Hili neno silipendi na wengi wanaolitamka huwa hawalimanishi

Mtanisamahe,nimevumilia nimechoka wacha leo niseme.

Hivi hili neno maarufu "Rest In Peace" huwa kweli lina maana yoyote kwa marehemu na wanaolitamka kweli huwa wanamanisha hivyo au ni mazoea tu?

Hivi unaposema "marehemu apumzike kwa amani" kuna maana yoyote katika sentensi hii?

Binafsi,sipendi hata kulisikia wala kulisoma na ni kielelezo tosha cha unafiki wa binadamu kwani hutamkwa kwa mazoea tu pasipo hata uchungu mioyoni mwa watu.

Ni bora tuwe tunasema "mungu amrehemu" au "mungu aiweke mahali pema roho ya marehemu".

Hata kama ni lugha tu,ila kweli inapendeza kusema "marehemu apumzike" na tangu lini marehemu akapumzika zaidi ya roho yake tu kwa imani zetu?

Kusema mungu ailaze roho pema peponi ni kama kumpangia mungu hvi
 
Mimi naona mtu akifa ni bora kukaa kimya na kufanya utaratibu wa kumzika tu na kuendelea na kazi zingine..

Hayo maneno mengine hayana maana hata kdgo
 
RIP - Rest in peace inatoka kwenye kilatini Requiescat in pace: expression yenye kuonesha tamaa au hamu ya kuona marehemu anaingia katika uzima wa milele ( yaani kupumzika kwa amani). Maneno hayo yanaonesha si matamanio tu ya mtamkaji bali pia yanakuwa ni sala ya kumwombea kwa Mungu ampe hilo pumziko. RIP iko katika lugha nyingi sana za dunia hii.
 
komba kazua mambo. jf itajaa mada za misiba na marehemu
 
Hiyo ni kama kumuomba Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake, na aiweke roho yake palipo pema, pia ni dua ya kum bembeleza Mola mtukufu kwamba na sisi uturehemu pindi tukifariki licha ya madhambi tuliyonayo...ila kusema mweke ANAPOSTAHILI hilo ni kosa kubwa sana (nionavyo mimi) kwa maana unamaanisha kama ni mkosefu basi umuadhibu, hivyo basi unampa ujumbe Mungu kwamba wewe ni msafi sana na huhitaji rehema zake hivyo uko tayari kuwekwa unapostahili ukifariki.
 
Salary Slip unajuaje linatamkwa kwa mazoea tu pasipo uchungu?

Au wewe ndiye unasrma linatamkwa kwa mazoea tu kwa mazoea tu?
 
Last edited by a moderator:
Mie huwa nalitamka pale ambapo naona linastahili kutamkwa kwa mtu ambaye simfahamu kiasi hicho au namfahamu na matendo yake hapa duniani kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni yale ambayo yalijaa upendo mkubwa kwa wanadamu wenzie na Muumba wetu. Pamoja na kuwa hakuna hakuna binadamu ambaye yuko perfect lakini wengine matendo yao hapa duniani kusema kweli ni mabaya mno kwa binadamu wenzao ambao hawajawakosea lolote. Wanakuwa na chuki za kutisha na wakati mwingine huweza kutamka hadharani chuki walizonazo dhidi ya mtu huyo au watu hao. Hivyo pale ambapo naona neno RIP sistahili kulitumia huwa nakaa kimya tu bila kusema lolote lile.
 
Hiyo ni kama kumuomba Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake, na aiweke roho yake palipo pema, pia ni dua ya kum bembeleza Mola mtukufu kwamba na sisi uturehemu pindi tukifariki licha ya madhambi tuliyonayo...ila kusema mweke ANAPOSTAHILI hilo ni kosa kubwa sana (nionavyo mimi) kwa maana unamaanisha kama ni mkosefu basi umuadhibu, hivyo basi unampa ujumbe Mungu kwamba wewe ni msafi sana na huhitaji rehema zake hivyo uko tayari kuwekwa unapostahili ukifariki.
Unajua maandiko yanasemaje?

Labda kama mungu amefanya editing ya maelekezo yake;otherwise, ni kujidanganya tu.

Kwakuwa ni kujifariji,bora hata kusema mungu ailaze mahala pema roho ya marehemu.
 
Sio Lazima Upende Au Ufatishe Kila Kitu Kinachosemwa Au Unachokisikia,
Kama Linakukera Usilisema
 
Kuna muda mwingine tunaondokewa na wapendwa wetu....waliokuwa wakizijaza nyoyo zetu kwa furaha tele kila uchao kutokana na uwepo wao......pamoja na kuwa wametutoka lakini bado tunawahitaji maishani mwetu na ndio maana kuonyesha uchungu tulionao kwa kuondokewa na wapendwa wetu wengine hushindwa kujizuia na kuangua kilio na wengine hadi kupoteza fahamu mara tu wapatapo taarifa za kuondokewa na wapendwa wetu.....kitu ambacho kinatuongezea machungu ni kukubali ukweli ndio hatutawaona tena ndani ya upeo wa macho yetu...hapo ndio mtu kila akikumbuka mpendwa wake hujikuta anaanza kulia.....lakini pamoja na kuwa wametoweka duniani haitufanyi kuwachukia ,bado tuna mapenzi nao.....na kwakuwa hatujui safari yao huko waendako wanafikia wapi....nasi huwatakia safari njema kwa kuwaambia REST IN PEACE.........
 
Back
Top Bottom