Hili la wazanzibari kuchoma baa limekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la wazanzibari kuchoma baa limekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by samirnasri, Feb 5, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya ITV leo usiku jumla ya baa tatu zimechomwa moto na watu wasiojulikana ndani ya wiki moja. Inavyoonekana watu hawa wana mpango wa kumaliza baa zote huko zanzibar.

  Wamiliki wa baa hizo mmoja anaitwa john na mwingine christopher ni wakristu. Inavyoonesha wachomaji wa baa hizo watakua waislamu ambao imani yao inapingana na pombe japokua baadhi yao ni wateja wazuri na wanatumia hata yule mdudu maarufu kama mbuzi mkatoliki. Katiba yetu inatoa uhuru wa kuabudu na kuheshimu uhuru wa kuabudu wa watu wengine.

  Kila mtu akianza kuharibu kitu kinachopingana na imani yake watu si wataanza kuchoma misikiti na makanisa?? Zanzibar sio religious state bali ni secular state..
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mi naona sawa tu maana hivi Bar zimejaa kila kona ya nchi mpaka kwenye sehemu za kuishi watu, utakuta mtu anafungua Bar karibu ya shule, Kanisa na Msiki. Hii Tabia inazidikukuwa maana hakuna serikali inayofuata sheria ufisadi kila kona. Yanahitajika mapinduzi kama ya Tunisia au Misri
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa mkuu hilo nitatizo tena tatizo kubwa, lakini hawa jamaa hawakuamka tu na kufungua hizo baa lazima wana vibali vya kufanya hizo biashara!!! Tuna mahakama ambazo mnaweza kuomba uhalali wa hiyo baa kuwa hapo kwa mujibu wa sheria uangaliwe, lakini sio kujichukulia sheria mkononi.... Kama kila mtu akianza kujichukulia sheria mikononi tutafika wapi :twitch: ?????
   
 4. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kwa nini mtu alazimishwe kutokunywa pombe. Mambo ya dini ni mtu na Mungu wake. Kama nakunywa pombe wacha nihukumiwe na Mungu lakini siyo mwanadamu. Hili la kuchoma Bar ni kosa la jinai ambalo linatakiwa kulaaniwa na kila mtu. Mbona waislamu kunakunywa nao kila siku jamani?
   
 5. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Unaongelea Zanzibar kweli!!!?
   
 6. M

  Mwera JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza we mtoa mada badili jina halafu ndio utetee mapombe,ushindwe na ulegee!
   
 7. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,228
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Stereotype illusion...km kosa kafanya mtu mmoja sioni sababu ya uzanzibari,na km aliyefanyiwa ni John pia sina hakika km mhalifu alilenga watu wa dini fulani....wakuu tuchunge sana hukumu za kiujumla!...km kosa kafanya Rutashobya haitoshi kusema "wahaya ndivyo walivyo..." likewise kofi moja la bwana Mwita halitoshi kusema " Wakurya ndivyo walivyo"...tuchunge sana kauli hizi!
   
 8. c

  chamajani JF-Expert Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Safi sana, zinazidisha vitendo viovu kwa jamii, ni vigenge vya kupanga uovu tu kwa jamii ya wazanzibari even tanganyika nadhani kampeni hii pia izinduliwe Tanganyika-Support 100% yachomwe yote!
   
 9. n

  niweze JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Where is religious tolerance? Hamad na CUF wapo wapi? Tunaomba Opinions...
   
 10. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #10
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati kama huu ndipo huwa natamani ningekuwa mzanzibari.

  Saafi sana wazanzibari endeleeni na moyo huo huo.
   
 11. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Tatizo siyo mabaa ambayo yako kwenye sehemu zake zinazostahiki, yaani mahotelini, beach na kadhalika. Tatizo liko kwenye mabaa yanayofunguliwa ovyo kwenye maeneo ya watu (residential areas). Nimesikia kwenye redio wananchi wamelalamika kwenye hayo mamlaka ya leseni na vinywaji without success, ndiyo maana wamechukua hatua mikononi mwao.

  Baa zilikuwepo tangu enzi ya mkoloni lakini hakukuwa na nakama hii ya sasa.
   
 12. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Are you Serious...:twitch:
   
 13. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Bar zingeongeza kodi kwa Serikali na kisha Serikali ingefanikisha kuanzisha na kusimamia mahakama ya Kadhi...

  Sasa wanavyozichoma je Serikali itapata wapi pato la kuanzisha na kuongoza mahakama hii jamani?
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Zanzibar sifahamu kulivyo, lakini miji ya bara biashara ya bar inakera. Baa zinarudisha nyuma maendeleo. Inatakiwa kodi ya uendeleshaji mabar iwe juu sana na kuhimiza maduka ya rejareja watu wanunue na kunywea majumbani kama wenzetu wafanyavyo.

  Bei ya bia ikiwa juu mno kwenye mabaa watu watalazimika kununua bia na kunywea majumbani hapo ulevi utapungua. Halafu watoa leseni hawaangalii kama sehemu kuliko mabaa ni makazi ya watu hivyo ni kuleta usumbufu kwa watu wenye familia.
  Sheria za mabaa ni kwamba yawe mbali na makazi ya watu, mbali na nyumba za kuabudia, mbali na huduma za umma kama mahospitali nk. mbali na shule.

  Lets stay sober
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Tabia ya kuchoma moto baa katika vitongoji vya Zanzibar haijaanza jana wala leo, ipo kwa muda mrefu tu! Zaidi ya uchomaji wa baa pia kuna uchomaji wa makanisa, uchomaji wa maduka ya pombe n.k Kuna wakati katika mtaa wa Darajani na barabara ya Benjamin Mkapa wasichana waliokuwa wamevaa suluali walichezea bakora za kutosha.

  Ukiangalia historia ya baa na unywaji wa pombe katika Zanzibar, unaweza kushangaa kwa tabia hii ambayo sasa inazidi kuota mizizi. Wengi wanakumbuka kuwa Zanzibar iliwahi kuwa na kiwanda cha pombe kali kule Mahonda, hii iliweza kufanyika tu kutokana na kuwa serikali ilikuwa ikiangalia jinsi ya kupata mapato zaidi ya kuendekeza utashi katika imani fulani.

  SMZ haina dini, na Zanzibar sio nchi ya kidini, hata hivyo hakuna shaka yoyote juu ya hujuma mbalimbali zinazofanyika huko kuchochewa na hao viongozi wa SMZ.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Baa Zanzibar hazifunguliwi hovyo hovyo, kuna Mahakama ya ulevi ambayo ndio inasimamia leseni zote za huduma za ulevi visiwani humo. Mahakama hii awali ndio iliyokuwa ikitoa hata leseni ya mtu kunywa bia visiwani humo miaka ile ya 47. Mahakama hii ufanya kazi yake mara moja kwa mwaka, ambapo hupitia maombi mapya ya ufunguaji wa baa na maduka ya ulevi, kufuta leseni za baa, na kuendeleza(renew) leseni za baa.

  Hata ukiangalia master plan ya wachina ya mwaka 1982 iliyotiliwa sheria ya ardhi ya mwaka 1985, hakuna maeneo yanayoenyeshwa kuwa ni kwa ajili ya baa pekee.

  Zaidi pamekuwepo na ongezeko kubwa la waakazi katika visiwa hivyo, hii inasababisha kuwepo na mahitaji zaidi ya huduma mbalimbali karibu nao, mojawapo ikiwa hii ya baa.
   
 17. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu;
  Kwa mujibu wa yule victim wa Mji mkongwe wakati anahojiwa na mwandishi wa Channel 10, mkabala ba bar yake kuna Bar na danguro la Mzanzibar ambala halikuchomwa!! kwa nini tusiamimi kuwa hujuma hiyo ni kwa Wabara walioko Zanzibar?
   
 18. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  waache unafki hao Wazanzibari mbona hawachomi moto hoteli za kitalii zinazouza pombe na nyama ya nguruwe pia? au uadui wao upo kwa Wazanzibari/Wabara wenzao wenye mabaa?
   
 19. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,890
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  nashangaa,wanakusanya kodi kwenye hotel zinazouza bia!
   
 20. M

  Mtwike Senior Member

  #20
  Feb 6, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Isijekuwa wanaripua makanisa kwakuwa mna Diva!i
   
Loading...