Hili la yanga na vodacom limekaaje?

Ni ujinga tuu! mbona fedha za udhamini wamechukua.TFF nao wanawaogopa yanga!
wengine wanasema hawanywi pombe lakini udhamini wa pombe ruksa!
Suala la advert sawa linaendana na ethics za makampuni husika lakini hakuna hata sehemu moja mwanachama wa Simba/Yanga na wengineo wanaweza kukwambia origin ya hizi rangi za klabu zao ilitokana na nini mbali na kuiga kutoka Brazil/Sunderland na upuuzi mwingine kama huo.
Sasa ikifika hatua 'kiongozi' (maana wazee sio viongozi) unasema bora timu ifutwe basi nia yao sio kuendeleza michezo bali uchawi maana wote tunajua michezo ni pesa kwa wakati huu. Na waje waseme kuwa wakiwa na jengo la biashara (kitega uchumi) kuwa hawawezi kumpangisha mpangaji asiye na mapenzi na timu yao au anayeuza vitu vyenye rangi nyekundi!

 
Back
Top Bottom