Hili la wazanzibari kuchoma baa limekaaje?

mbona wanapata taabu sana...waende pale kiwandani TBL wakipige kiberiti kiwanda chote na vingine vyote

labda watafarijika

kaka hapo na mimi nimekupata vizuri.
ingefaa pia ungefanya tathmini ya kutosha juu ya mikoa inayoongoza kwa kuwa na waathirika wengi wa UKIMWI.
1.0 IRINGA 2. MBEYA 3. MOSHI. 4.0 MWANZA. 5.0 DSM (KINONDONI). 6. ARUSHA.
Na mikoa ambayo ina idadi ndogo ya waathirika wa ukimwi = Zanzibar.
Halafu ungefanya pia utafiti wa mikoa ambayo katika sakata la EPA na ufujaji wa Rasilimali za nchi aka MAFISADI ni ipi imeongoza. MOSHI NA ARUSHA.
Mungu alisema ukweli: "Ndani ya pombe kuna manufaa kidogo lakini madhara yake ni makubwa kuliko manufaa yake".
Napongeza ndugu zetu kuchoma mabaa.
Ni aibu kuhusianisha pombe na Ukristu.

Kweli wanaonewa, wakristo wengi si walevi!

Mi naona sawa tu maana hivi Bar zimejaa kila kona ya nchi mpaka kwenye sehemu za kuishi watu, utakuta mtu anafungua Bar karibu ya shule, Kanisa na Msiki. Hii Tabia inazidikukuwa maana hakuna serikali inayofuata sheria ufisadi kila kona. Yanahitajika mapinduzi kama ya Tunisia au Misri

Hujui unachoongea sijui umetoka kuamka?, mimi nipo hapa Zanzibar na kuna Bar moja imechomwa usiku wa ijumaa na watu ambao hawajulikani na kulikuwa na kesi mahakamni jamaa mwenye bar kawashinda kesi lakini kutokana na chuki na watu ambao wanatoka bara ndio maana wakaamua kurusha mabomu na kuunguza kila kitu ikiwemo pikipiki kubwa na pool tables,,, hivi tatizo hapa liko wapi kwani mtu akilewa si analewa kwa pesa zake, kusema kweli hii serikali ya mseto hapa Zanzibar ni maafa tupu, huwezi amini kuna jamaa muuza matunda jana wamekuja wamebeba kila kitu wamepeleka manispaa na wakati hiyo biashara anaifanya kwa miaka 9 mahari pale lakini kwa kuwa ni mwana CCM tu kafanyiwa vituko ni serikali ya mseto....

:msela:Huu kwa kweli ni uhuni usio na mpango wowote. Ukikubali utalii maana yake unakubali na mambo yote yanayoaambatana na utalii. Utalii wa kutegemea nchi za Ulaya na Amerika ni LAZIMA uambatane na pombe na totoz. Tuache hizo tufanye kazi

kusema kweli hii serikali ya mseto hapa Zanzibar ni maafa tupu, huwezi amini kuna jamaa muuza matunda jana wamekuja wamebeba kila kitu wamepeleka manispaa na wakati hiyo biashara anaifanya kwa miaka 9 mahari pale lakini kwa kuwa ni mwana CCM tu kafanyiwa vituko ni serikali ya mseto....
Koh koh koh...MMhm! Interesting, siku hizi unaisemea CCM

Hivi hakuna kitu cha maana mnaweza kutetea?

Always nyie wenzetu upande wa pili kazi mmekuwa wepesi sana kutetea uchafuzi wa maadili?

What wrong guys?

Hivi hakuna kitu cha maana mnaweza kutetea?

Always nyie wenzetu upande wa pili kazi mmekuwa wepesi sana kutetea uchafuzi wa maadili?

What wrong guys?

huu ni uchafuzi na unyanyapaa wa lugha za watu.....

Written by administrator // 05/02/2011 // Kitaifa // 14 Comments

Na Salma Said,
SIKU chache baada ya wananchi wa Mji Mkongwe kutoa malalamiko yao kudharauliwa amri ya mahakama ya kutaka baadhi ya baa zilizopo katika makaazi ya watu zifungwe, watu wasiojulikana wameripua na kuiteketeza kwa moto baa moja iliyopo Mji Mkongwe Zanzibar.
Wimbo hilo la watu kujichukulia sheria mikononi limeanza wiki iliyopita katika maeneo ya Darajabovu na Mwanyanya kuzichoma baa mbili zilizopo katika maeneo ya makaazi ya watu baada ya malalamiko yao ya muda mrefu kutochukuliwa hatua yoyote.
Juzi watu wasiojulikana waliiongia katika baa ya Migombani iliopo kati kati ya Mji Mkongwe wa Zanzibar na kuteketeza kila kitu ikiwemo masanduku ya kuhifadhia ulevi na vitu vyengine muhimu vilivyopo katika baa hiyo.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea majira ya saa nane za usiku, walisema kwamba moto huo ulianza baada ya kusikika mlio mkubwa wa mripuko ambapo majirani walitoka kwenda kuona kinachoendelea na kukuta moto ukiwaka eneo hilo la baa.
Kwa mujibu wa mlinzi aliyekuwepo katika lindo la baa hiyo alisema awali aliwaona watu wawili wakiingia ndani ya jengo hilo na baada ya muda mdogo akasikia mlio wa risasi ambapo walipigwa mbwa wawili waliokuwepo katika baa hiyo kwa ajili ya ulinzi ambapo mbwa mmoja aliuliwa baada ya kupigwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni risasi baada ya kubweka kwa sauti kubwa.
“Nimesikia kishindo kikubwa cha mlio kama vile kitu cha kuripuka na sio muda mrefu nikamuona mbwa wetu mmoja amelala na kufariki dunia hapo hapo nadhani ilikuwa ni risasi lakini sina hakika hiyo….alisema mlinzi huyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema uchunguzi zaidi unaendelea ili kujuwa chanzo cha tukio kwani hivi sasa kumeibuka vitendo hivyo kwa kasi.
“Tumepata taarifa ya tukio hilo la kuchomwa moto kwa baa mmoja iliopo katikati ya Mji Mkongwe…hatujajuwa chanzo chake kinatokana na nini lakini tutatoa taarifa baada ya kufuatilia kwa kina chanzo na sababu za moto huyo kwa sababu hatuwezi kutoa taarifa wakati watu wetu ndio wanafanya hiyo kazi ya kiuchunguzi” alisema Kamanda huyo.
Mkurugenzi wa baa hiyo na mmiliki wa biashara hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Christopher John Makata alisikitishwa na kitendo hicho cha kuripuliwa baa yake ambapo amesema amepata hasara kubwa kutokana na mali yake iliyokuwa ikihifadhiwa ndani ya baa hiyo kuteketea kwa bila ya kubaki kitu.
Makata alisema kwamba wakati moto huo unateketeza baa hiyo kulikuwa na jumla ya kreti mia sita (600) za bia pamoja na vinywaji vyengine vikiwemo soda na maji ya chupa ya aina mbali mbali ambazo zilikuwa zikiuzwa katika baa hiyo.
Aidha alikiri kupata hasara kubwa inayofikia zaidi ya shilingi milioni 60 na kusema kwa sasa anafikiria kuhamisha biashara zake Zanzibar kufuatia kupata mkasa huo ambao umerudisha nyuma maendeleo ya maisha yake.
“Nimepata hasara kubwa ya kuchomwa moto kwa baa yangu maisha yangu nategemea biashara zangu ikiwemo hii baa, mali zangu zote zilizokuwa zimehifadhiwa katika chumba cha akiba kwa hivyo kuteketea kwa moto katika baa yangu kumemaliza kila kitu changu”alisema Makata.
Uchunguzi zaidi unaonesha kwamba baa ya Migombani ambayo ipo kati kati ya Mji Mkongwe wa Zanzibar ilikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakaazi wa eneo hilo ambao waliweka pingamizi mahakamani kupinga uhalali wa kufanya biashara eneo hilo.
Khaleed Said Gwiji anasema suala la baa katika Mji Mkongwe linawakera wakaazi wengi kwa kuwa baa hizo mbali ya kuwa katika maeneo ya makaazi ya watu lakini baadhi yao zipo karibu na nyumba za ibada na kibaya zaidi ni kuwa zinaendesha biashara za ukahaba na kupiga miziki usiku kucha jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na wakaazi wa eneo hilo.
Hata hivyo baa hiyo ambayo tokea mwaka jana kesi yake ambayo ipo katika ngazi ya kukatiwa rufaa ingawa kesi hiyi imekuwa ukisuasua jambo ambalo wakaazi wa Mji Mkongwe wakilalamika kwamba haikupaswa kisheria kuendesha biashara zake hadi hapo uamuzi wa mahakama utakapotolewa lakini ilikuwa ikiendelea na biashara zake kama kawaida.
“Huu ni mwaka mmoja sasa wananchi tunasubiri kusikilizwa kwa rufaa ya pingamizi la mfanyabiashara huyo bila ya mafanikio wakati biashara ya ulevi katika eneo hilo ikiendelea kitendo chake cha kuuza bia kama kawaida nadhani ndicho kilichowatia watu hasira hizo” alisema mkaazi mmoja wa Mji Mkongwe ambaye anaishi karibu na baa hiyo.
Alisema wakaazi wa Mji Mkongwe wamekuwa na kilio cha muda mrefu kutoka na kuenea kwa baa katika mkaazi ya watu jambo ambalo biashara za uhahaba, wizi na upigaji wa miziki kwa sauti kubwa ni miongoni mwa malalamiko ya wakaazi hayo jambo ambalo serikali haijalichukuliwa hatua za kakusudi kukabiliana na kero hizo za wananchi.
Wakizungumza na waandishi wa habari juzi wananchi wameilalamikia baa ya Dharma Lounge, iliuopo Vuga, wananchi wa Mji Mkongwe wamesema kuwepo kwa baa hiyo kunachochea vitendo vya uhalifu katika eneo hilo ikiwemo kufanyika vitendo vya kuuza miili na kufanya fujo za miziki usiku kucha.
Wananchi hao walisema Dharma Lounge ni miongoni mwa baa zinazoendelea kuchangia kero hiyo licha ya Mahakama ya Vileo ya Mwanakwerekwe kutoa amri ya kufunga baa hiyo lakini bado inaendelea na shughuli zake kama kawaida.
Amir Hamza Amir, Khaleed Said Gwiji, na Raya Ali ambao ni wote ni wakaazi wa Vuga eneo la Mji Mkongwe wamesema serikali inapaswa kusimamia vyombo vyake kwa kuhakikisha sheria zinafuatwa.
Amir alisema kuendelea kuwepo kwa shughuli za baa hizo katika eneo lao kunachochea kasi ya mmomonyoko wa utamaduni, mila na desturi za Zanzibar zinazozingatia misingi ya dini jambo ambalo serikali inatakiwa kuingilia kati suala hilo .
Kwa mujibu wa hati iliyotolewa na Mahakama ya Vileo ya Mwanakwerekwe Januari 24, mwaka huu, baa ya Dharma Lounge pia imenyimwa leseni kwa kipindi cha mwaka 2011.
Uamuzi huo, kwa mujibu wa hati hiyo ambayo gazeti hili pia imepata nakala yake ilitolewa na Hakimu Abdulrazak Ali ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Mahakama ya Vileo ya Mwanakwerekwe.
Hakimu Ali akitoa uamuzi huo, alikataa ombi la Dharma Lounge kuongezewa muda kw akupew akibali cha mwaka huu wa 2011 na kusema kwamba baa hiyo haitaruhusiwa kuendelea na shughuli zake katika eneo hilo kutokana na wananchi wa eneo hilo kukataa baa hiyo katika eneo lao.
“Ombi limekataliwa. Muombaji asipewe leseni ya 2011, kwa sababu majirani zake hawataki baa yake,” alisema Ali katika hati hiyo ya mahakama ya Manakwerekwe iliyotolewa uamuzi januari 24 mwaka huu.
Wiki iliyopita baa ya Peace Love iliopo Daraja bovu pamoja na baa iliopo Mwanyanya zilichomwa moto kwa madai kwamba zinaendesha biashara ya ulevi katika maeneo wanayoishi wananchi.
Hadi sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijasema lolote kuhusiana na suala hilo la kuripuliwa kwa moto baa ambapo kwa mujibu wa sheria wamiliki wa baa hizo hukata leseni katika mamlaka zinazohusika za biashara hiyo.
Biashara ya ulevi inaendeshwa katika maeneo mengi ya Unguja na Pemba ambapo hivi sasa kumekuwepo na utitiri wa vilavu vya pombe katika maeneo ya wazi, makaazi ya watu pamoja na karibu na sehemu za nyumba za ibada jambo ambalo kwa mujibu wa sheria hairuhusiwi kufungua baa katika maeneo kama hayo lakini baa hizo zimekuwa zikiendeshwa bila ya kufuata sheria za vileo.
Karibu asilimia 25% ya mapato yanayokusanywa na Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB) yanatokana na vinywaji vikali vya vileo pamoja na soda katika mahoteli ya kitalii Zanzibar na baa za mitaani.
Kama matukio ya uchomaji moto na uharibifu wa hoteli za kitalii utaendelea basi unaweza kabisa kuharibu mapato ya nchi ambayo yanategemea sekta ya Utalii ikiwemo vinywaji vya vileo.

