Hili la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kumtambulisha Diamond na Meneja wake likoje ?

Mkwaju Ngedere

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
1,046
872
Leo katika hafla ya usimikaji wa RADAR, nimeona jambo ambalo sikuelewa dhamira ya Mkuu wa Mkoa wetu ilikuwa nini. Amemtambulisha Diamond na meneja wake kana kwamba wana umuhimu mkubwa zaidi ya hata mawaziri kina JAFFO na KIGWANGWALA ambao walikuwepo.Nini tafsiri ya hili jambo?
 
Makonda ametambulisha wageni wake wa mkoa wake
Mbarawa ametambulisha mawaziri wenzake
 
Washa king'amuzi cha Azam, tune channel namba 122. Halafu jikumbushe historia ya maisha ya Diamond Platinumz, kutoka kwenye kuiba cheni ya mama yake hadi sasa kuweza kumiliki TV, acha tu namna analipaisha jina la Tanzania katika tasnia ya muziki, acha tu anavyowalazimisha wageni kujifunza kiswahili ili waweze kuimba nyimbo zake, ukishayatafakari hayo bila shaka utajua kwa nini anapata heshima ya kutambulishwa. Usisahau pia kuwa ni muwakilishi wetu katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika huko Russia. Bila kusahau kuwa ndiye yeye pekee aliyepeperusha bendera ya Tanzania katika kombe la mataifa ya Africa.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom