Hili la Ole-Naiko kuwa Executive Director wa Acacia baada ya kustaafu TIC limulikwe

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu wana-JF kama mtakubuka ndugu Emanuel Olenaiko amekuwa Mkuu wa uendeshaji na baadaye Mkurugenzi mkuu wa Kituo cha uwekezaji TIC kwa miaka mingi sana. Na amehusika kutoa leseni kwa makampuni/wawekezaji mbalimbali hapa Tanzania wakiwamo Barrick/Acacia.

Sasa kitendo cha kuajiriwa na Acacia/Barick kama Executive director anayeshughulikia mahusiano na serikali kinaleta ukakasi. Ni lazima itungwe sheria kali kuzuia hawa maafisa wakuu wa serikali kuajiriwa na makampuni waliyokuwa wanayasimamia katika utekelezaji wa sheria.

Kama Ole Naiko alikuwa mtumishi/wakala wa serikali katika kuingia makubaliano, je kwa sasa si ni hatari katika kipindi ambacho tunaenda kwenye majadiliano na Acacia/Barrick ambapo atatumika kutoa taarifa za ndani/siri za serikali zitakazotumika kutunyima fursa ya kuwa na nguvu katika majadiliano?

Ifike wakati Emmanuel Ole Naiko aondoke Barrick/Acacia ili kulinda maslahi ya serikali na nchi ya Tanzania. Ujumbe huu naomba usambazwe hadi aupate leo leo kisha usiku wa leo aondoke mwenyewe.
 
Mnaenda kwenye majadiliano yapi na nani..??

Mleta uzi unafahamu kweli kinachoendelea kwenye hii kesi ya ACACIA na serikali??

ACACIA wameshasema baada ya kupelekewa credit note na TRA kuwa hawalitambui deni and so hawalipi.
Sasa mnaenda kujadiliana na nani Mkuu..??

Fatilia taarifa zipo hapa thread za jana.
 
Hizo ni press release, tunachokijua ni kuwa Acacia kupitia mkuu wao waliahidi kukutana na serikali. Naona wewe unaendeleza siasa kwenye masuala ya msingi. Usizungushe mikono,tulia.
 
Hizo ni press release, tunachokijua ni kuwa Acacia kupitia mkuu wao waliahidi kukutana na serikali. Naona wewe unaendeleza siasa kwenye masuala ya msingi. Usizungushe mikono,tulia.
Hahahahaahhahahhahahaha..
Wala usibadilike Mkuu... Endelea kuwa ivyo ivyo kama jiwe kwa haya matumaini yenu ya kulipwa hayo Matrilioni hewa..
Dunia nzima toka jana inawacheka.
 
Kama ndivyo,kwa nini mmewapelekea bill kabla ya mazungumzo?,tulizeni mishono hao wenzenu vichwa hawafugii nywele.
Kweli adui wa maendeleo ya Tanzania ni Mtanzania.....kwa sababu Raisi anaongoza mapampano tunategemea kabisa tutakuwa na vibaraka wa wakoloni katikati yetu, tutawashinda.
 
Mnaenda kwenye majadiliano yapi na nani..??

Mleta uzi unafahamu kweli kinachoendelea kwenye hii kesi ya ACACIA na serikali??

ACACIA wameshasema baada ya kupelekewa credit note na TRA kuwa hawalitambui deni and so hawalipi.
Sasa mnaenda kujadiliana na nani Mkuu..??

Fatilia taarifa zipo hapa thread za jana.
Kwani ile notice iliishia wapi ya kwenda london kwenye mahakama ya usuluhishi??
 
Aisee kumbe ukitokwaga na povu unakuwa kituko cha karne...
Endelea kusubiri Matrilioni hewa.
Rais mwenyewe anasema wazi kuwa Tanzania kila kitu hewa: watumishi hewa, wanafunzi hewa, vyeti hewa, matrilioni hewa...kasoro kimoja, labda vichwa vya walio wengi, havina hewa bali vichwa maji...
 
Rais mwenyewe anasema wazi kuwa Tanzania kila kitu hewa: watumishi hewa, wanafunzi hewa, vyeti hewa, matrilioni hewa...kasoro kimoja, labda vichwa vya walio wengi, havina hewa bali vichwa maji...
upinzani hewa.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom