Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu wana-JF kama mtakubuka ndugu Emanuel Olenaiko amekuwa Mkuu wa uendeshaji na baadaye Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha uwekezaji TIC kwa miaka mingi sana. Na amehusika kutoa leseni kwa makampuni/wawekezaji mbalimbali hapa Tanzania wakiwamo Barrick/Acacia.
Sasa kitendo cha kuajiriwa na Acacia/Barick kama Executive director anayeshughulikia mahusiano na serikali kinaleta ukakasi. Ni lazima itungwe sheria kali kuzuia hawa maafisa wakuu wa serikali kuajiriwa na makampuni waliyokuwa wanayasimamia katika utekelezaji wa sheria.
Kama Ole Naiko alikuwa mtumishi/wakala wa serikali katika kuingia makubaliano, je kwa sasa si ni hatari katika kipindi ambacho tunaenda kwenye majadiliano na Acacia/Barrick ambapo atatumika kutoa taarifa za ndani/siri za serikali zitakazotumika kutunyima fursa ya kuwa na nguvu katika majadiliano?
Ifike wakati Emmanuel Ole Naiko aondoke Barrick/Acacia ili kulinda maslahi ya serikali na nchi ya Tanzania. Ujumbe huu naomba usambazwe hadi aupate leo leo kisha usiku wa leo aondoke mwenyewe.