Asubuhi hiyo jamaa mmoja ambaye inasemekana ndio mkuu wa kituo cha mwenge bosi wa wale vibaka alikuja kumtolea dhamana atoke , kabla ya yote hayo , yule kibaka akaomba dawa yaani madawa ya kulevya , polisi mmoja akamwambia asubiri kidogo .
Ghafla polisi akaja na unga sikujua ule unga ni aina gani , lakini akampa yule kibaka atumie , kibaka hakuridhika akaomba tena aletewe bangi na moto ili achanganye hizo dawa za kulevya na ile bangi yake .
Kweli polisi yule alienda officini kwake na kumpa mambo yote hayo ndio kijana yule akaanza kuwa na nguvu na kuanza kuwa na furaha kufanya na kuongea mambo yake .