Hili la Nchimbi Butiama limekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la Nchimbi Butiama limekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbopo, Oct 12, 2011.

 1. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siku kadhaa zilizopita, waziri wa Utamaduni, Habari na Michezo alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha miaka 50 ya uhuru ambazo wizara yake iliamua kuziandaa kijijini Butiama. Katika sherehe hizo jambao moja lilikuwa dhahiri. Kwamba si mjane wa Hayati Baba wa Taifa, wala familia yake na hata ukoo wa Mwalimu waliokuwepo kwenye sherehe hizo.

  Ukizingatia kwamba madhumuni ya sherehe hizo kufanyikia Butiama ni kuenzi na kutambua mchango wa Malimu katika ukombozi wa nchi hii na yale yote mazuri tunayojivunia leo, suala la kukosekana kwa watu hao, ambao siyo kwamba ndiyo wenyeji wake, bali pia ni walengwa muhimu, kunaleta maswali mengi sana ambayo pengine yanaia dosari kubwa katika utendaji wa wizara hiyo na hasa Nchimbi binafsi.

  Taarifa tulizonazo ni kwamba Mama Maria alikuwa safarini Uingereza, wakati wanafamilia wengine walikuwa Dar na Musoma lakini kwa vile hawakuhusishwa walikaa kando. Kinachoshangaza ni kwamba Nchimbi huyo huyo analalamika kwamba familia hiyo ilimsusia sherehe hiyo na kusema kwamba kitendo cha wao kutokuwepo kwenye hafla hiyo na kuhudhuria kwa wingi kwenye sherehe ya wizara ya mambo ya nje siku chache baadae kinatafsiriwa katika jicho la kisiasa na uchaguzi wa 2015.

  Mimi naona kwamba Nchimbi aitake radhi familia hii na watanzania kwa kuwadhalilisha!
   
 2. T

  Tiote Senior Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Laiti wangejua tulivyochoka na huu upuuzi wa kuhusisha kila kitu na siasa za 2015, wasingeendelea kuimba singo hii. Mtu kayavuruga mwenyewe anaanza kuweweseka. Hivi watu hawa wanapendaje madaraka wakati hawana ukomavu?
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako mkuu Mbopo uko biased, ok Nchimbi is just a looser kwa tunaomfahamu tunashangaa hata hou uwaziri alipewaje. Lakini mkuu bosi wako Membe naye si alikuwa huko juzi juzi tu? Anywayz, nilisahau alikuwa na mabalozi hahaha ahahaha ahahaha ahahaha!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. m

  mudavadi Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni utovu wa nidhamu, uhuni na kukosa maadili. Yeye alidhani familia ile ni ya kuiburuza tu na kushadadia sherehe bila kupewa heshima. Hata mkuu wa nchi akitaka kwenda huwa anatoa taarifa ya muda mrefu na kupata ridhaa. Yeye alijiingilia tu kama anavyoingia jimboni kwakwe? Akome!
   
 5. b

  banyimwa Senior Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nadhani hukumuelewa Mbopo. Hoja hapa ni kwamba Nchimbi alikwenda kinyemela bila kuihusisha familia. Akakuta hakuna mwenyeji na badala ya kuomba radhi anaishutumu familia na kudai kwamba anahujumiwa. Membe alikuwa huko (sijui kama ni boss wa Mbopo anyway) na alikuwa na baraka zote za familia ambayo ilimpokea na kushiriki hadi mwisho halafu yule aliyekwenda kinyemelea anaanza kulia kwamba kuna foul play.
   
 6. n

  ndutu Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kajamaa kanajiona kamekomaa mara hii? Kiburi hiki kitammaliza kisiasa.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimemwelewa vizuri sana mkuu, nilichokiandika ndiyo lugha pekee wanayoielewa hawa watu wanaoendeshwa na ideolgies za CCM. Mbopo kwa sasa kazi yake kubwa ni ku-attack kila anayeonekana kuwa mshindani wa bosi wake 2015. Huko CCM kuna kazi nyie acheni tu. Ndiyo maana he's against Lowassa na Mashabiki wake lakini ni die-hard fan wa JK, hapa anampiga nyundo Nchimbi ambayo ni halali kabisa lakini ni die hard wa CCM. Principally huwezi hata siku moja kumuona JK ok lakini Lowassa hapana. Au Nchimbi hafai lakini JK juu. All in all hivyo ndivyo walivyo wanaCCM just kama Nchimbi.
   
 8. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Unajua mkuu, kati ya mawaziri mizigo wanaolishwa na walipa kodi wa nchii ni Nchimbi. What merits does this guy have to make him think he is more than any Tanzanian except his boss jk. He has never done good thing to this country zaidi ya kufikiri he is more iportant than others. Imagine unplanned event such as this eating taxpayers money namna hii alafu mtu anapanua domo lake linalonuka kuwa hakutendewa haki.Wametumia hela kiasi gani kwenye shere hiyo. Matumizi ya hovyo akabisa ya hela wakati wanaondolewa ofisini kwa kukosa kulipa hela za pango za nhc. Kweli Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu.
   
 9. w

  watenda Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sishangai. Suala la elimu yake bado lina utata mkubwa!
   
 10. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pamoja na kwamba kuendeshwa na ideologies za CCM si jambo la aibu kiasi cha mtu kulikwepa, mimi siyo mwanachama wa CCM na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote. Lakini kwenye masuala ya kitaifa issues za chama zinakuja baadae. Huwezi kunitarajia kumuunga mkono Lowassa (hata kama angekuwa hagombei urais) wakati najua kwamba huyu bwana ni mchafu na ni mtu ambaye ni adui kwa ustawi wa mtanzania maskini. Na wala huwezi kumfananisha JK na Lowassa, kwa matendo na itikadi kwa sababu unapozungumzia maadili JK yuko kushoto na Lowassa yuko kulia. Labda unachosema wewe ni kwamba dhambi ya JK ni kuwateua hao wawili. lakini kuwateua ni kuwatuma wakatende mabaya waliyoayatenda? Mbona wengi wa wateule wake wengine ni waadilifu? Sijutii kusifia yale mema yanayofanywa na JK hata kama kufanya hivyo ni kuonekana mana CCM.

  Unapozungumzia suala la 2015 na kunihusisha mimi na harakati hizo, unaingia kwenye mkubo wa watu wanaodhani kwamba kusifia jema ni kumfagilia mtu kwa 2015 na kukemea maovu ni kumvurugia mtu kwa 2015. Hilo hatuwezi kulikubali maana linatufanya tuwe wanafiki na waoga wa kutoa maoni ya wazi na ya kweli kwa hofu tu ya kuonekana tunampinga mtu kwa sababu ya ambition zake. Juu ya wewe kudai Nchimbi ni sawa na wengine, then hiyo ni self defeating kwa sababu mbona Waziri wa CCM aliyefuata hakufanya madudu kama hayo? Labda wewe mwenzangu umewekwa kwenye mtego wa kupenda chama chako kuliko nchi, au kupenda mtu kuliko nchi ndo maana mada zako zinaangalia mtu kuliko hoja.
   
 11. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchimbi siku chache zilizopita huko Songea alikimbia na sanduku la kura katika uchaguzi wa Meya. Asifikiri watu hawajui kinachoendelea, pamoja na madiwani wake kulalamika hachukui hatua zozote za kuleta muafaka kwenye hiyo Halmashauri.
   
 12. m

  mharakati JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nchimbi kadanganya PHD eti dakta halafu jitu kama hili linakua waziri. Huu ni ujinga unafanyika Tz tu nchi ya wananchi wajinga wanaokubali yote
   
 13. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Nchi Ya Kitu Kidogo
   
 14. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Well said mkuu. Mwenye macho haambiwi tazama. Thanx again.
   
 15. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  what is so special kwa familia ya nyerere? they are just a citizens. Sioni sababu ya wanasiasa kila siku kwenda kujikomba kwa ajili ya kutafuta popularity za kijinga. huu ni upuuzi aka porojo kama nyerere alivyowaambia waandishi wa habari
   
 16. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  serikali ya kisela hivo kila mtu anaamua kisela tu
   
 17. Painstruth

  Painstruth Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnafiki! huwezi kumtenganisha JK na Lowassa hata kidogo, kukubali kuwa wewe ni CCM na kuwagawa hawa wasafi na hawa wachafu...hutafiki mbali

  hakuna msafi CCM si wewe si bosi wako Membe na mjomba wako Kikwete!

  Aibu!!!
   
 18. m

  mkomavu Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yetu macho na masikio na mbio za 2015, tutasikia mengi na tutaona mengi
   
 19. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Nyerere ndie Abraham Lincon wa Tanzania ndie maana tunamuenzi huyo Nchimbi si akaenzi Monduli huko atakuta watu wengi tu wanamsubiri
   
 20. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Unaruhusiwa kufikiria hivyo lakini wenye akili watakwambia kwamba kifo cha Koplo na Jenerali vina uzito tofauti. Huyu Nchimbi alichagua kufanyia hiyo sherehe Butiama for obvious reasons na the reason why analalamikia kukosekana kwa familia hiyo ni kutokana na umuhimu wa familia hiyo. Mbona hajalalamikia familia ya Butiku, Mkono au Warioba na hata ya Kingunge? Kuibeza familia hiyo, tena kwa mambo yanayofanyika Butiama ni kuikana historia ya nchi hii na hilo linaweza kufanywa na watu ambao hawana kiu ya kujua tulikotoka.
   
Loading...