Hili lijamaa bana . . .

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,709
Huyu dada alikutana na huyu mtu kwenye pati ya harusi,wote walikua waalikwa.Jamaa akamwomba huyu dada contact dada akakataa,jamaa akawa anamsumbua dada wa watu mpaka akaiona pati chungu,lakini dada akashikilia msimamo wake. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Sherehe ilipoisha hili lijamaa likamfuatilia yule dada mpaka nyumbani.Baada ya kupajua jamaa likawa linamsumbua dada wa watu nyumbani kwake dada akawa bado mgumu. . . . . . . . . . . . . . . . . . Juzi lilimemvizia wakati anatoka kazini,alivyofungua mlango jamaa akaingia ndani kisha likamwambia halitoki mpaka lipate jibu kwani limechoka kuteseka na penzi.Dada wa watu akaliambia kistaarabu hamhitaji kwani ana mchumba,lijamaa likaanza kufoka,likadai kwani huyo mchumba wake ana nini.Yule dada akaamua kutaka kutoka nje,likamvuta,purukushani ikatokea. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Dada katika ile purukushani akaona anazidiwa nguvu,akalipiga teke la ikulu,lijamaa likampiga ngumi yule dada likamng'oa jino moja.Bahati majirani tukawa tumefika baada ya kelele za kuomba msaada kutoka kwa yule dada,tulipofika lijamaa likatoka nduki,dada ameshachukua RB.Jamani wadada kuweni makini sana!
 
Pole yake mdada ila mbona unasema kina dada wawe makini, huyo dada hakua makini kivipi?
 
mnaishi wapi huko?
angebakwa je?
utasema ile Soweto ya zamani

hhuyo dada ajifunze 'kutoa vibuti' vyenye kueleweka
usikute na vocha alikuwa anaomba na kupokea
huku akijifanya hataki
na mijitu mingine ustaarabu haukuwafikia
 
The Boss,si unajua mida ya jioni umerudi umechoka,wengine wanawaza kukosa hela,sasa tuliposikia kelele ndo tukaenda kujua kulikoni,kufika jamaa nduki!
 
Sa ile kosa litakua na jina gani? Coz mi najaribu kufanya digital self ya huyo jamaa,inawezekana huyo mdada hakua serious enough 2drive away the guy datc why he kept onto her.............. But still alichofany jamaa it isn't gud am depressed by it japo am sure alikua na ryt reason 4da wrong thing
 
Naamini msimulizi wa hili tukio kuna vipengele hajatusimulia (Pengine amesahau)
Haiwezekani ikawa kirahisi namna hiyo bila ya huyo dada ku'entatain.
 
Huyu dada alikutana na huyu mtu kwenye pati ya harusi,wote walikua waalikwa.Jamaa akamwomba huyu dada contact dada akakataa,jamaa akawa anamsumbua dada wa watu mpaka akaiona pati chungu,lakini dada akashikilia msimamo wake. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Sherehe ilipoisha hili lijamaa likamfuatilia yule dada mpaka nyumbani.Baada ya kupajua jamaa likawa linamsumbua dada wa watu nyumbani kwake dada akawa bado mgumu. . . . . . . . . . . . . . . . . . Juzi lilimemvizia wakati anatoka kazini,alivyofungua mlango jamaa akaingia ndani kisha likamwambia halitoki mpaka lipate jibu kwani limechoka kuteseka na penzi.Dada wa watu akaliambia kistaarabu hamhitaji kwani ana mchumba,lijamaa likaanza kufoka,likadai kwani huyo mchumba wake ana nini.Yule dada akaamua kutaka kutoka nje,likamvuta,purukushani ikatokea. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Dada katika ile purukushani akaona anazidiwa nguvu,akalipiga teke la ikulu,lijamaa likampiga ngumi yule dada likamng'oa jino moja.Bahati majirani tukawa tumefika baada ya kelele za kuomba msaada kutoka kwa yule dada,tulipofika lijamaa likatoka nduki,dada ameshachukua RB.Jamani wadada kuweni makini sana!

msimuliaji umeileta stori in funny way nimejikuta nacheka tuuuuuu
 
It seems huyo dada hakua na msimamo wa kueleweka toka awali..sasa kama mtu unamkatalia mdomoni lakini body language yako inaonyesha unamkubali what do you expect??jamani wadada wenzangu linapokuja swala la hapana semeni hapana kuanzia moyoni,akilini na mwilini and vice versa! Sio No ichanganyikane na Yes..
 
Sa ile kosa litakua na jina gani? Coz mi najaribu kufanya digital self ya huyo jamaa,inawezekana huyo mdada hakua serious enough 2drive away the guy datc why he kept onto her.............. But still alichofany jamaa it isn't gud am depressed by it japo am sure alikua na ryt reason 4da wrong thing

Huyo jamaa alitaka afanyiwe nini ili ajue hahitajiki?
 
hilo lijamaa limbukeni la mapenzi....

mapenzi hayalazimishwi....

tena halifai kuwa hata mpenzi litaleta ubabe tu....

alifungulie kesi ya kutaka kubakwa loh....
 
Huyu dada alikutana na huyu mtu kwenye pati ya harusi,wote walikua waalikwa.Jamaa akamwomba huyu dada contact dada akakataa,jamaa akawa anamsumbua dada wa watu mpaka akaiona pati chungu,lakini dada akashikilia msimamo wake. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Sherehe ilipoisha hili lijamaa likamfuatilia yule dada mpaka nyumbani.Baada ya kupajua jamaa likawa linamsumbua dada wa watu nyumbani kwake dada akawa bado mgumu. . . . . . . . . . . . . . . . . . Juzi lilimemvizia wakati anatoka kazini,alivyofungua mlango jamaa akaingia ndani kisha likamwambia halitoki mpaka lipate jibu kwani limechoka kuteseka na penzi.Dada wa watu akaliambia kistaarabu hamhitaji kwani ana mchumba,lijamaa likaanza kufoka,likadai kwani huyo mchumba wake ana nini.Yule dada akaamua kutaka kutoka nje,likamvuta,purukushani ikatokea. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Dada katika ile purukushani akaona anazidiwa nguvu,akalipiga teke la ikulu,lijamaa likampiga ngumi yule dada likamng'oa jino moja.Bahati majirani tukawa tumefika baada ya kelele za kuomba msaada kutoka kwa yule dada,tulipofika lijamaa likatoka nduki,dada ameshachukua RB.Jamani wadada kuweni makini sana!

Hivi siku hizi bado kuna mambo ya kulazimishana to this extent? Mweee!
 
Unamaanisha nini????

Bora umeuliza ila nimecheka hadi staffs wenzangu wananiuliza umeona nini kwenye laptop yako? NIKAWAJIBU JAMANI TUSIWACHEKE WENYE MAPENGO KISHA NIKAWASIMULIA HADITH HII:loco:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom