Hili la yanga na vodacom limekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la yanga na vodacom limekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by piper, Oct 10, 2012.

 1. piper

  piper JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naomba tujadili sakata hili kati ya Yanga na Vodacom bila kuingiza unazi wowote, je ni halali kwa Yanga kukataa kuvaa jezi yenye logo ya mdhamini (Vodacom) ambayo ina rangi nyeupe na nyekundu kwa kisingizio kuwa ni rangi ya jezi inayovaliwa na watani zao Simba? na je nini mustakabali wa soka letu? maana utakuta timu kama Manchester United jezi zake ni nyekundu ila muda mwingine huvaa jezi za bluu zivaliwazo na timu kama Chelsea, Everton na nyinginezo,karibu tujadili bila unazi
  N.B- ningetupia hii kwenye jukwaa la sports but naona nililete kisheria zaidi
   
 2. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  unajua Watanzania tulio wengi kama sio wote ikijumulisha na wewe na mimi tumekuwa confused. Utakataa au utakubali lakini haitabadidilisha hilo mkuu, wengi wetu ni dhaifu kama ilivyowekwa na Mh Myika siku moja Bungeni.
  Angalia wanaoendesha mpira wa Tanzania (hasa katika capital city) ni akina nani ...zaidi ya 96% ni watu ambao ni hopeless na upeo wa malengo yao ni mdogo mno. Mtu anaweza kuzuia jambo la maana lisifanyike just kwa ahadi ya sahani ya pilau na sod tu, aibu.
  Kuna jamaa mmoja yuko Simba SS pia na huwa anaongea sana kwenye kipindi cha TV cha Sport Kizaazaa, jamaa ni mbishi na mwenye jazba sana lakini nilipokuja kushtuka ni pale nilipogundua kuwa ndiye katibu mwenezi wa ccm wa mkoa wa Dar es Salaa (nafasi ya Nape kitaifa). Na nadhani uliona hata julio alitaka kugombea nafasi nyingine ccm.
  naeleza hayo yote hili angalau kutoa picha ya hali halisi ilivyo.
  Katika mpira wa Tanzania ikichochewa na dar es Salaam, bila kujua fitina na unafiki huwezi kufanya lolote na huo ndio msingi wa viongozi wa Simba na Yanga. Lakini kama tunavyojua unafiki na fitina ndio msingi mkubwa wa umasikini wa mtu/jamii/jumuia/chama/timu/taifa lolote hapa duniani.
  Hiyo hoja ya Vodacom ni muendelezo huo huo wa watu ambao ni hopeless na wasiowaza mbali zaidi ya matumbo yao. Tuliiga mambo ya mpira kutoka Ulaya lakini huko japo wana mambo yao ya rangi za jezi (identity) likija suala la biashara na pesa hawaangalii hilo, wanaangalia pesa na maendeleo.

   
 3. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni ujinga tuu! mbona fedha za udhamini wamechukua.TFF nao wanawaogopa yanga!
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kisheria naamini Yanga wako sahihi... Yanga is not not part to the contract signed between TFF and Vodacom, therefore, the team, or any other Premier League team for that matter, is not bound to that contract.
   
 5. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Soka la bongo linaendeshwa kisanii. Club haitakiwi kuwa na uhusiano na mdhamini wa jumla wa ligi kwa kuwa yeye ameingia mkataba chama cha soka hivyo vilabu vyote ni Third Party. TFF na Vodacom wanatakiwa kuingia makubaliano ya udhamini wa ligi kwa ujumla ambao hautahusu vilabu, otherwise Vodacom waingie mkataba mwingine na vilabu. Hapa kuna umbumbumbu na usanii wa hali ya juu wa Vodacom kuviibia vilabu. Udhamini kupitia vodacom unavinyima vilabu uhuru wa kupata lucrative deals za kutangaza biashara kwa sababu tangazo la biashara mbele ya jezi ndio linalolipiwa fedha nyingi zaidi, lakini hapa TFF wameishaingia mkataba na Vodacom na wanalipiwa hadi Administration costs wakati vilabu vinapata fedha kiduchu. Ndio maana vilabu vya ligi ya Uingereza havivai nembo za Baclays wala kule Spain hauoni Club yenye nembo ya BBVA, kila club ina sponsors wake. Huu wizi wa TFF kuchukua hela za vilabu kuanzia viingilio vya mlangoni hadi matangazo ya jezi unatakiwa kukoma mara moja. Timu zinazokosa udhamini kwa kutokuwa na marketing strategy ndio zilazimishwe kuvaa nembo za Voda
   
 6. piper

  piper JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,931
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Yanga sio party to the contract signed between Voda na TFF, lakini kwa kukubali kwao kushiriki ligi inayodhaminiwa na voda, tayari wanabanwa na kanuni za ligi hiyo. Labda kama suala ni uhalali (legitimacy) wa kanuni hizo za ligi! Kwa hiyo kama TFF wakitaka kuwa strict, Yanga atakuwa na option mbili tu, kuvaa nembo jezi yenye nembo ya mdhamini na kushiriki ligi husika au kujitoa/kutolewa kwenye ushiriki wa ligi hiyo. Nafahamu kumekuwepo na mazungumzo kati ya Yanga na mdhamini ili kuiruhusu Yanga kuvaa nembo lakini ikiwa na rangi ambayo sio nyekundu!

  Binafsi nadhani bado kuna tatizo kwa TFF na ushirikishwaji wa vilabu katika mikataba ya udhamini.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hapo uko sahihi, Yanga hawabanwi na sponsorship contract bali na kanuni za ligi which they have signed. But, do the kanuni za ligi zinalazimisha kuvaa jezi za voda?
  Jambo la pili ni la precedent... mwaka jama Voda waliwakubaliana na Yanga kuhusu rangi na wakawatengenezea nembo nyingine, why mwaka huu hawataki kufanya hivyo?
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,931
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Kanuni zinawataka kuvaa jezi za mdhamini wa ligi. kwa hiyo kama Voda wameweka nembo yao kwenye hizo jezi, kikanuni yanga hana 'uwezo' wa kuzikataa. Na ndio maana umeona mwaka jana walilazimika kuzungumza na mdhamini - lakini hiyo bado inategemea hisani ya mdhamini tu!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wasi wasi wangu ni kuwa kanuni zimaweza kuzilazimisha timu kuvaa jezi za mdhamini, lakini je, kisheria, hiyo inazifanya timu ziwe bound kwa contract between TFF na VOda?
  Na pia, What is legal connection between Kanuni za ligi na mkataba wa udhamini between TFF na Voda?
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,347
  Likes Received: 22,197
  Trophy Points: 280
  Timu inaongozwa na teja, wachawi, makomando na vigagula, yaani reasoning capacity yao iko finyu kuliko maelezo.
  Wakisusia jezi wasusie na hela za udhamini.
   
 12. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,931
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Timu hazipo bound na mkataba moja kwa moja isipokuwa kupitia kanuni hizo. Voda imeingia mkataba na TFF wa kudhamini ligi ambayo ina kanuni za uendeshaji wake. Naamini hata huo mkataba utakuwa kwa namna moja ama nyingine unafanya reference kwenye kanuni hizo. Yanga (na timu nyingine) kwa kukubali kushiriki ligi hiyo, kimsingi wamekubali kufungwa na kanuni za ligi hiyo. Na zaidi, kwa kukubali kuchukua vifaa kutoka Voda, pia impliedly wanakubali "udhamini" wa kampuni ambayo rangi yake ya biashara ni nyekundu.
   
 13. O

  Omugurusi Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa naona na Vodacom wana uvyaifu. Kama wao rangi yao ni nyekundu kwanini watengeneze nembo ya rangi tofauti ? Naamini hiyo logo yao imesajiliwa na BRELA sasa inakuwaje leo waisikilize timu. Jambo lingine ni uonevu kwa timu ndogo kama African Lyon, kwa nini nao hawakupewa fursa ya kuongea na voda ?
   
 14. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  ni kwa vile waliangalia kiasi cha pesa tu na sio contents za mkataba.
  Mfano mwingine wa tatizo la TFF na clubs ni issue ya African Ryon. Wangelikuwa wanasoma contents wangeliweza kuepuka kukosa mkataba wa ZANTEL lakini hwafany hivyo
   
 15. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna vitu tujiulize kwenye hili swala.
  *je huo mkataba una sainiwa na nani kati ya TFF na Yanga nani ana sign mkataba na vodacom

  kama yanga haku sign mkataba na vodacom basi Yanga is third party to that contract!

  Pia tuangalie ina wezekana Yanga waliingia Mkataba na TFF kuhusu hizo jezi kwa hiyo pia hapo yanga wana weza kubanwa.

  Pia tuangalie miongozo ya sheria za TFF zina semaji kuhusu mdhamini mkuu,timu na jezi zao.

  Tukiangalia hapo ni kwamba yanga walikuwa wana kataa rangi tu, kwa hiyo ilikuwa ni swala la majadiliano na mdhamini tu!

  Pia kama yanga hawana mkataba na Vodacom basi hawa kuwa na kosa kukataa jezi,
   
 16. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,346
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  TFF inawaogopa Yanga PERIOD! Kwanini wasisimamie sheria n kanuni zao?? Yanga hawavai nembo ya mdhamini wa ligi?? Yanga wametumia njia za panya kupata kibali cha kocha wao kufanya kazi nchini ilhali tff ndo waliotakiwa kuwaombea. Inatakiwa kocha wa yanga asiwepo ktk benchi kwani tff hakuna kumbukumbu zake zozote?? Yanga inadaiwa na njoroge, papic, marashi, ndlovu, zaidi ya milioni 170. Hukumu imetoka fifa tff wameshindwa kuchukua hatua hata ya ile kuwakata mapato ya mechi zao ili kulipa deni hilo kilazima kwani inaharibu jina la nchi. Pesa za twite hazijalipwa. Siku 21 walizotoa zimekwisha siku nyingi hakuna lolote linalofanyika. Hata ktk hili nategemea hakuna lolote litakalofanyika.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
 17. zethumb

  zethumb JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 606
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hao nao wameishiwa hoja, waangalie Ulaya wanaocheza mpira sio kunywa kahawa na majungu pale kwenye harufa mbaya jangwani! Madhalan karibia kama si timu zote zinavaa rangi zoooote....hpa duniani na soka linachezwa! Mnapigwa goli TANO hapa mnaleta hatuvai nguo nyekundu...!
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kusema hivi kwani nani ana jua mikataba yao ina semaje?

   
 19. j

  joel amani Senior Member

  #19
  Oct 16, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijui nitakuwa nje ya mada hii,napenda kuuliza kwanini timu ya taifa ilibadilisha jezi ya timu ya taifa kwa kuondoa rangi ya njano na kijani? je lilikuwa liathari gani kisoka? kwanini yanga wakatae hiyo nembo yenye rangi nyekundu
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Ni mgundua kuwa Tff ndio wana tatizo.

  Kwa maelezo niliyo pata kutoka kituo kimoja cha redio nime gundua kuwa
  *vilabu havijui huo mkataba una nini
  *vilabu ni party ya huu mkataba

  *vilabu vyetu vingi havijui haki zo kwenye mikataba.
  * Tff kuna vitu ina ficha kwenye hiyo mikataba.

  *Tff inajua vilabu vingi havijui haki zao hivyo wana tumia hiyo nafasi.

  (Leo hii kupitia redio fulani nimesikia vilabu vimeagizwa kama vina taka kuona mkataba waende offisi za Tff waka usome palepale na hawaruhusiwi hata kutoa copy ya huo mkataba au kuondoka nao)

  katika hili vilabu vimedharirishwa sana na kunyimwa haki zo.

  *kwanza vilabu vilitakiwa viusome mkataba huo kabla ya kuwa signed
  * vilabu pia vina haki ya kubaki na copy ya mkataba hili visiweze ku breach contract

  hivyo basi ni vyema vilabu vikagomea huo mkataba kwani hautoi haki kama law of contract inavyo sema.

  Na wapongeza African Riyon japo sijui kama walikuwa wana gomea mkataba au jezi, kwa hiyo naona wana haki maana hawakujua terms za hiyo contract.

  Na viomba vilabu visiangalie jezi tu na rangi kama yanga wanavyo fanya bali waingie ndani kabisa na kwenye haki zao kuhusu contract!
   
Loading...