Hili la Nchimbi Butiama limekaaje?

Hili la Nchimbi Butiama limekaaje?

Mnafiki! huwezi kumtenganisha JK na Lowassa hata kidogo, kukubali kuwa wewe ni CCM na kuwagawa hawa wasafi na hawa wachafu...hutafiki mbali

hakuna msafi CCM si wewe si bosi wako Membe na mjomba wako Kikwete!

Aibu!!!

Hizo blanket accusations zako dhidi ya JK bila kuwa na hoja ambazo mimi na watu wa aina yangu zitatubaidilisha msimamo au mtazamo wetu hazikupi heshima na kinyume chake unaonekana ni mtu ambaye anaendeshwa zaidi na chuki . Kila siku tumekuwa tuki-demand tuambiwe uchafu wa JK au hata huyo Membe lakini stori zinazokuja hapa ni kwamba wanajipanga kwa 2015. Wewe ambaye unasema Lowassa na Kikwete ni one and the same ndiye mwenye onus ya kuthibitisha hilo maana matendo ya Lowassa yanafahamika kwa ushahidi na hatujafika hatua ya kumuona hivyo kwa hisia au kwa kukurupuka.

Mimi nimekuambia kwamba sijawahi kuwa CCM wala chama chochote cha siasa and I am happy this way. Lakini siwezi kuingia kwenye fashion ya kudhani kuitukana CCM pasipostahili na kuisifia CDM pasipostahili ni uzalendo. Upumbavu uitwe hivyo unapostahili na hivyo hivyo ustaarabu. Kwa vile wewe unawiwa na allegiance ya chama chako, ndio maana kila wakati unajikuta ni mateka wa kushabikia kila linalofanywa na chama chako na hivyo hivyo kuponda kila linalofanywa na chama pinzani na chako. Grow up man!
 
Kwa kweli ninasikitika sana kwa watu kuitumia vibaya jamii forums kulisha maneno watu wengine
1.nchimbi hajapata kusema mahali popote wala kulalamikia kwa familia ya Mwalimu Nyerere kutohudhuria.

2.Shughuli ya kumuenzi Mwl Nyerere itaendelea kuwepo hata kama hakuna mjukuu wake butiama.nyerere si mali ya familia ni mali ya watz wote
3.Kwani miaka mia baadae wakati familia yake haitakuwepo watu hawatakuwa wanaenda tena Butiama ama itakuwaje
4.Nani kasema kuwa nchimbi hana analoweza,hata kuweza kukaa ktk siasa kwa muda mrefu pia ni kujua jambo.

End of the day mwanasiasa makini ni yule anaeweza kudumu ndani ya siasa.kumsaidia Membe kuwa rais wala sio kumsifu kwa kwenda butiama na kupokelewa huko....Wizara ya Nchimbi itakuwa tena tar 14 kuwasha mwenge ni wazi kuwa kama ni muhimu hao watu na atawaalika
 
Serikali ya CCM kama inafikia mahala wanainyima familia ya Mwalimu Nyerere maji mpaka Mb Mkono alalamike bungeni au barabara kuwa na mashimo kuliko kawaida au kuwanyima umeme unadhani watawakumbuka kwenye sikuukuu,zaidi zaidi wanatumia jina la Mwalimu Nyerere period hawana shida wala hata na heshima yeyote siwangejenga jengo la Mwalimu Nyerere Foundation liko wapi umeliona mahala
 
2015 ni lazima CCM imegeke tu! Just like Mwalimu said! and we will be there waiting.
 
JAMBO LA MUHIMU NI CCM KUFA NA KUZIKWA NA KILA BAYA LINALOFANYWA NAO NI FAIDA KUBWA KWETU NAOMBA WAENDELEE KUFANYA MAKOSA HAYO HAYO ILI WATANZANIA WAUJUE UKWELI NA UKWELI UWAWEKE HUrU
 
Kwanza nampongeza mhe.Dr.Nchimbi kwa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika huko Butiama kupitia Wizara yake lakini asikatishe tamaa na watu wanaoingiza siasa ktk shughuli zake kiwizara.Pia ana fursa nzuri ya kujijenga wakati wa UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU ijumaa 14/10/2011 huko Butiama ambapo wizara yake itasimamia shughuli hiyo.Mwisho mhe jiandae kupambana urais 2015 maana vijana tunataka nchi hii iongozwe na vijana either wewe Nchimbi,zitto au kijana mwingine.
 
Kwa kweli ninasikitika sana kwa watu kuitumia vibaya jamii forums kulisha maneno watu wengine
1.nchimbi hajapata kusema mahali popote wala kulalamikia kwa familia ya Mwalimu Nyerere kutohudhuria.

