Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 213
Unapoenda sehemu yoyote labda kwa uzuri na ubaya na ukifanikiwa kutoka eneo hilo ukiwa salama basi unashukuru sana , lakini hautakiwi uache mambo yale nyuma , kama mambo hayo ni zawadi kwa binadamu wengine hakuna budi kuyahadithia kwa watu wengine ili wapate kujifunza mengi ya dunia na hata serikali husika ipate muda wa kuweza kujua jinsi baadhi ya watendaji walivyo .
Nami nilipata changamoto nyingi kujifunza hapo mahabusu kutoka kwa wale wengine waliomo mule ndani na kutoka kwa polisi wengine hadithi walizokuwa wanapigiana na mikasa mingine mbali mbali .
Kuna jamaa mmoja aliletwa kule ndani kwa kosa la wizi wa simu pale stendi ya mabasi mwenge , huyu kijana aliiba simu na kumrushia mwenzake ambaye alikimbia na hiyo simu watu wakaanza kumpiga lakini vibaka wenzake walikuja kumuokoa na kumpeleka polisi ambako ndio alikuwa salama .
Asubuhi hiyo jamaa mmoja ambaye inasemekana ndio mkuu wa kituo cha mwenge bosi wa wale vibaka alikuja kumtolea dhamana atoke , kabla ya yote hayo , yule kibaka akaomba dawa yaani madawa ya kulevya , polisi mmoja akamwambia asubiri kidogo .
Ghafla polisi akaja na unga sikujua ule unga ni aina gani , lakini akampa yule kibaka atumie , kibaka hakuridhika akaomba tena aletewe bangi na moto ili achanganye hizo dawa za kulevya na ile bangi yake .
Kweli polisi yule alienda officini kwake na kumpa mambo yote hayo ndio kijana yule akaanza kuwa na nguvu na kuanza kuwa na furaha kufanya na kuongea mambo yake .
Jiulize madawa ya kulevya yanafanya nini kituo cha polisi , bangi zinafanya nini kituo cha polisi ? inawezekana kuna watu wengine wanakuja pale wanawekewa mifukoni ili baadaye watolewe pesa kwa urahisi zaidi .
HII NDIO NCHI YETU BWANA , YAANI WALE WATU TUNAOWATEGEMEA WAWE WATIIFU NA WAADILIFU KULIKO WOTE NDIO WAKO TOFAUTI KULIKO WENGINE NA NDIO WANAONGOZA KATIKA MAMBO MENGINE YASIYOPENDEZA KWA JAMII
HILI NDIO JESHI LETU