahe,nimevumilia nimechoka wacha leo niseme.
Hivi hili neno maarufu "Rest In Peace" huwa kweli lina maana yoyote kwa marehemu na wanaolitamka kweli huwa wanamanisha hivyo au ni mazoea tu?
Hivi unaposema "marehemu apumzike kwa amani" kuna maana yoyote katika sentensi hii?
Binafsi,sipendi hata kulisikia wala kulisoma na ni kielelezo tosha cha unafiki wa binadamu kwani hutamkwa kwa mazoea tu pasipo hata uchungu mioyoni mwa watu.
Ni bora tuwe tunasema "mungu amrehemu" au "mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu".
Hata kama ni lugha tu,ila kweli inapendeza kusema "marehemu apumzike" na tangu lini marehemu akapumzika zaidi ya roho yake tu kwa imani zetu?
Kusema mungu ailaze roho pema peponi ni kama kumpangia mungu hvi