2.Shughuli ya kumuenzi Mwl Nyerere itaendelea kuwepo hata kama hakuna mjukuu wake butiama.nyerere si mali ya familia ni mali ya watz wote
3.Kwani miaka mia baadae wakati familia yake haitakuwepo watu hawatakuwa wanaenda tena Butiama ama itakuwaje
4.Nani kasema kuwa nchimbi hana analoweza,hata kuweza kukaa ktk siasa kwa muda mrefu pia ni kujua jambo.

End of the day mwanasiasa makini ni yule anaeweza kudumu ndani ya siasa.kumsaidia Membe kuwa rais wala sio kumsifu kwa kwenda butiama na kupokelewa huko....Wizara ya Nchimbi itakuwa tena tar 14 kuwasha mwenge ni wazi kuwa kama ni muhimu hao watu na atawaalika

Hii uliyojiingiza nayo huifahamu. Kama huwezi kutambua kwamba familia ya Mwalimu ina mchango na katika hili walistahili kujulishwa kama wenyeji basi liko tatizo la uwezo wa kufikiri hapa. Kukaa muda mrefu kwenye siasa wakati mwingine kunaweza kuwa ni kwa sababu yuko politically correct na siyo kutokana na kujua mambo. Wote tunafahamu kwamba Nchimbi hafanani na elimu anayosingizia kuwa nayo maana hata ukizungumza naye kwa muda mfupi unajua kwamba hiyo advanced diploma ya IDM ndicho kitu pekee alichokipata na bado anashindwa kuitumia. Ikifikia mahali hata Nchimbi anafikiriwa kwenye urais wa nchi hii basi nadhani tumelogwa na namna nzuri sasa ni kuandamana kushinikiza wakoloni warudi kutunyoosha. Nchimbi ni masquarader ambaye hata kuandika speech ya kiingereza ya nusu ukurasa ni mgogoro halafu eti ana Phd. A big shame.
 
Huyu nchimbi ni bonge la kilaza huku songea hatuna umeme wiki ya pili ye anakula bata ndiyo maana Mungu kamlaan kampa masikio madogo sana kama ya kenge
 
Mtanisamehe wana jamvi najua mnataka kusikia nitasemaje kuhusu hili ila mimi nina list ya watu ambao siwezi wajadili kabisa

1.Nape
2.Nchimbi
3.JK
4.Wassira
5.Lukuvi na wengine wanaongezeka kila siku sasa Msechu etc
 
Mnafiki! huwezi kumtenganisha JK na Lowassa hata kidogo, kukubali kuwa wewe ni CCM na kuwagawa hawa wasafi na hawa wachafu...hutafiki mbali

hakuna msafi CCM si wewe si bosi wako Membe na mjomba wako Kikwete!

Aibu!!!
Huyu nchimbi upeo wake wakufikiri ni mdogo saana.Amesoma kwa kuungaunga tu na mpake leo hajatuambia Phd yake kama ni halali au la.Tatizo langu na nchimbi nikuwa na uelewa mdogo katika mambo hata ya kawaida kabisa.
 
Labda ni Jk tu aliyemteua, anayehisi kuwa nchimbi kakomaa. Mi nakumbuka tulikuwa wote alifukuzwa form two kwa kitu kidogo tu cha kitoto, nilidhani sasa amekomaa, kumbe bado
 
Pamoja na kwamba kuendeshwa na ideologies za CCM si jambo la aibu kiasi cha mtu kulikwepa, mimi siyo mwanachama wa CCM na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote. Lakini kwenye masuala ya kitaifa issues za chama zinakuja baadae. Huwezi kunitarajia kumuunga mkono Lowassa (hata kama angekuwa hagombei urais) wakati najua kwamba huyu bwana ni mchafu na ni mtu ambaye ni adui kwa ustawi wa mtanzania maskini. Na wala huwezi kumfananisha JK na Lowassa, kwa matendo na itikadi kwa sababu unapozungumzia maadili JK yuko kushoto na Lowassa yuko kulia. Labda unachosema wewe ni kwamba dhambi ya JK ni kuwateua hao wawili. lakini kuwateua ni kuwatuma wakatende mabaya waliyoayatenda? Mbona wengi wa wateule wake wengine ni waadilifu? Sijutii kusifia yale mema yanayofanywa na JK hata kama kufanya hivyo ni kuonekana mana CCM.

Unapozungumzia suala la 2015 na kunihusisha mimi na harakati hizo, unaingia kwenye mkubo wa watu wanaodhani kwamba kusifia jema ni kumfagilia mtu kwa 2015 na kukemea maovu ni kumvurugia mtu kwa 2015. Hilo hatuwezi kulikubali maana linatufanya tuwe wanafiki na waoga wa kutoa maoni ya wazi na ya kweli kwa hofu tu ya kuonekana tunampinga mtu kwa sababu ya ambition zake. Juu ya wewe kudai Nchimbi ni sawa na wengine, then hiyo ni self defeating kwa sababu mbona Waziri wa CCM aliyefuata hakufanya madudu kama hayo? Labda wewe mwenzangu umewekwa kwenye mtego wa kupenda chama chako kuliko nchi, au kupenda mtu kuliko nchi ndo maana mada zako zinaangalia mtu kuliko hoja.

