Hili ndilo gari linalotumiwa na Rais wa Marekani

Mkuu nikiingia kwenye PC ntakuwekea link ya utorrent uweze kuishusha kwani sio kubwa mb250, ikishindikana ntaku-pm unipe email yako nikutumie..

thanks chief, email io katika pm yako tayari
 
2355933_cadillacone01_jpg334679e82233f60f7be52ab0ccf12d15



Walioona msafara wa obama wataona namna msafara ulipita kwa speed ya kawaida sana tofauti na ile speed tuliyozoea anapopita JK, our president normally huwa ana cruise at an average of 120kmh.

Ile speed ikanifanya nitafute habari zaidi, niliyoyaona yamenishangaza, kumbe Maximum speed ya limo ya Obama ni 60mph tu, sawasawa na kilimita kama 97 kwa saa. hii gari haina ujanja wa kwenda hata 100km kwa saa, hata boda boda inaweza kwenda speed kuliko hii gari

  1. ina uzito unaokadiria kukaribia tani 9
  2. matumizi ya mafuta ni 8mpg, kwa lugha ingine inahitahi lita 35.31 ili kutembea kilomita 100, hii ni sawa na lita 1 kwa kila kilomita 2.8
  3. vioo vyote havifunguki isipokua pale kwa dereva kwa mbele. gari iko 100% sealed
  4. Vioo vya dirishani vina thickness ya inchi 5 wakati milango ni nchi 8.
  5. kutokana na unene wa madirisha na milango, obama hawezi kusikia chochote kinachoendelea nnje, spika zimewekwa ili kunasa sauti za nje
  6. gari ina night vision kamera zinazomuwezesha dereva kuendesha usiku bila hata kuwasha taa
  7. Karibu kila penye nafasi imewekwa tenki ya mafuta
Jambo Tz: SIFA ZA GARI YA OBAMA INAWEZA KWENDA 97KM TU KWA SAA AT MAXIMUM ..... YA JK IPO JUU KWA SPEED
 
Je wajua???

>> Ni Gari la kipekee na la aina yake analotumia rais wa Marekan Barack Obama.

>> Lina thamani ya dola milioni 1.5 za kimarekani sawa na zaidi bilioni nne za Kitanzania.

>> Lina silaha za kutosha aina ya RPC.

>> Ukilitazama kwa nje unaliona kama gari la kawaida tu.

>> Endapo gari hilo litaanguka au kupata madhara yoyote, rais anaweza kukaa ndani ya gari kwa saa 24 akitumia hewa maalum iliyopo ndani ya gari hilo.

>> Pia lina vifaa maalum vya kurekodi mzunguko wa damu ya rais.

>> Pia Gari hilo lina uwezo wa kutembea usiku bila kuwasha taa kutokana na kufungwa kifaa maalum (lenz).

>> Pamoja na matairi yake kuwa imara sana, lakini gari hili lina uwezo wa kutembea zaid ya kilometa 100 likiwa lina pancha. Ni umbali wa kutoka Dar hadi Chalinze.

>> Bodi ya Gari ni imara sana na hakuna risasi inayoweza kupenya.

>>Vioo vya Gari hili vina unene wa inch 8 au cm 20 au mm 200 na hakuna risasi inayoweza kupenya kutokana na utaalam uliotumika.

>> Ni Gari ndogo lakini lina uzito wa tani 9.

>> Pamoja na uzito huo linakimbia hatari.

>> Hakuna kioo kinachofunga zaidi ya kioo kimoja tu, pale anapokaa dereva.

>> Pia Gari hili limewekwa spika maalum ili kunasa sauti za nje rais asikie akiwa ndani.

Hilo ndilo gari analotumia rais wa Marekani.

car.jpg


beast-ri_653.jpg
 
Back
Top Bottom