Hatua hii ya kachoma mabaa ni ya kupongezwa kwa sababu zifuatazo:

1) Baa ni mahala salama kwa kuchochea uzinzi na madanguro na kusababisha UKIMWI kuenea kwa haraka!

2) Baa ni mahala wanapokutana majambazi na wezi na hapo ndipo mikakati ya uhalifu husukwa!

3) Baa hukutanisha mafisadi papa na nyangumi!

4) Baa huchangia sana kuharibu Afya ya Binaadamu kwa kulewesha watu na kuchangia maendeleo ya jamii kudorora!

5) Baa huchangia kuharibu maadili na utu wa binaadamu kwa kuuza pombe na kusababisha walevi wachafue mazingira kwa kukojoa ovyo barabarani!

6) Baa husababisha ajali za barabarani kwa mlevi kuendesha gari na kusababisha roho za watu kupotea!

7) Baa husababisha umasikini kwa mlevi kutumia fedha zake kwa pombe badala ya kununua chakula kwa familia yake!

8) Baa husababisha mifarakano ya familia na kusababisha talaka!

9) Baa ni mahali pa ugomvi na vita visivyokuwa na msingi!

10) Baa unaweza kujipatia pombe na hata madawa ya kulevya na mengi machafu!

Kama Wazanzibari wameanza kuchoma moto baa na madanguro ya walevi, basi ni tendo la kuungwa mkono na kila mwenye kuwatakia mema ndugu zetu wa huko! mimi nadhani hatua hii imechelewa kuchukuliwa kwani ilitakiwa ianze siku nyingi!

Nashindwa kuelewa ni vipi Ukristo unahusishwa na Pombe wakati BIBLIA inakataza unywaji wa Pombe?

Usiwe miongoni wanywao pombe!

mithali 23:20

Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;miongoni mwao walao nyama kwa pupa

kwa maana mlevi na mlafi huingia umasikini!

na utepetevu humvika mtu nguo

mith 23: 30

ni nani aliye na macho mekundu?

niwale wakaao sana kwenye mvinyo waendao kutafuta divai iliyochanganywa!

usitizame mvinyo iwapo ni nyekundu mwisho wake huuma kama nyoka macho yako yataona mambo mageni na moyo wako utatoa yaliyopotoka!

Hivyo sio Uislamu peke yake unapiga vita pombe bali hata Ukristo umeharamisha Pombe bali viongozi wa Dini ndio wameruhusu kwa ulafi wao!

Angalia madhara ya pombe:

Long-term effects of alcohol - Wikipedia, the free encyclopedia

Mwisho nashauri hatua kama hiyo ya kuchoma Baa za pombe pia zianze Tanzania Bara kwani Pombe na Baa zimezagaa kama uyoga! na Changudoa na ukimwi umekuwa donda ndugu! Tuanze kuchoma Baa zote zilizoko maeneo wanaoishi familia zenye watoto na wanafunzi ili kupunguza vichocheo!!!!

jaribu kutembelea ujerumani,polland au marekani. tatizo lako ww ni kutotoka nje ya bongo ili uwe na mawazo mapana.gnite

Tabia ya kuchoma moto baa katika vitongoji vya Zanzibar haijaanza jana wala leo, ipo kwa muda mrefu tu! Zaidi ya uchomaji wa baa pia kuna uchomaji wa makanisa, uchomaji wa maduka ya pombe n.k Kuna wakati katika mtaa wa Darajani na barabara ya Benjamin Mkapa wasichana waliokuwa wamevaa suluali walichezea bakora za kutosha.

Ukiangalia historia ya baa na unywaji wa pombe katika Zanzibar, unaweza kushangaa kwa tabia hii ambayo sasa inazidi kuota mizizi. Wengi wanakumbuka kuwa Zanzibar iliwahi kuwa na kiwanda cha pombe kali kule Mahonda, hii iliweza kufanyika tu kutokana na kuwa serikali ilikuwa ikiangalia jinsi ya kupata mapato zaidi ya kuendekeza utashi katika imani fulani.

SMZ haina dini, na Zanzibar sio nchi ya kidini, hata hivyo hakuna shaka yoyote juu ya hujuma mbalimbali zinazofanyika huko kuchochewa na hao viongozi wa SMZ.

Hapo kwenye RED unatakiwa umalizie na neno ambao ni wanaCCM

Where is religious tolerance? Hamad na CUF wapo wapi? Tunaomba Opinions...
Hivi tuwaulize jamani, kuna dini ya kweli inayotetea ulevi na ufedhuli, hakuna zaidi ya dini ya uislamu- UISLAMU UNACHUKIA MAOVU NA UNAAMRISHA MEMA TU.... sisi wanzanzibari kama jamii ya kiislamu tuna haki zaidi ya kutunza mila na silka za jamii pamoja na kuheshimu tamaduni zetu UKIWEMO UISLAMU. hatuwezi kuuacha umma wetu upoitee eti kwa kuwafurahisha watu fulani. hatupo kuridhishana......... maovu ya wachache yawe kero kwa walio wengi. NASEME MUACHE KUSEMA MAMBO AMBAYO YAANAUDHI NA KUAMSHA MIHEMKO ITAKAYOPELEKEA CHUKI KATIKA JAMII. HATUTAKI WATOTO WETU WAWE WALEVI KAMA NYINYI............UPO!

Back
Top Bottom