Hili la JWTZ(Mabomu) kukaa katika makazi ya Raia linatatiza sana. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hili la JWTZ(Mabomu) kukaa katika makazi ya Raia linatatiza sana.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Feb 17, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Maeneo mengi yaliyopo ndani ya mji wa Dar es salaam inashangaza kumilikiwa na Jeshi la Wananchi mfano:Kigamboni(mwanzoni)i,Masaki,Mwenge (Lugalo),Mikocheni,Msasani,Kawe n.k haya ni maeneo yalipaswa kuwa makazi rasmi ya Wananchi.Tofauti yake ni kuwa Wananchi wanaishi nje ya Mji na jeshi linamiliki katikati huku maeneo yake mengi yakiwa wazi eti mara Range,oooh mess hatari kweli.Hili jeshi la ajabu huwezi kulinda Wananchi ukiwa katikati yao,hapo ni kuwa jeshi ndilo linalindwa na Wananchi.Ndio inawezekana kuwa wao ndio walitangulia kukaa kabla ya ukuaji wa Mji,lakini kwa usalama na "nature" ya kazi zao walipaswa KUHAMA na kuelekea nje ya Mji.

  Leo hii tunapoteza watu,kusababisha ulemavu wa Maisha na kuongeza umasikini kwa uzembe usiohitaji kujifunza kutokana na matukio (MBAGALA).Serikali mara ngapi itatoa fidia na kutumia gharama nyingi za kimaafa.

  Ebu tuache "SIASA" ni wakati sasa kwa JWTZ kuhama maeneo ya Raia na kuelekea nje kabisa ya mji,huko mtakuwa mmetunusuru.Kwa wote wanaopinga hili Mwenyezi Mungu atawaadhibu.
   
Loading...