Hili la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kumtambulisha Diamond na Meneja wake likoje ?

Leo katika hafla ya usimikaji wa RADAR, nimeona jambo ambalo sikuelewa dhamira ya Mkuu wa Mkoa wetu ilikuwa nini. Amemtambulisha Diamond na meneja wake kana kwamba wana umuhimu mkubwa zaidi ya hata mawaziri kina JAFFO na KIGWANGWALA ambao walikuwepo.Nini tafsiri ya hili jambo?
Inamaana hujui umuhimu wa Mond au unamchukia?.
Huyo sasa hivi yuko kwenye kiwango cha kuitangaza nchi, kuna watu wengi sana hapa Duniani wameijua/wataijua TZ kupitia Mond.
Sema ndio hivyo Kibongobongo Fitna & Husda100%.
 
Washa king'amuzi cha Azam, tune channel namba 122. Halafu jikumbushe historia ya maisha ya Diamond Platinumz, kutoka kwenye kuiba cheni ya mama yake hadi sasa kuweza kumiliki TV, acha tu namna analipaisha jina la Tanzania katika tasnia ya muziki, acha tu anavyowalazimisha wageni kujifunza kiswahili ili waweze kuimba nyimbo zake, ukishayatafakari hayo bila shaka utajua kwa nini anapata heshima ya kutambulishwa. Usisahau pia kuwa ni muwakilishi wetu katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika huko Russia. Bila kusahau kuwa ndiye yeye pekee aliyepeperusha bendera ya Tanzania katika kombe la mataifa ya Africa.
Du!, Maboso hebu pata Coca baridi hapo kwa Mangi.
 
Leo katika hafla ya usimikaji wa RADAR, nimeona jambo ambalo sikuelewa dhamira ya Mkuu wa Mkoa wetu ilikuwa nini. Amemtambulisha Diamond na meneja wake kana kwamba wana umuhimu mkubwa zaidi ya hata mawaziri kina JAFFO na KIGWANGWALA ambao walikuwepo.Nini tafsiri ya hili jambo?
watajuana wenyewe hata akimtambulisha kila siku hiyari yao
 
Hata Kiba alikuwepo...ila hapendi show off....

Huyo Jaffo na Kigwangala wewe wanakusaidia nini.. !?
 
Leo katika hafla ya usimikaji wa RADAR, nimeona jambo ambalo sikuelewa dhamira ya Mkuu wa Mkoa wetu ilikuwa nini. Amemtambulisha Diamond na meneja wake kana kwamba wana umuhimu mkubwa zaidi ya hata mawaziri kina JAFFO na KIGWANGWALA ambao walikuwepo.Nini tafsiri ya hili jambo?
kwani hawana umuhimu , mtu anaitangaza nje ya nchi na kutoa ajira sio jambo dogo
 
Wa tz tunawivu wa ajabu mond mpen haki yake tu
Tusimuhukumu kwa mapungufu yake bado yuko katika foolsh age lakin ndio ka invest vya kutosha na ndio aneipeperusha bendera ya taifa katika maswala ya burudani

Ukifuata historia yake maisha anastahil na pia anajua kujitoa katika jamii
Miaka 27 bado unaita ni foolish age?...

Kazi tunayo kuifikia Tanzania ya viwonder
 
Kw
Washa king'amuzi cha Azam, tune channel namba 122. Halafu jikumbushe historia ya maisha ya Diamond Platinumz, kutoka kwenye kuiba cheni ya mama yake hadi sasa kuweza kumiliki TV, acha tu namna analipaisha jina la Tanzania katika tasnia ya muziki, acha tu anavyowalazimisha wageni kujifunza kiswahili ili waweze kuimba nyimbo zake, ukishayatafakari hayo bila shaka utajua kwa nini anapata heshima ya kutambulishwa. Usisahau pia kuwa ni muwakilishi wetu katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika huko Russia. Bila kusahau kuwa ndiye yeye pekee aliyepeperusha bendera ya Tanzania katika kombe la mataifa ya Africa.

Hivyo? ni kweli naye ni mwekezaji kwenye industyr ya muziki
 
hakika kuna watu hawajui kusoma alama za nyakati na humu kwny huu uzi nimewaona baadhi yao hakuna mwenye chuki na platinumz hapa tatizo ni consistency ya suala husika na unchokifanya je vinaendana? jambo ambalo linahusu ulizi wa nchi ww unarecognised presence ya mwana burudani kweli? je kuna mwingiliano wowote? Mond sawa amewekeza je ni mpaka kwenye radar na defence systems za nchi au wizara ya mambo ya ulinzi? Maana rada kawa kiasi kikubwa inashabihiana na na hayo mambo kuwepo sioni kosa coz inaonesha how far Mond ni mzalendo ila kumrecognise ndio shida. Mahali ambapo unaweza kutambua uwepo wake pamoja na mambo ya ujasiria mali sanaa na michezo and alike
 
Kushangilia kwa watu wa Lumumba kawaida yao huko mi sipo ila Diamond anaitangaza Tanzania vizur ilianza michuano ya CUF kapewa bendere siku chache zijazo anapeperusha FIFA world cup hadi hapo hujajua umuhimu wako hata kama anabebwa ukibebwa nawe jisapport ubebeke vizur sio yule alie pigiwa promo na mange mwisho wasiku hasisiki tena
 
Leo katika hafla ya usimikaji wa RADAR, nimeona jambo ambalo sikuelewa dhamira ya Mkuu wa Mkoa wetu ilikuwa nini. Amemtambulisha Diamond na meneja wake kana kwamba wana umuhimu mkubwa zaidi ya hata mawaziri kina JAFFO na KIGWANGWALA ambao walikuwepo.Nini tafsiri ya hili jambo?
Tafsiri yake ni kuwa Juliana Chonja akome kufuatilia fuatilia watu wenye network zao serikali kuu...
 
img-20170322-wa0000-jpg.732678

Mkwaju Ngedere huyo ni mtoto wa baba, anaweza fanya lolote, achilia mbali kumtambulisha yeyote..
 
Washa king'amuzi cha Azam, tune channel namba 122. Halafu jikumbushe historia ya maisha ya Diamond Platinumz, kutoka kwenye kuiba cheni ya mama yake hadi sasa kuweza kumiliki TV, acha tu namna analipaisha jina la Tanzania katika tasnia ya muziki, acha tu anavyowalazimisha wageni kujifunza kiswahili ili waweze kuimba nyimbo zake, ukishayatafakari hayo bila shaka utajua kwa nini anapata heshima ya kutambulishwa. Usisahau pia kuwa ni muwakilishi wetu katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika huko Russia. Bila kusahau kuwa ndiye yeye pekee aliyepeperusha bendera ya Tanzania katika kombe la mataifa ya Africa.
Tunashukuru kwa hiyo Biography nzuri sasa turudi kwenye mad.a husika tafadhali
 
Back
Top Bottom