Bahati nzuri sana nipo huru na sifikirii "kiitikadi" sina interest na chama chochote na wala sifikirii kufanya kazi chini ya serikali inayoendeshwa na CCM hata siku moja. The 2015 fever ni juu yenu nyie wenye maslahi of who will be who ndani ya CCM. The only interest I have in 2015 ni kuiona CCM inashindwa na kuondoka madarakani. With that I will support anyone, any party or independent who can make that dream come true.

CCM na serikali yake is a completely failure na kama hukubali hili basi you are living in a denial and total delusional. Sasa haiwezekani ndani ya hiyo failed project eti kiongozi wake akawa powa ila some subordinates hapana. Waziri huyo huyo unayesema hakufanya madudu kama ya Nchimbi tumemshuhudia aki-flip flop kuhusu uhalali wa NTC kule Libya.
 
Mi sikubaliani na generalization ya kaka yangu Mbopo, you are wrong kutuambia kwamba CCM ina watu wanaofanya makubwa mengi, wakina nani? CCM na serikali yake ni janga la kitaifa, JK hawezi lolote bahati yake ni kwamba anatawala watu wapumbavu ama sivyo ukikaa kufikiria ni nini hasa kinachoendelea, kama si kwa hii insanity tuliyonayo wote sisi ama tungekua tumeshauawa na askari wake ama tumesha commit suicide, huyu bwana mwenyewe ni janga la kitaifa, si muungi mkono Lowassa kwa sababu mimi ni kundi la wale tunaoamini kwamba katika nchi ya watu 43 m there is life beyond JK na Lowassa, why settle for nicomcoups if there are angels out there? Japo ninachofahamu ni kwamba kama Lowassa being as vindictive as we are told he is, basi ntampigia kura ili aje atu komeshee huyu bwana JK na vizazi vyake.
 
Hivi na Membe alipoenda na mabalozi waliwasiliana na familia ya Nyerere? familia ilikuapo?
 
Hizo blanket accusations zako dhidi ya JK bila kuwa na hoja ambazo mimi na watu wa aina yangu zitatubaidilisha msimamo au mtazamo wetu hazikupi heshima na kinyume chake unaonekana ni mtu ambaye anaendeshwa zaidi na chuki . Kila siku tumekuwa tuki-demand tuambiwe uchafu wa JK au hata huyo Membe lakini stori zinazokuja hapa ni kwamba wanajipanga kwa 2015. Wewe ambaye unasema Lowassa na Kikwete ni one and the same ndiye mwenye onus ya kuthibitisha hilo maana matendo ya Lowassa yanafahamika kwa ushahidi na hatujafika hatua ya kumuona hivyo kwa hisia au kwa kukurupuka.

Mimi nimekuambia kwamba sijawahi kuwa CCM wala chama chochote cha siasa and I am happy this way. Lakini siwezi kuingia kwenye fashion ya kudhani kuitukana CCM pasipostahili na kuisifia CDM pasipostahili ni uzalendo. Upumbavu uitwe hivyo unapostahili na hivyo hivyo ustaarabu. Kwa vile wewe unawiwa na allegiance ya chama chako, ndio maana kila wakati unajikuta ni mateka wa kushabikia kila linalofanywa na chama chako na hivyo hivyo kuponda kila linalofanywa na chama pinzani na chako. Grow up man!

grow up??

huoni unavyorukaruka na kutapatapa? una ushahidi wa Lowassa kuwa fisadi, nani wa kumpeleka mahakamani? JK kama rais anafanya nini kuhusu hili?

mimi siyo CDM mkuu naona unachanganya mafuta na maji, I have never liked CDM but I always hate CCM!

Wewe ni CCM hata useme nini, hoja za JK kuwa ni mwizi ukipewa unafanya nini? mikataba ya madini yote ni JK, SONGAS ni JK ana share mle, IPTL nani aliingia mikataba ile? Richmond au Dowans source ya tatizo ni Lowassa..you must be joking! really , upofu umekupata mkuu kwa penzi lako kwa JK. for more than six years unayesema msafi hajafanya lolote la yeye kuonekana yuko kinyume na ufisadi...meremeta, kagoda, n.k hajaweza kutibu.EPA yeye ndiye chief architect wa maswala yote na Balal yuko hai majuu. Ukitaka ku-prove kuwa EPA ni JK kamuulize mkapa.

am I still young?
 
Hivi na Membe alipoenda na mabalozi waliwasiliana na familia ya Nyerere? familia ilikuapo?

Sijui kama aliwasiliano nao, lakini ukweli kwamba familia ilikuwepo na kuhudhuria inatoa picha kwamba familia ilihusishwa.
 
Nasikia kila anae utaka urais anajipendekeza huko Butiama ili wapate mzimu wa Nyerere
 
Back
Top Bottom